Friday, February 17, 2012

AKUTWA KAJINYONGA KUTOKANA NA KUTOSWA NA MKE WA MTU!

HAMISI TUMBUKA [25] Mkazi wa Kibamba, amekutwa amejinyonga kutokana na sababu za kimapenzi baada ya kukataliwa na mke wa mtu ambaye alikuwa akimpenda kupita kiasi.Marehehemu huyo alikutwa amekufa akining’inia juu ya mti na kuacha ujumbe mzito ambapo alibainisha sababu cha kifo chake na kumtaja mwanamke ambaye alikuwa akimsumbua akili na kumuandika jina lake lililofahamika kama Ashura 
Mbali na kuacha ujumbe pia alitoa maagizo kwenye ujumbe huo kuwa azikwe kiiislamu na aliomba msichana huyo aliyemtaja kwa jina la Ashura ashuhudie mazishi yake kwa kuwa alisababisha kifo hicho
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi , majira ya saa 2 asubuhi, huko Kibamba ambapo polisi walikuta mwili wake ukining’inia kwenye mti. 
Kamanda Kenyela amesema kuwa marehemu huyo alitumia kamba ya katani kujinyonge na kukutwa na ujumbe uliosema
“Naomba Waislamu wanizike hapa hapa na Ashura ashuhudie ninavyozikwa..., Ashura nakupenda uishi salama na mumeo.” Ulimaliza ujumbe huo
Polisi mkoani Kinondoni wameuhifadhi mwili huo katika Hospitali ya Tumbi Kibaha kwa uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment