Tuesday, July 17, 2012

'SELEMAN TOLL' AMTAKA KASEBA ULINGONI.

Na Mwandishi Wetu
BONDIA Selemani Galile 'Selemani Toll'  amejitokeza hadharani na kumtaka bondia Japhert Kaseba baada ya kukimbiwa na Fransic Cheka katika mpambano wao uliokuwa ufanyike uwanja wa taifa jijini Dar es salaam katika tamasha la matumaini
Galile amesema yupo tayari kupambana na Kaseba mda wowote ule baada ya Cheka kumuona Kaseba kuwa rekodi yake ni mbaya ya kushinda mbili na kupigwa michezo miwili won 2 (KO 1) + lost 2 (KO 2) + drawn 0 = 4 na ya Galile won 11 (KO 9) + lost 7 (KO 5) + drawn 2 = 20
  'amesema kuwa Kaseba anataka kuleta rekodi yake Kick Boxing katika masumbwi wakati kitu hicho si cha kweli yeye ni bingwa wa kick boxing lakini mimi ni mtaalamu wa masumbwi hivyo kabla ya kumkabili Cheka inatakiwa tujichuje kuweza kumkabili bingwa wa ngumi IBF Afrika Fransic Cheka
Mimi nina uwezo wa kumgalagaza Kaseba na kuona mchezo wa masumbwi kwake ni hatari kwa kuwa mimi ni mtaalamu wa mchezo huo na mashabiki wa masumbwi wananijua kazi yangu katika ulingo wa masumbwi na redi yangu inafahamika vizuri Duniani kwa kuwa nimesha cheza Nje ya Nchi mara nyingi na nina uzowefu wa mapambano mengi hivyo naisi nikikutana nae nitamwonesha kiwango changu katika mchezo uhu wa masumbwi
Hata hivyo bondia huyo amewataka mapromota kujitokeza kuandaa mpambano wake na Kaseba kwa kuwa hana hamu na usongo wa kumfundisha mchezo wa ngumi unachezwaje
Bondia huyo katika mpambano wake wa mwisho alicheza na  Thomas Mashali  katika mpambano wa kugombania ubingwa wa TPBO na alioshindwa kwa point ambapo alionesha ustadi wa ali ya juu kwa ufundi wa mchezo uho na kuleta upinzani wa ukweli na kustajabisha mashabili baada ya kumlaza chini mara mbili bondia Thomas Mashali wakati wa mpambano huo
Bondia huyo anaefanya kazi katika klabu ya Delvis Corener iliyopo Temeke Chini ya  kocha wake wa ngumi ajulikanae kwa jina la  haji pela Bondia mkongwe wa siku nyingi

No comments:

Post a Comment