Wednesday, November 24, 2010

KAA TAYARI KWA UJIO MPYA WA MTU MZIMA QJ.

QJ
Hapa ni siku yake ya harusi

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu mnsanii Qj al;iyetamba kipindi cha nyuma na ngoma kama vile sifai na nyingine nyingi tu akiwa kwenye kundi la wakali kwanza sasa anakuja na ngoma yake mpya aliyoipa jina la NISAMEHE aliyomshirikisha Pipi.
Qj aliyasema hayo pale alipofanya mahojiano na mtoto wa kitaa na kuweka bayana kuwa ameamua kuachia ngoma hiyo kutokamna na kuwa kimya kwa muda mrefu kwasababu ya kufanya show nyngi mikoani.

NISAMEHE ni ngoma iliyoifanyika chini ya projuza TC kutoka katuika studio za 69.

Mtu mzima Qj pia hakusita kuweka wazi kuwa hiyo ndio ngoma yake ya kwanza kutoa tangu alipomaliza mkataba wake na MJ rec. “kaka nimeamua kuachia hii ngoma ambayo ndio itakuwa yakwanzqa tangu nimalize mkataba na MJ rec. sa watu wategemee vitu vizuri tu zaidi ya vile vya mwanzo kwani nimejipanga vya kutosha mzazi!”
Kuhusu kujaza mkataba na lebo nyingine mtu mzima QJ alisema hivi “kwa sasahivi naweza kusema sihitaji kuwa kwenye lebo yeyote ila ikitokea lebo itakayokuwa na mslahi zaidi ya ninanyotaka mimi basi nitakuwa sina budi kingia nao mkataba”
“Cha msingi ni maslahi tu kaka ndio tunayohitaji!” aliongeza QJ.
Akiiongelea NISAMEHE mtu mzima QJ alisema kuwa humo ndani anamzungumzia mshikaji aliyekua akimpotezea demu wake kwakua aliona kama dizaini demu amezimika kwake kwani alikuwa akimpa kila kitu lakini baadae demu alivyoamua kukata tamaa ikabidi mshkaji arudi kuomba msamaha.


KAA TAYARI KWA UJIO MPYA WA MTU MZIMA QJ.

No comments:

Post a Comment