b..

B1

Wynem

animation

Sunday, November 7, 2010

SIKU NILIPOTEMBELEA AEGIES RECORD KWA AJILI YA KUFANYA JINGLES.

Hapa ndio nilikuwa naingia studio kama inavyoonekana kwa nyuma ndio mlango mkuu na umendikwa receiption.

Hapa nilikua na mtu mzima NICE P. audio producer wa kutegemewa kabisa wa pale Aegies Rec.
Hapa niko na Brother from another Mather ATHER KD. Video producer wa Aegies Production
Baada ya kumaliza kazi mtoto wa kitaa ckuwa na lakufanya zaidi ya kuwashukuru wadau wote wa pale studiuo kwa kunipa ushirikiano wa kutosha mpaka kuweza kufanikisha mambo.

Friday, November 5, 2010

VODACOM TANZANIA YATANGAZA ZAWADI ZA MWANZA CYCLE CHALLENGE.




Vodacom Tanzania imetangaza zawadi zitakazotolewa kwa washindi mbalimbali watakaoshiriki mashindano ya baiskeli ambayo yatafanyika Jijini Mwanza mwezi huu yanayotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 50.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Jijini leo, katika makao makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa alisema kwamba mashindano ya mwaka huu yameboreshwa zaidi na kuwaomba waendesha baiskeli kujitokeza kwa wingi.

“Mashindano haya yameboreshwa kwa upande wa zawadi, ubora na viwango,” alisema.

Aidha alifafanua kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa siku mbili yaani Novemba 12 na 13 mwezi huu na kwamba tarehe 12 itakuwa maalumu kwa mashindano ya walemavu ambao watashindana kilometa 15 kwa wanaume na 10 kwa wanawake. Na tarehe 13 Novemba yatafanyika mashindano ya kilomita 196 kwa wanaume, 80 kwa wanawake ambapo kwa upande wa walemavu ni Kilometa 15 kwa walemavu wanaume na Kilomita 10 kwa walemavu wanawake.

Akitangaza zawadi hizo kwa washiriki wa mbio za kilometa 150 Mtingwa alisema mshindi wa kwanza atajipatia shilingi 1,500,000, wa pili kiasi cha 1,000,000, wa tatu 700,000, ambapo mshindi wa nne hadi wa kumi kila mmoja atajipatia shilingi 500,000 kila mmoja. Aidha kwa upande washindi wa 11 hadi 20 kila mmoja atajinyakulia kitita cha 250,000 kila mmoja, na kuanzia mshindi wa 21 hadi wa 30 watapatia shilingi 90,000 kila mmoja.

Kwa upande wa mbio za mita 80 kwa wanawake mshindi wa kwanza pia atajipatia zawadi ya shilingi milioni 1,100,000, wa pili 800,000, mshindi wa tatu 600,000, wakati washindi wa nne hadi wa kumi kila mmoja atazawadia kiasi cha shilingi 350,000 kila mmoja. Vilevile washindi watakaoshika nafasi ya 11 hadi ya 20 katika mbio hizo watapewa jumla ya 130,000 kila mmoja, na kuanzia mshindi wa 21 hadi wa 30 watapatia shilingi 70,000 kila mmoja.

Mbali na hayo Mtingwa alibainisha kwamba kwa upande wa mbio za kilometa 10 ambazo zitawashirikisha watu wenye ulemavu alisema washindi wa kwanza wawili kila mmoja atajipatia jumla ya shilingi 400,000.

Kwa washindi wa pili wawili nao watajishindia kiasi cha shilingi 250,000 kila mmoja, washindi wa tatu wawili kila mmoja atapewa kiasi cha 150,000 kila mmoja wakati washindi wa nne wane hadi wa kumi watajipatia kitita cha 70,000 kila mmoja.

Aidha alifafanua kuwa mashindano ya mwaka huu ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge yameandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa takribani miaka mitano sasa na kudhaminiwa na Alphatel, Knight Support na SBC kupitia kinywaji chake cha Pepsi.

