Monday, January 24, 2011

KILI MUSIC AWARDS YAZINDULIWA RASMI.Kutoka kushoto ni Mratibu wa Tunzo za Kilimanjaro kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Angelo Luhala, katikati ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe na Msaidizi wa KTMA Edith Bebwa wakiwa katika mkutano uliofanyika na waandishi wa habari hawapo pichani.
*********************************************
Na mwandishi wetu
Kampuni ya Bia Tanzania kwa kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro (Kilimanjaro Premium Lager) imezindua rasmi tunzi zake ambazo hutolewa kila mwaka wamesema mwaka huu watawatumia wasanii wa nyumbani katika kutoa burudani siku ya kilele cha hafla hiyo tofauti na ilivyokuwa katika miaka iliyopita ambako washereheshaji walikuwa ni wasanii kutoka nje.
Katika kunongesha zaidi onyesho hilo kubwa zaidi la utoaji tunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati , wasanii waliofanya vizuri mwaka jana tayari wametoa wimbo wao ambao waliutambulisha kwa wadau mwishoni mwa juma na utaanza kusikika katika vyombo mbalimbali ikiwa nikatika kuzitambulisha tunzo hizo kwa wadau kwamba kuna kitu kinakuja.
Tunzo hizo ambazo zinaratibiwa na Baraza la Sanaa Tanzania huku mdhamini wake mkuu tangu zianzishe ni TBL leo asubuhi wamezindua rasmi mchakato wa kuwatafuta na kutoa tunzo kwa wasanii waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka jana.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya TBL ,Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema tunzo hizo zitatolewa kwa wasanii wa Tanzania ambao wamefanya vizuri kwa kupitia kazi zao za muziki walizofanya katika kipindi cha mwaka 2010.
Alisema tunzo hizo zimepangwa kutolewa katika hafla maalum itakayofanyika Machi 26 kawenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini.
Aidha Kavishe aliongeza kwa kusema wataendelea kufanya kazi na makampuni matatu katika mchakato wa utoaji tunzo na uwezeshaji wa tunzo za muziki huku akiyataja majina ya kampuni hizo kuwa ni Digital Arts ambao ni wasimamizi wa mawasiliano ya wasanii pamojana na umma.
Kampuni zingine ni One Plus Communications ambao nao ni wasimamizi ya wasanii pamoja na umma,Entertainment Masters watakaosimamia burudani na mahitaji yake kwa ujumla.
Kampuni nyingine ni Deloite Management Consulting ambao ni wasimamizi na wahakiki wa mchakato wa upatikanaji wa wateule pamoja na washindi wa tunzo nchini.
Ratiba ya mchakato huo inaonyesha Januari 19 walifanya uzinduzi kwa wadau katika hoteli ya nyota tano Double Tree Masaki, jana wamezindua kwa nahabari.
Februari 12 hadi 13 wataandaa jopo la wana Academy 100 katika hoteli ya Kunduchi Beach, Februari 16 watatangaza majina ya wasanii waliopitishwa kuwania tunzo.
Februari 21 wasanii waliochaguliwa watahudhuria semina ya siku moja na ifikapo Machi mosi ndipo kura zitaanzakupigwa kadhalika Machi 24 majaji watakutana na kuhakiki kura.
Kavishe aliongeza kwa kusema kuwa kura za wapenzi wa muziki nazo zitajumuishwa katika kuchagua washindi , mwaka huu kura za wapenzi na mashabiki wa wasanii zitahesabiwa kwa asilimia 50 na majaji asilimia 50.Njia za kupiga kura ni kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno katika simu(SMS), Barua Pepe, Magazeti na Vipeperushi

No comments:

Post a Comment