Saturday, July 21, 2012

BODI YA MISS UTAALII TAIFA YAFUTA MISS UTAALII KANDA YA ZIW

BODI YA TAIFA YAFUTA MISS UTALII KANDA YA ZIWA 2012

Bodi ya Taifa ya Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO),imefuta na kutokulitambua shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012 lililo fanyika New Mwanza Hotel ,wakati taifa likiwa katika maombolezo ya msiba mkubwa wa kitaifa wa watu waliopoteza maisha katika ajali ya meli iliyo tokea Zanzibar.
Bodi imechukua hatua ya kulifuta na kutolitambua shindano hilo, ambalo limefanyika bila ya kuzingatia misingi ya kibinadamu na hata uzalendo kwa Taifa. Waandaaji wa shindano hilo Fania Hassan wa Fania Beauty Salon,pamoja na kutambua kuwa taifa lipo katika maombolezo ya siku tatu kwa tangazo na tamko la serikali, bado hakuzingatia maelekezo ya waandaaji wa Taifa ambao walisitisha mashindano ya Miss Utalii Tanzania katika ngazi zote,likiwemo lile la Miss Utalii Kinondoni 2012 ambalo lilikuwa lifanyike tarehe 20-7-2012 katika ukumbi wa Traveltine Dar es Salaam ambalo sasa litafanyika 31-7-2012 katika ukumbi wa Club Maisha Oyterbay na lile la Miss Utalii Ilala 2012 ambalo lilikuwa lifanyike 21 -7-2012 katika ukumbi wa Eriado View pont Pugu Dar es Salaam ambalo sasa lifanyika siku ya Iddy Pili katika ukumbi wa Eriado point View Pugu.
Bodi ya mashindano katiaka kikao chake cha dharula kilichofanyika leo asubuhi baada ya kupata taarifa kutoka kwa vyanzo vyetu vya uhakika,juu ya kufanyika kimyakimya kwa shindano hilo imeamua kuchukua hatua hiyo kali ya kulifuta na kutolitambua shindano hilo, ili iwe fundisho kwa waandaaji wengine wasiozingatia maagizo kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mashindano haya. 
Bodi imesikitishwa sana na tukio hilo kisilo la kizalendo, na inawaomba radhi watanzania wote,ndugu na jamaa wote waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo,serikali, mamlaka zote za mkoa wa Mwanza, mamlaka za sanaa,wadhamini na wadau mbalimbali wa mashindano ya urembo utalii na utamaduni nchini na nje ya nchi.
Washiriki wote watalazimika kusubiri tarehe mpya ya kufanyika kwa shindano hilo,baada ya mfungo wa ramadhani,ambapo pia watagharamiwa gharama zote za ushiriki wao upya,kama kanuni na taratibu za mashindano zinavyo bainisha kuwa washiriki wote wa mashindano ya Miss Utalii tanzania wanagharamiwa gharama zote za mavazi,usafiri,vinywaji,chakula na saluni.
Kamati ya nidhamu ya mashindano haya itakutana mwisho wa mwezi ili kujadili hatua zaidi za kuchukua dhidi ya waandaaji hao wa Miss Utalii kanda ya Ziwa 2012.
Haiwezekani hata kidogo wakati taifa lina omboleza halafu mtu anatumia mashindano haya ambayo ni alama ya urithi wa Taifa na kielelezo cha utamaduni wa mtanzania kukiuka utamaduni,mila na desturi za Tanzania,tena wakati hata serikali 
imetangaza maombolezo na bendera zinapepea nusu mlingoti. 
Kwa mara nyingine tena tunaungana na watanzania wote kuwapa pole Ndugu zetu wa Zanzibar walio Potelewa na ndugu jamaa pamoja na Marafiki, Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape Nguvu katika kipindi hiki kigumu. Pia kwa wale majeruhi na ambao wapo kwa matibabu pia Tunawaombea wapate kupona Haraka ili warejee katika kazi zao za kujenga taifa. 
Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa – Utalii ni Maisha ,Utamaduni ni Uhai wa Taifa.
Asante,
Abubakari Omary Bakari
MKURUGENZI WA UTAWALA NA FEDHA - MISS TOURISM TANZANIA ORGANISATION

No comments:

Post a Comment