Friday, April 15, 2011

MISS ARUSHA CITY CENTER HAPATOSHI


         Mshindi wa mwaka jana Zahra Selemani ambaye alinyakua taji la Miss Arusha City Center 2010. 
warembo walioshiriki Miss Arusha City Center 20100 wakicheza kwa pamoja.

Mashindano ya ulimbwende ngazi ya kitongoji kanda ya kaskazini, Miss Arusha City Center 2011 yanatarajiwa kufanyika mei 13 mwaka huu katika Club ya Tripple A, jijini Arusha.

Akizungumza na gazeti hili, mraribu wa shindano hilo Bi. Sophia Urio alisema kuwa  kwa sasa wamejiandaa vyema tayari kwa ajili ya kufanya mashindano hayo.
Shindano hilo linalotarajia kufanyika katika jijini Arusha tayari mpaka sasa wameshakamilisha mchakato wa kuwasaka warembo na watahakikisha Miss Tanzania wa mwaka huu wanatokea mkoani Arusha.
"Tunamshukuru Mungu kwa maandalizi ambayo tumeshayafanya mpaka sasa, tunachosubiri  kwa sasa ni uzinduzi wa mashindano hayo ili tuweze kuendelea na kila kitu," alisema Bi. Sophia Urio.

Mashindano hayo ambayo yanatarajia kuwakutanisha warembo 10 hakika yatakuwa ya kupendeza sana maana mwaka huu kuna mabadiriko makubwa na mafanikio mengi. 

No comments:

Post a Comment