Tuesday, January 25, 2011

TEKLA AACHIA NGOMA YA VALENTINE


Katika kukaribisha sikukuu ya wapendanao yaani valentain msanii wa kike kutoka M Lab TEKLA a.k.a TEK ameachia ngoma yake kali kabisa alioipa jina la NAFURAHI ikiwa imetangenezwa na pale studio za M Lab chini ya watayarishaji makini Nendeze & Kanye huku wakiongozwa kabisa na mtu mzima Duketachez wakati aditional vokal akiwa amesimama kijana Ben pol
Tekla ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa Tumaini univasity mwaka wa pili akichukulia kozi ya A mass communication a.k.a uandishi wa habari pia Tekla alipata kushirikiana na wasanii wengi kwa kuwaimbia koras a.k.a viitikio, nyimbo alizoshirikishwa Tekla ni kama ESHI LA MTU MMOJA by Fid Q, NYETI, USISHABIKIE VITU USIVYOVIJUA & RUSHWA by WAGOSI WA KAYA, BINTI KISURA by INSPECTOR Haroun na hizo ni chache tu!
na hii ngoma ya NAFURAHI ni ya pili kwa TEKLA tangu awe chini ya M LAB studio.
pia TEKLA anaomba sapot kwa mashabiki kwani wiki ijayo ataachia ngoma nyingine kali hivyo.

Gonga hapo pembeni kusikiliza ngoma mpya ya Tekla.

No comments:

Post a Comment