Thursday, January 27, 2011

20% ALAMBA ZAWADI KUTOKA KWA MAN WATER.


John VN Shariza aka Man Water ambaye ndiye mmiliki wa Studio ya Combinations Sounds ambaye pia ndio Producer wa msanii wa 20 Percent.
Kufuatia kazi nzuri aifanyayo msanii wake Man Water mapema jana mchana aliamua kumsaprise msanii huyo kwa kumpeleka kwenye duka moja la vyombo vya mziki lililopo maeneo ya Kariakoo na kumnunulia vifaa kadhaa likiwemo gitaa.

"Nimemkabidhi zawadi hii ikiwa ni hatua ya kwanza na haikuwahi kutokea kwa Producer wa hapa bongo, kuonyesha kukubali kazi ya wasanii wao mpaka kutoa zawadi. Mimi nimeweka historia kwakua wa kwanza kufanya hivi na pia kuzidi kumpa support ya kusongambele katika muziki wake wa ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment