Wednesday, April 20, 2011

FID Q ATOA SOMO KUHUSU MALARIA KWA WASANII WA MWANZA


Ma-mc's wa hiphop wa jijini Mwanza wamekutana katika hoteli ya Coconut kupigwa darasa kwaajili ya kutumika wakiwa kama sehemu ya kuendeleza mbiu ya kutokomeza maralia inayojulikana zaidi kwa Zinduka.


Fid Q akiwa kama mmoja wa mabalozi wa maralia alishiriki kwa kiwango kikubwa kuelimisha wana hip hop wa home kutumia sanaa kama sehemu ya darasa kwa umma.
Ezden (pale kati) naye alihudhuria kwaajili ya kuchukuwa mada zitakazo jadiliwa kuzifanya sehemu ya kipindi Kiss Fm (Kiss mix collabo show).
Kama haujui Dark Master (wa2 kulia)naye Mwanza ndiyo home.
Waandishi wa habari.
Sambamba na kupata darasa washiriki nao walipata fursa kujadiliana wao kwa wao, katika kijiwe hiki Mnahela ndiye alikuwa host.
Anti Sadaka alitoa elimu: ndani yake Iligundulika kuwa Idadi kubwa ya watu wanaishi na marelia hivyo washiriki wakashauri kuwa usambazaji neti ungeenda sambamba na upimaji.
Moyo wa Kujitolea, Uadilifu, Upendo, Uzalendo na Kujituma ni moja kati ya mambo waliyotiliwa msisitizo. 
Weka ongezAAA!! washiriki pia walipata fursa ya kupata chakula cha pamoja.
'Pilipili kwa wingi' aling'aka Dj Cutter (mwenye rasta) anayefuata ni Kabago nakati ya Passion.
Mwisho wa siku wanahip hop walijichanganya stone club kunoa sauti zao kwaajili ya shughuli ya kesho (jumapili) ambapo sambambamba kushiriki zoezi la uelimishaji matumizi ya chandarua na maleria, nyumba kwa nyumba pia wasanii hao watapiga show ya wazi ya pamoja eneo la Kisesa nje kidogo ya jiji la Mwanza.

No comments:

Post a Comment