b..

B1

Wynem

animation

Monday, October 10, 2011

SBL YAZINDUA UPYA KINYWAJI CHA PILSNER LAGER.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe wa pili kutoka kulia akigonganisha chupa kuashiria uzinduzi wa kinywaji Pilsner Lager na Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Serengeti Breweries Bi. Teddy Mapunda (kulia) na Mkurugenzi wa Masoko Bw. Ephraim Mafuru wa pili kutoka kushoto pamoja na na meneja wa kinywaji cha Pilsner Lager Maurice Njowoka kushoto.

Na Mwandishi Wetu.

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kinywaji cha Pilsner Lager na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali zinazogusa mambo mbalimbali ya maendeleo katika kupunguza ama kuondoa kabisa umasikini uliokithiri miongoni mwa jamii ya kitanzania. Kinywaji cha Pilsner Lager pamoja na vingine vinavyozalishwa na kampuni hiyo vitaongoza mapambano ya kupunguza umasikini wa watanzania kwa kurudisha faida wanayopata katika mambo tofauti ya kimaendeleo.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Ephrahim Mafura aliyasema hayo wakati wa uzinduzi maalumu wa kinywaji cha Pilsner Lager katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mafuru alisema kuzinduliwa kwa kinywaji hicho kinachotumia slogan ya ‘kinywaji imara kama simba’ ni matumaini mapya kwa watanzania kwani wamedhamiria kuyafanya maisha ya watanzania kuwa imara kama Simba.
“Kampuni ya Serengeti ni miongoni mwa wadau wakubwa wa maendeleo nchini ambao tumedhamiria kuendelea kuongeza nguvu ya uzalishaji itakayotufanya tupate faida zaidi na kusaidia zaidi watanzania,”  Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof Jumanne Maghembe aliishukuru kampuni hiyo kwa mchango wake katika maendeleo ya nchi na kuwataka wadau wengine kuunga mkono jitihada hizo.
Alisema serikali inatambua na kuthamini mchango wa maendeleo wa kampuni ya Serengeti kwa watanzania na kwamba wakati wote serikali inaunga mkono wadau wa aina hiyo na wizara ipo wazi na huru kupokea maoni ya kuboresha huduma za kimaendeleo. “Mmekuwa wadau wakubwa wa maendeleo nchini, mchango wenu unatambulika na kuthaminiwa na serikali kwani changamoto tulizonazo zinahitaji nguvu ya pamoja, hongereni kwa kujitolea na tunatoa wito kwa wengine kufuata nyayo zenu,” alisema Waziri Maghembe.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda alitaja baadhi ya michango ya maendeleo ya kampuni hiyo kwa watanzania kuwa ni pamoja na kurahisha soko la malighafi ya wakulima wa ndani ambao sasa wanauza shayiri na mtama kwa kampuni hiyo. Pamoja na hayo alisema SBL imekuwa ikifadhili masomo ya elimu ya juu lakini pia imekuwa na mchango mkubwa katika kuzalisha nafasi za ajira kwa watanzania waliopo maeneo ya Dar es Salaam, Moshi na Mwanza vilipo viwanda vyao.

No comments:

Post a Comment