Tuesday, July 24, 2012

TWANGA, MSONDO KUPAMBA TAMASHA LA SIKU YA WACHAGA‘CHAGA DAY 2012’

Baadhi ya wasanii wa Msondo Ngoma
Wasanii wa Twanga Pepeta

Na Mwandishi Wetu
BENDI  zenye ushindani mkubwa nchi za Twanga Pepeta na Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo kali na ya aina yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012), siku ya jumamosi Julai 28, katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul Siboka walioandaa tamasha hilo, alisema  siku hiyo itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza
Na kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.
“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya utamaduni  wa kabila hilo la Chaga, na makabila mengine  na burudani kutoka kwa bendi hizo za Twanga na Msondo,  pamoja na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema Siboka.
Pia alisema kua, kutakua na wazee wa  mila ambo watazungumzia asili la kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha, Siboka alisema  baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo nbalo litapambwa na sherehe mbalimbali. 

No comments:

Post a Comment