Mtaa mzima ukawa hauna utulivu mpaka Wafanyabiashara pia hapakukalika hivyo walilazimika kusitisha huduma kwa muda.Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika kitongoji cha Tandika mara baada ya kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu.Hali hiyo ambayo ililete mtafaruku mkubwa sana katika eneo hilo mpaka kupelekea jeshi la Polisi kufika katika eneo hilo na kuanza kutuliza ghasia zilizokuwa zikiendelea katika eneo hilo,ambapo maduka yalifungwa na wamiliki wake kulazimika kuondoka kabisa katika eneo hilo. Hadi mpiga picha wetu anaondoka katika eneo hilo,ni kwamba mambo yalienda poa na vurugu ziliweza kudhibitiwa kabisa.
No comments:
Post a Comment