Alisema Alphatel watadhamini mashindano ya walemavu, Knight Support watatoa ulinzi, huduma ya kwanza na gari la wagonjwa wakati SBC watakuwa wasambazaji rasmi kwa kupitia kinywaji chake baridi cha aina ya Pepsi .

“Shindano hili la Vodacom Mwanza Cycle Challenge ni mahususi kwa kukuza mchezo huu hapa nchini kwa lengo la kupata wawakilishi bora katika mashindano mbalimbali ya kimataifa,” alifafanua.

Alisema kampuni yake imekuwa ikidhamini michezo mbalimbali kama vile Soka, Riadha, kuogelea, mashindano ya boti, mashindano ya Mbuzi, Vodacom Miss Tanzania,Tenisi na mingine mingi ili kuhakikisha kwamba taifa linafanya katika tasnia nzima ya michezo.

KUNDI LA MUZIKI LA AFRIKA LIJULIKANALO ONE8 LIKIENDELEA NA MCHAKATO WAKE.

Amani na Ali kiba wakiwa wamepumzika baada ya kurekodi nyimbo na kundi zima la ONE8 jijini Chicago nchin Marekani.
Ali Kiba akitengenezwa ili apendeze zaidi kabla ya kupigwa picha za kundi lao la wanamuziki wa Africa lijulikanalo kama ONE8 huko Chicago nchini Marekani.
Ali Kiba na Fally Ipupabaada ya kumaliza kupigwa picha za kundi lao la ONE8.

Thursday, November 4, 2010

JUKWAA LA SWAHILI FASHION WEEK LAANZA RASMI KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE

Kutoka kushoto Mpho Kuaho-Designer kutoka Botswana, Judy Muya- Representative kutoka Southern Sun na designers wengine.
Saphia akiwatambulisha designers.
Baadhi ya designers wa SFW 2010  wakiwa kenye picha ya pamoja.

Jukwaa la tatu la Swahili fashion Week linaanza leo katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaam na kudumu kwa muda wa siku tatu hadi tarehe 6 ya mwezi wa November 2010.

Katika jukwaa la mwaka huu jumla ya wabunifu 24 kutoka nchi za Afrika hasa zile zinazozungumza lugha ya Kiswahili wamejiandaa vya kutosha katika kuonesha kazi zenye viwango vya kimataifa.

“Tunashukuru kwani mipango yote inakwend kama tulivyopanga na tayari wabunifu wote wamefika kwa ajili ya shoo kabambe ambapo itakuwa na tofauti kubwa kulinganisha na zile zilizopita. Tayari wabunifu wote 24 kutoka Tanzania na nchi za Pan Afrika wapo tayari kwa shoo ya mwaka, inayoandaliwa nyumbani mwa Swahili Fashion Week.” Alisema Mustafa Hassanali muandaaji wa Swahili Fashion Week

“Kwa mara nyingine tena tupo na Swahili Fashion Week 2010, na kusaidia kukuza Sanaa ya ubunifu wa mavazi hapa nchini, pamoja na kuwakaribisha wageni wetu ambao ni wabunifu wa kimataifa. Southern Sun inajivunia kutokana na mchango wake inayotoa kwa Sanaa ya ubunifu wa mavazi Afrika na hii intupa fursa ya kuendelea kwa njia mbalimbali.” Alisema meneja mkuu wa southern sun Hotel Ndugu Adam fuller

Southern Sun hotel imekuwa nyumba ya Swahili Fashion Week toka mwaka 2009.
Swahili Fashion Week inafanyika kwa mwaka watatu sasa na itawashirikisha wabunifu 24 ambapo kwa mujibu wa ratiba, siku ya kwanza shoo itapambwa na Manju Msita (Tanzania),Sonu Sharma (Kenya),Shelina Ebrahim (Tanzania/Canada),United Against Malaria (Tanzania Various),Farha Sultan (Tanzania),Tanzania Mitindo House (Tanzania - Various), KemiKalikawe (Tanzania) na Asia Idarous (Tanzania)

