Monday, April 18, 2011

WASHINDIWA 'SIKU YA UWEZO' WAKABIDHIWA HAKI YAO

Meneja Udhamini na Promosheni wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akimkabidhi hundi Yuda Joseph mfanyakazi wa dukani eneo la Kinondoni jijini kitita cha shilingi milioni kumi alichojishindia katika promosheni ya siku ya uwezo iliyoendeshwa na kampuni hiyo. Katikati anayeshuhudia ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kahude.
Mshindi wa promosheni ya siku ya uwezo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Yuda Joseph mfanyakazi wa dukani eneo la Kinondoni jijini akiwa ameshikilia hundi ya shilingi milioni kumi aliyokabidhiwa na Vodacom Tanzania baada ya kushiriki na kushinda kupitia promosheni hiyo.
Meneja Udhamini na Promosheni wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa, Mshindi wa promosheni ya siku ya uwezo inayoendeshwa na kampuni hiyo, Fadhil Felix, Mwanahabari Kambi Mbwana na Mtaala wa Masuala ya Habari  Matina Nkurlu wakiteta jambo mara baada ya kumkabidhi Felix hundi ya shilingi milioni kumi aliyojishindia kupitia hiyo.

Na Mwandishi Wetu.

Washindi saba kati ya 10 waliojishindia vitita vya shilingi milioni 10 kila mmoja katika promosheni ya ‘Siku ya uwezo’iliyochezeshwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania, mwishoni mwa wiki wamekabidhiwa hundi zao, baada ya kushinda shindano hilo.
Shindano hilo lilichezeshwa Aprili 4 mwaka huu, huku likiwataka wateja wao watume ujumbe mfupi wa maneno kuzungumzia malengo yao, endapo watafanikiwa kushinda Sh Milioni 10. Timu ya watendaji wa Vodacom Tanzania ikiongozwa na Meneja Udhamini na Matukio wa kampuni hiyo, Rukia Mtingwa, ilitembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, ili kujionea mazingira wanayoishi wateja hao walioshinda fedha hizo.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Rukia alisema kwamba ziara hiyo ya siku nzima, ililenga kujua mazingira wanayoishi wateja wao wote ikiwemo wale wa mikoani mara baada ya washindi hao kuingiziwa fe dha zao kwenye akaunti zao za benki. Alisema shindano la Siku ya Uwezo lilibuniwa ili kuleta changamoto na kutimiza malengo kwa wateja walioamua kujitolea na kushikiriki promosheni hiyo.
“Nimefurahi kuona mazingira tofauti ya wateja wetu ambao ni washindi wenye bahati ya Siku ya Uwezo ya Vodacom. Ni matarajio yangu washindi wetu watazitumia pesa hizi vizuri kama walivyoandika meseji zao, wakiainisha malengo yao endapo watafanikiwa kushinda,” alisema Mtingwa.
Washindi hao wenye bahati ni pamoja na Innocent Julius Tete (Mbezi Juu), Yuda Joseph Mang’anya (Kinondoni), Gaspary Kasimiry Kamina (Chang’ombe), Fadhiri Felix Gwabisaba (Yombo Kilakala), Kombo Ally Athuman (Kipunguni B Ukonga), Judith Peter Ruge (Mongolandege) na Ibrahimu Abdallah Msigwa
(Mbagala).
Kampuni ya Simu ya Mikononi ya Vodacom Tanzania, imekuwa ikichezesha promosheni mbalimbali kwa nia ya kuwawezesha wateja wao. Kupitia promosheni hii ya Siku ya Uwezo Zaidi, jumla ya wateja 10, waliibuka na ushindi huo. Kati ya hao miongoni mwao saba walitokea jijini Dar es Salaam wakati wengini ni wa mikoa ya Mwanza na Dodoma.

No comments:

Post a Comment