Monday, January 31, 2011

GETHOKING AACHIA WANAPAGAWA

Msanii wa hip hop anaeweza kubadilika kutokana na mazingira hapa namzungumnzia mtu mzima GETHOKING sasa ameachia ngoma yake mpya ailiyoipa jiana la WANAPAGAWA ambayo ipo katika mahadhi ya ragamaphy huku akiwa amewashirikisha wasanii wawili wakali kabisa katika miondoko ya hip hop.
Akizungumza na mtoto wa kitaa GETHOKING alisema kwa sasa ameamua kuachia ngoma hiyo kwa kuwa watu wengi wamezoea kusema kuwa wana hip hop hawawezi kubadilika ndio maana ameiachia ili kuwaziba midomo "kaka mimi humu ndani nimedondosha maraga ya ukweli kabisa, na hii nimeifanya makusudi kabisa kwa sababu wabongo wengi wanasema kuwa wanahip hop hatuwezi kubadilika"
"mimi ningeweza kuchana lakini nimeamua kubadilika na nafasi ya kuchana nikawapa wanangu TEMBA na JOSE MTAMBO." aliongeza GETHOKING
GETHOKING pia aliwahi kukimbiza na songi zake kadhaa kama vile Kufa kiume, Msaliti aliewashirikisha Geez mabov na Rado, na My Birthday ambayo ipo kwenye video.

TUSHIRIKIANE KUIPELEKA MBELE HIP HOP NA SANAA YETU KWA UJUMLA.

No comments:

Post a Comment