Kwa upande wa tarehe tano, siku ya ijumaa mwanamitindo kutoka Tanzania Jamila Vera Swai tfungua pazia akifuatiwa na Marinella Rodriguez (Mozambique),Stella Atal (Uganda),Kooroo (Kenya),Zamda George (Tanzania),Mafi Designs (Ethiopia),Moo Cow (Kenya),Robi Morro (Tanzania),Made by Africa (Tanzania) na Asos Africa (UK)

Tarehe sita November siku ya mwisho ya jukwaa la Swahili Fashion Week, wabunifu wtakoonesha kazi zao ni pamoj na wabunifu wanane wanaochipukia waliofanikiwa kuingia fainali kupitia shindano la wabunifu wanaochipukia, Emerging Designers Competition (Tanzania - Various),Gabriel Mollel (Tanzania),Khadija Mwanamboka (Tanzania),KikoRomeo (Kenya), John Kaveke (Kenya), Chichia London (Tanzania/UK), Ailinda Sawe (Tanzania)

“ Pamoja na kuwakaribisha wageni wetu ambao ni wabinifu wa mavazi , pia Southern itatoa zawadi kwa gauni bora katika Swahili Fashion Week kwa huu , lengo ni kusaidia kukuza Sanaa ya ubunifu wa mavazi” Aliongeza Saphia Ngalapi, Swahili Fashion Week PR manager

Swahili fashion week 2010 imedhaminiwa na home of Swahili Fashion Week - Southern Sun, Origin Africa, USAID Compete, , Malaria Haikubaliki, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania), Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print Ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danish make up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery Ltd, 1&1 Internet Solutions, Sengi Tours, iFashion, 361 Degrees na EATV & East Africa Radio.

Kuhusu SOUTHERN SUN
Southern Sun ni hoteli inayojivuni kuwa Afrika kwa zaidi ya miaka 40 sasa, ikitoa huduma bora kwa wageni wa nje na ndani ya nchi. Imetunukiwa sifa ya kuwa kundi la hoteli inayosifika barani Afrika.

USALAMA WA TAIFA WAPINGA MADAI YA DK. SLAA.

Bw. Jacky Mugendi Zoka Naibu Mkurugenzi Idara ya Usalama wa Taifa akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar es salaam wakati alipotoa taarifa ya kupinga madai ya Dk Willbrod Slaa Mgombea urais Kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuwa idara hiyo imeshiriki katika kuchakachua Kura za mgombea huyo wa urais. Mkurugenzi huyo amesema wananchi wampuuze Dk Willbrod Slaa na kauli yake kwani madai yake hayana ukweli wowote na ameongeza kwamba idara yake haijajihusisha kabisa na masuala ya uchaguzi hivyo madai hayo ni ya kuipaka matope idara hiyo.

DIAMOND ATAMBULISHWA URBAN PULSE

Diamond akiwa Bond Street, London, Uingereza
Mkuu wa u utawala Bi Carol Chipeta na Diamond
Mh Balozi Kallaghe, Diamond na Kaimu Balozi Chabaka Uingereza

Frank, Balozi Kallaghe, Diamond, Kaimu Balozi Chabaka, Baraka na Nocha.


Salam,

Baada ya Kuwasili ndani ya UK jumanne jioni Urban Pulse walimpeleka Msanii Mahiri wa Kizazi Kipya Diamond aka mzee wa Mbagala katika ubalozi wa Tanzania hapa jijini London kumtambulisha na kutoa Salam kwa Mh Balozi, Naibu Balozi na pamoja na staff wake. Diamond ametua kwa ajili ya Kufanya Urban Tour dhidi ya malaria. Show ya kwanza itafanyika jumamosi hii hapo ndani ya mji wa MILTON KEYNES CLUB OPUS ikifuatiwa na THE CLUB CROYDON 12/11.



