b..

B1

Wynem

animation

Sunday, April 10, 2011

Geraldine Odour, Faraja wathibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka


Faraja Ntaboba
Geraldine Odour

Na Mwandishi Wetu
WAIMBAJI wa muziki wa Injili, Geraldine Odour kutoka nchini Kenya na Faraja Ntaboba wa nchini DR Congo wamethibitisha kushiriki katika tamasha kubwa la Pasaka litakalofanyika Aprili 24 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Msama Promotions, amesema kwamba wanamuziki hao wamekubali kushiriki katika tamasha hilo.
Faraja anatamba na albamu ambaye anatamba na albamu ya Yupo Mungu atashiriki katika Tamasha hilo litakalfanyika katika mikoa mitatu, Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.
Kwa upande wake Geraldine Odour pia ameshiriki katika albamu ya Haleluya Collection Vol 5 na akiwa na wimbo wake wa Ndoto Yangu.
Kwa mujibu wa Msama Geraldine pia atashiriki kwenye Tamasha hilo katika mikoa yote ya Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza.
Tamasha la Pasaka la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete.
Tamasha hilo baada ya kufanyika jijini Dar es salaam, pia litarindima kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 25.
Pia tamasha hilo litatibwirika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Aprili 26 mwaka huu ambayo itakuwa Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.
Pia fedha nyingine zitatumika kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mabomu yaliyotokea kambi ya JWTZ Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, Februari 16 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment