Saturday, April 9, 2011

BREAKING NEWSSSS: BENDI YA EXTRA BONGO YAPATA AJALI MAENEO YA MAGOMENI.

Bendi ya Extra Bongo imepata ajali mbaya maeneo ya Magomeni kwenye mataa katika makutano ya barabara za Kawawa na Morogoro na kusababisha majeraha kwa wanamuziki wa bendi hiyo, wakati walipokuwa wakirejea nyumbani baada ya kumalizika kwa onyesho lao lililokuwa likifanyika kwenye ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es salaam, usiku wa kuamkia leo. Mmoja wa Wanenguaji wa bendi hiyo anayejulikana kwa jina la Otilia akizungumza na FULLSHANGWE kwa njia ya simu, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema "Baada ya wanamuziki wenzangu kunishusha mimi nyumbani waliondoka huku wakisema nikiingia ndani niwaambie, lakini haikuchukua muda nilipoingia tu ndani nikapigiwa simu wenzangu wamepata ajali mbaya maeneo ya Magomeni Mikumi". FULLSHANGWE pia imewasiliana kwa jia ya simu na Mkurugenzi wa Bendi Kamalade Ally Choki hiyo akiwa katika hospitali ya Muhimbili, ambapo amesema Majeruhi wapo katika Hospitali hiyo kwa matibabu zaidi na baadhi wamepata majeraha kwa ndani , kwa sasa wanaendelea kuchunguzwa zaidi ili kuona wamejeruhiwa kwa kiwango gani. Hii ni ajali ya pili baada ya ile ya Mkoani Morogoro iliyoteketeza wanamuziki 13 wa kundi la Five Star Molden Taarab na kujeruhi wengine .

No comments:

Post a Comment