Je? Unajua kuwa hadithi za Filamu zozote hujengwa kwa
wahusika, wahusika ndiyo wabeba lengo zima la filamu? je wajua jinsi ya
kuwajenga wahusika wako ili waweze kubeba lengo la hadithi ya Filamu kiufasaha? je unajua kuwa ukikosea kumjenga
mhusika mkuu katika hadithi ya Filamu
yako ni vigumu hadithi ya Filamu bora? basi ukitaka kuyajua yote haya
karibu katika warsha ya uandishi wa miswada ya filamu pale IDARA YA SANAA CHUO
KIKUU CHA DAR ES SALAAM Kuanzia tarehe 13-15 Februari 2012 ,Kutakuwa na Warsha
ya Uandishi wa Miswaada ya Filamu/Screenplay Workshop(Level 1) , Idara ya Sanaa
na Sanaa za Maonesho, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kila siku kuanzia saa 3
asubuhi hadi saa 8 mchana , Cheti cha Ushiriki kitatolewa mwishoni mwa mafunzo.
Warsha itakuwa kwa
Kiswahili (na Kiingereza ikibidi) na mshiriki anaweza kuwa mtu yoyote
anayependa kuandika miswada ya filamu (amateur scriptwriter) au mwandishi
anayechipukia (upcoming scriptwriter)
Hima wadau wote wa Tasnia ya Filamu ,Sanaa, Sanaa za
Maonyesho na Uandishi wa ubunifu msikose nafasi hii muhimu ya warsha mafunzo
daraja la kwanza ilikujijengea misingi mizuri ya Uandishi wa Miswaada ya Filamu
Kwa maelezo zaidi kuhusiana
na warsha hii tafadhali wasiliana na:-IDARA YA SANAA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Ndg.John Mwakilama
Simu Namba 0714 13 22 49,
barua pepe :mwakilamajohn@yahoo.com
No comments:
Post a Comment