Thursday, April 14, 2011

Q-JAY AAMUA KUOKOKAJOSEPH KELVIN 
            Mkali wa RnB nchini Tanzania ,Joseph Kelvin Mapunda aka Q-Jay kwa sasa ameamua kuchukua uamuzi wa kuokoka na kumfuata Bwana yesu!
Q-Jay amekuwa akitolea nje concert kibao ambazo anaalikwa kwa ajili ya kufanya show, kutokana na imani yake mpya aliyonayo sasa amefunguka kuwa “mziki niliokua nafanya ulikua ni wa dunia na ningewashauri wasanii wenzangu wote wanaoimba nyimbo za dunia kuufata wokovu na kuachana nazo,kwa sasa nimepumzika kufanya shughuli za mziki lakini kuanzia mwezi wa sita nitaanza kurekodi mziki yangu mipya ya kumtukuza mungu yaani gospel na natarajia kutoa album”....alimalizia Q Jay kwa sauti pole ya kilokole,akifuata nyayo za Stara Thomas,K Basil na Renee Lamira!

No comments:

Post a Comment