Thursday, February 23, 2012

Super D

BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya muziki’, inawaomba radhi mashabiki wao wa DDC Kariakoo kwa kuwakosa kwa wiki moja kwani kwa sasa wanapiga shoo Ya Jumapili hii watakua katika ukumbi wa Max Bar ya Ilala Bungoni Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila ‘Super D‘, alisema kuwa hawakupanga kuondoka Kariakoo lakini kutokana na muingiliano wa ratiba hawana budi kufanya hivyo ingawa wanaamini wiki zijazo mambo yatakuwa mazuri.Alisema hata hivyo bado wanahitaji kuwa karibu na mashabiki wao kwani uwepo wao ndiyo kazi yao ya kuimba inakuwa inakamilika.“Wiki hii hatutapiga shoo hapa Kariakoo, na tutakuwa Max bar Ilala na hii imetokana na ratiba fulani ambayo tulipewa lakini naamini wiki ijayo kila kitu kitakuwa sawa, hivyo mashabiki wetu tunaomba radhi kwa usumbufu huo,” alisema Super D.

No comments:

Post a Comment