Tuesday, November 16, 2010

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU DODOMA WASOTA NA FOLENI YA KUCHUKUA FEDHA BENKI YA CRDB-DOM

Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali vya mjini Dodoma, wakiwa katika foleni kubwa katika Benki ya CRDB mjini humo leo mchana kusubiri huduma. Baadhi ya wanafunzi hao wamelalamikia utaratibu kutokana na kuwekwa mahala hapo kwa muda mrefu bila kuwa na uhakika wa kuhudumiwa ambapo baadhi yao wameshindwa kuvumilia na kuamua kuondoka kwa ajili ya kujipanga kuwahi tena kesho. "Sijui ni kwanini hawaweki hata Matawi yao hawa jamaa kwani wengine tusingekuwa na haja ya kuja mahala hapa na kukaa muda wote huu" alisikika mmoja wa wanafunzi hao akilalama.
Chanzo ni www.fufianimafoto.blogspot.com

No comments:

Post a Comment