Thursday, October 27, 2011

ZITO KABWE KUPELEKWA INDIA KWA MATIBABU ZAIDI


Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya kichwa.

Awali Zitto alilazwa katika hospitali ya Aga Khan kabla ya jana kuhamishiwa Muhimbili baada ya hali yake kubadilika na kutetemeka mwili mzima na o alipokelewa hospitalini hapo alikimbizwa katika Idara ya magonjwa ya dharura (EMD) na kuanza kupatiwa matibabu.
Habari zilizopatikana zinasema Mbunge huyo machachari na mwanachama wa Simba anatarajiwa kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

No comments:

Post a Comment