NYOTE MNAKARIBISHWA,
URBAN PULSE CREATIVE

MISS TANZANIA 2010 AREJEA KUTOKA CHINA.

Miss Tanzania Genevieve Emanuel mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwlimu J.K.Nyerere jana akitokea nchini China.
Warembo kadhaa wakiwapokea wenzao wakati walipowasili jana kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere wakitokea nchini China
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Itifaki Kamati ya Miss Tanzania Bw. Albert Makoye, pamoja na Mrembo wa Chuo Kikuu Kikuu Huria Christina Justine, na Miss Shinyanga 2010 Buduri Ibrahim kwa pamoja wakiwapokea Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel na mshindi wa pili Glory Mwanga kushoto kwa Genevieve, na Miss Temeke mshindi wa pili Anna Daudi ambao waliwasili jana kwenye uwanja wa ndege wa Mwlimu J.K.Nyerere wakitokea Sanya China katika mashindano ya urembo ya dunia.
Mrembo Anna Daudi na Glory Mwanga walikwenda Sanya China kumpa sapoti Miss Tanzania 2010. pamoja na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashimu Lundenga, Katibu Mkuu Bosco Majaliwa, na mama wa Miss Tanzania 2010 Mrs. Mary Emmanuel Mpangala.

Tuesday, November 2, 2010

SUGU AWASHUKURU WATU WOTE WALIOMUWEZESHA KUINGIA MJENGONI HASA WATU WAKE WA JIMBO LA MBEY MJINI.

Mr SUGU Joseph Mbilinyi Mbunge Mteule Mbeya mjini kuanzia mwaka 2011 mpaka 2015.

SWAHILI FASHION WEEK 2010MODEL CASTING TOOK PLACE ATSOUTHEN SUN HOTEL.

Final selection of Models who will participate in Swahili Fashion Week 2010.
Male models being selected at the model casting for Swahili Fashion Week 2010.


Swahili Fashion Week 2010 Model Casting took place at Southern Sun Hotel

100 expectant models auditioned...

60 female and 40 male models arrived at Southern Sun Hotel for the greatly anticipated model casting for Swahili Fashion Week 2010.

All hopeful models were welcome to audition for the chance of being a part of the Swahili Fashion Week extravaganza.

The final selection included 16 female models and 8 male models who will open this years show on Thursday 4th to 6th November 2010 at Karimjee Garden.

Swahili Fashion week is a platform for designers – both fashion and accessory – from Swahili speaking countries to showcase their creativity, market their art and network with their clientele.

This is all aimed at promoting fashion as an income generating, job creating industry while emphasizing a “Made in East Africa” concept.

Swahili Fashion Week 2010 has been sponsored by the home of Swahili Fashion Week - Southern Sun, Origin Africa, USAID Compete, MALARIA HAIKUBALIKI , BASATA (Baraza La Sanaa Taifa), Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print Ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danish make up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery Ltd, 1&1 Internet Solutions, Sengi Tours, Ifashion, 361 Degrees and EATV & East Africa Radio.

MAMBO YALIYOTOKEA KWENYE KIPINDI CHA MATOKEO KULE TANDIKA JIJINI DAR.

Hili ni gari la maji ya kuwasha likiwa tayari kwa lolote litakalotokea.
Raia wakiwa wamejichanganya na mawakala wa uchaguzi katika kituo cha polisi.
Palianza kuchafuka kihivi
Ikaja hivi
Polisi nao wakaanza kujisogeza.
Mapambano kati ya raia na polisi yalikuwa hivi.
Mwana habari akifuatilia habari kwa umakini.
Polisi wakafanikiwa kuwatia nguvuni baadhi ya raia kama wanavyoonekana katika picha
Mtaa mzima ukawa hauna utulivu mpaka Wafanyabiashara pia hapakukalika hivyo walilazimika kusitisha huduma kwa muda.Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika kitongoji cha Tandika mara baada ya kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu.Hali hiyo ambayo ililete mtafaruku mkubwa sana katika eneo hilo mpaka kupelekea jeshi la Polisi kufika katika eneo hilo na kuanza kutuliza ghasia zilizokuwa zikiendelea katika eneo hilo,ambapo maduka yalifungwa na wamiliki wake kulazimika kuondoka kabisa katika eneo hilo. Hadi mpiga picha wetu  anaondoka katika eneo hilo,ni kwamba mambo yalienda poa na vurugu ziliweza kudhibitiwa kabisa.

