b..

B1

Wynem

animation

Friday, July 27, 2012

SHIWATA YAPEWA KIBALI CHA MAPAMBANO YA NGUMI MWAKA MZIMA NA TPBC


SHIWATA yapata kibali kuchezesha ngumi nchini
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) imekubaliwa kupata kibali cha kuandaa mashindano ya ndondi za kulipwa kupitia Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia  Julai 24 mwaka huu. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Viwango vya Mabondia wa Ngumi za Kulipwa  TPBC,  Boniface Wambura alisema kibali hicho kinaruhusu SHIWATA kuandaa mapambano na la kuanzia ni kati ya bondia Alfonce Joseph (Mchumiatumbo) na David Michael Mlope (Zola D – King) litakalofanyika katika Tamasha la Watani wa jadi katika Sikukuu ya Idd El Fitri kwenye Uwanja wa Chuo cha Bandari Temeke.
Pambano hilo ambalo limeandaliwa na SHIWATA ili kukusanya fedha za Ujenzi wa nyumba za kisasa za gharama nafuu kwa ajili ya Wasanii, Waandishi wa Habari na Wanamichezo katika Kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.
Kamisheni ya Ngumi za kulipwa nchini Tanzania (TPBC) ambalo inasimamia pambano hilo la Mabondia  hawa watakaocheza katika uzani wa juu (Heavy Weight) raundi nane (8) pia kutakuwa na pambano moja la utangulizi.
Mwenyekiti wa SHIWATA Cassim Taalib alisema pamoja na pambano hilo, kutakuwa na mechi ya mpira wa miguu kati ya Simba na Yanga (Veteran) katika Uwanja huo huo wa Chuo cha Bandari Temeke na mshindi wa mchezo huo atazawadiwa ng’ombe dume.
Taalib alisema kwamba kikundi cha Mchiriku cha Jagwa kitatumbuiza, Roman Mg’ande wa Msondo atapigana mieleka na Lumole Matovolwa (Big na upande wa wanawake Sophia Lubuva wa Simba atapambana na Mwajuma Jimama wa Yanga huku washangiliaji wa Mpira Pesa (Simba) watapambana  katika mpira wa miguu na Watani wao wa jadi Yanga Bomba.
Tamasha litapambwa na mechi ya Mpira wa Kikapu ya Ngongoti pamoja na mashindano ya Pikipiki ambayo yanatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa watoto na wakubwa ambao siku hiyo watakuwa wakisherekea Sikukuu ya Idd el fitri baada ya kumalizika kwa mwezi wa Ramadhani, Wasanii wa Bongo Flava nao watakuwepo.

No comments:

Post a Comment