Thursday, April 21, 2011

MSAMA: MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA YAMEKAMILIKA 100%


Alex Msama - mkurugenzi MSAMA PROMOTIONS na mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha la pasaka

Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha kubwa la Pasaka, Alex Msama amesema kwamba maandalizi yote yamekamilika na wiki hii waimbaji kutoka nchi mbalimbali wataanza kuwasilini nchini.
Msama ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Msama Promotions, amesema kwamba wanamuziki hao wataanza kuwasili nchini Jumatano wiki hii tayari kwa ajili ya tamasha hilo litakalofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka Aprili 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
“Kwakweli hadi sasa kila kitu kimekamilika kwa ajili ya Tamasha la Pasaka, tunachosubiria kwa sasa ni muda na siku yenyewe tu ifike,” alisema Msama.
Tamasha hilo baada ya kufanyika jijini Dar es Salaam pia litafanyika mjini Dododma Aprili 25 na baadaye Mwanza Aprili 26.
Wakati huo huo, kwaya ya Kinondoni Revival Choir imethibitisha kushiriki kwenye Tamasha hilo la Pasaka ikunganana na waimbaji wengine.
“Yaap, Kwaya ya Revival imethibitisha kushiriki kwenye Tamasha la Pasaka… tunakuwa nao pamoja na waimbaji wengine, alisema Msama.
Tamasha la Pasaka la mwaka huu linawashikisha waambiji wote nyota wa muziki wa Injili wanaotamba nchini na pia wengine kutoka nyingine barani Afrika.
Waaimbaji watakaoshiriki kwenye Tamasha hilo ni pamoja na Rose Mhando, Boniface Mwaitege, Christina Shusho, Updeno Nkone, Faraja Ntatoba kutoka nchini DR Congo, Ephraime sekeleti kutoka Zambia na Anastazia Mukabwa kutoka Kenya.
Wengine ni Solomon Mukubwa, Geraldine Odour na Pamela Wandela wote kutoka nchini Kenya.
Pia katika kilele cha Tamasha hilo itazinduliwa albamu mpya ya muziki wa Injili ya Haleluya Collections Vol 5.
Albamu hiyo imeandaliwa na kusambazwa na Msama Promotions na malengo yake ni kusaidia watoto yatima na misaada kwa wanawake wajane.
Tamasha la Pasaka la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete.
Kwa mujibu wa Msama, Tamasha hilo baada ya kufanyika jijini Dar es salaam, pia litarindima kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 25.
Pia tamasha hilo litatibwirika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Aprili 26 mwaka huu ambayo itakuwa Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.
Pia fedha nyingine zitatumika kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mabomu yaliyotokea kambi ya JWTZ Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, Februari 16 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment