Wednesday, October 12, 2011

Priva P atoka na Wema videoni

Na Andrew Chale
MWANAMUZIKI nyota wa miondoko ya  takeu na  Afri pop, nchini Tanzania, Privatus  Peter  ‘Priva P’  amekamilisha video yake mpya  iitwayo ‘Wema’ aliyemuimbia mrembo huyo aliyemtesa katika mahusiano  yao yaliyodumu kwa muda mchache na kisha kumkimbia.
Akiteta  na mtandao huu, mapema hivi leo jijini Dar es Salaam, Priva P, alisema kua, wimbo huo  ambao tayari umeshaanza kutamba katika vituo vyote vya  redio nchini na nje ya nchi, tayari ameweza kutoa video hiyo ambayo itakua ni moto wa kuotea mbali kutokana na ubora wa hali ya juu.
 “Nashukuru wadau kwakuupokea wimbo wa Wema, redioni na sasa wataweza kumuona Wema rasmi katika  videoni ..kiukweli alinidatisha sana hii ni historia ya kweli nilimpenda sana Wema lakini sasa ameenda kwa mwingine” alisema Priva P.
Priva P anasema wimbo huo wa Wema ambao ni historia ya kweli kutokana na kumpenda msichana aliyekua na mahusiano naye aliyefahamika kwa jina la Wema, ambaye kabila lake ni Mhaya lakini alimtenda na kumuacha pekee yake.
Wimbo huo wa Wema uliotengenezwa video yake chini ya John Kallage, kupitia studio ya Kallage’s Pictures  utakua ni wapekee hasa kutokana na kupigwa picha hizo kali hasa ‘location’  na  washiriki ndani ya video hiyo.
Priva P awali aliwahi kutamba na wasanii mbalimbali akiwemo Q.Chila aliyeimba wimbo wa 'Tuvumiliane'  pia alikua katika albam hiyo yenye wimbo kama 'Tuvumiliane,Kalolina,Mapenzi ya kweli,Nondamaiza na nyingine, na albam ya pili ilijulikana 'Juhudi' na hii ya 'WEMA' ni albam yake ya tatu na ameweza kuwashirikisha wasanii,Chege, Q.chief na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment