Wednesday, November 10, 2010

PATA KITU KIPYA KUTOKA KWA SUMA SKILLS.


Unaweza kuwa unamjua lakini pengine hufahamu mabalaa mengi ya huyu bwana… ana mambo matatu makubwa ambayo pengine wengi wetu twalijua moja tu. Kwanza ni Rapper mkali, pili anauwezo wa ku shoot, ku direct na ku edit  music videos, tatu ni brazamen haswaa anapoamua ku upgrade image yake.
Huyu simwingine bali ni SUMASKILLZ, akiwa msanii wa kwanza kuanguka sign na label mpya ya WA3 Records, chipukizi huyu mkali anaejulikana sana na ngoma yake ya HISIA ZA MTAA (ft STEVE RnB) alipata muda wa kuingia studio za Mlab , DUKETACHEZ akamkabidhi kwa  MR. Magician aka WILLIE HD (producer aliyeufanya kazi nzuri sana katika wimbo wa FREE SOUL na NYIMBO zote za grace matata) pamoja na mtu mzima Innocent Mujwahuki aka KANYE (anakumbukwa sana kwa mabalaa yake ya kuhusika partially kwenye productions za   nyimbo kama Bado robo saa,wrong SMS, Atatamani na hata nyimbo mpya ya DITO “wapo” hasa kwenye kunyonga milio ya keyboards katika nyimbo hizo).
Baada ya Beat kukaa sawa, mtu mzima SUMA akatupia lines zake pale na jitihada za kumtafua mtu wa kukaa kwenye chorus zikaanza. Inaonekana chemistry ya STEVE RnB haipo tu kwa BABYBOY bali pia hata SUMA nae yupo katika usawa huo..maana mtu wa kwanza kumfikiria alikuwa mkali huyu wa RnB…baada ya kuita na kutupia zile vocals pale kati hakukuwa hata na mtu mmoja aliebisha studioni. Ngoma ikamaliziwa mixing na mtu mzima DUKETACHEZ  mchezo ukaisha.
Hivyo basi kwa mara ya kwanza, Wa3 records ina release single yake ya kwanza kabisa ya label kupitia kwa brazamen SUMASKILLZ aka THE DIRECTOR aka Kichefuchefu. Na hizi hapa ndio ndio details za mzigo mzima:
Artist: SUMASKILLZ feat Steve r’n’b
Song title: Ungejua
Composed By: SUMASKILLZ, Steve r’n’b
Produced by: Willie HD
Mixed By: Willie HD & DUKETACHEZ
Studios: Music Lab
Label: Wa3 records
 

No comments:

Post a Comment