Wednesday, January 5, 2011

CHADEMA WACHEZEA KICHAPO BAADA YA KUKAIDI AGIZO LA POLISI


Mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa, Josephine akiwa ametapakaa damu baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kipigo na polisi wakati wakivunja maandamano ya viongozi na wanachama wa chama hicho yaliyofanyika mjini Arusha jana.Katika maandamano hayo watu kadhaa walijeruhiwa baada ya kupigwa na pilisi wa kutuliza ghasia.
Viongozi wa juu wa CHADEMA, wakiongowa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe (Watano kulia) na katibu mku, Dk.Wilbroad Slaa(Wasita kulia) wakiongoza maandamano yaliopigwa marufuku na polisi jana mjini Arusha.Hatimaye polisi iliwatolea uvivu na kuwapiga kwa mabomu ya machozi. Habari zaidi zaeleza kuwa Mbowe anashikiliwa na polisi.
Askari Polisi wakijaribu kulizuia gari moja lilikuwepo katika maandamano hayo.
Wanausalama wakimtuliza mmoja wa waandamanaji aliekuwepo katika maandamano hayo.
Wakazi wa maeneo ya jirani na zilipotokea vurugu hizo wakinawa maji usoni ili kupunguza makali ya sumu za mabomu ya machozi yaliyokuwa yakilipuliwa katika kutuliza ghasia hizo.
Mitaa ya Jijini Arusha ililindima milio ya Mabomu ya Machozi huku mitaa ikiwa imepoa kabisa.
Askari Polisi wakiwa wameenea kila kona kuhakikisha hali inakuwa shwari na hakuna mtu anaefanya maandamano hayo

No comments:

Post a Comment