Monday, November 1, 2010

SHINDANO LA GIRAFE UNIQUE MODEL LAZINDULIWA RASMI LEO.

Mkurugenzi wa shindano la Urembo liitwalo Unique Modol, Bwa. Magessa akizungumza mchana huu katika moja ya kumbi za hoteli ya Giraffe jijini Dar,kuhusiana na uzinduzi wa shindano hilo linalotarajiwa kuanza hivi karibu.Miriam Gerald.
Hawa pia ni majaji kulia ni Mwakilishi wa Hoteli ya Girrafe Ocean View Gonza Muchunguzi na Mbunifu wa mavazi Ally Remtullah.
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano huo leo.


Kampuni ya Unique Entertainment imeandaa shindano la uanamitindo linalojulikana kama Unique Model litakalofanyika Desemba 24 mwaka huu katika hoteli ya Giraffe Ocean View. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Unique Entertainment Methusale Magese alisema kuwa shindano hilo litajumuisha washiriki ishirini.
Alisema kuwa washiriki hao watapatikana katika mchujo utakaofanyika Novemba 20 mwaka huu katika hoteli ya Giraffe Ocean View. Aliwataja majaji watakaohusika katika mchujo huo kuwa ni mbunifu maarufu wa mavazi nchini Ally Rhemtulla, mwanamitindo Victoria Martin, Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald na mcheza filamu maarufu Steven Kanumba.

Alivitaja vigezo vitakavyotumiaka katika shindano hilo kuwa ni urefu wa futi 5’ 8’-6’, hips 35-37, kiuno 26-29 na kifua 32-35.Vigezo vingine ni muonekano wa kiuanamitindo, kijiamini na umri 18-25, tabia njema na minato.Aliwataka wasichana wenye sifa hizo kujitokeza Giraffe Hoteli Novemba 20 kwa ajili ya mchujo kupata washiriki 20 watakaoingia kambini katika hoteli hiyo Desemba mwaka huu.

UGONJWA WA SARATANI YA MATITI KWA KINA MAMA WAONGGEZEAKA.


Mtaalam wa Magonjwa ya Saratani katika Hospitali ya African Medical Investments ya jijini Dar es Salaam,Dkt. Rajiv Rao akifafanua jambo mbele ya wanahabari waliofika leo katika mkutano uliofanyika kwenye hospital hiyo,iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam. Mtaalam wa Magonjwa ya Saratani katika Hospitali ya African Medical Investments ya jijini Dar es Salaam,Dkt. Rajiv Rao akifafanua jambo mbele ya wanahabari waliofika leo katika mkutano uliofanyika kwenye hospital hiyo,iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Dharula katika Hospitali ya African Medical Investments ya jijini Dar es Salaam,Dkt. Sabrina Kazia akifafanua jambo kuhusu ugonjwa wa Saratani ya Matiti leo katika mkutano na waandishi wa habari.
Baadhi ya wanahabari pamoja na madaktari wa Hospitali hiyo wakifuatilia kwa makini mkutano huo.


Kwa kipindi cha miaka mingi, dhana ilijengeka kwamba saratani ya matiti lilikuwa ni jambo ambalo liliwaathiri zaidi wanawake kutoka bara ulaya ambao walikuwa kwenye umri wa miaka ya kati kutoka kwenye familia tajiri katika nchi zilioendelea, na kwa muda Fulani, dhana hii ilikuwa sahihi.

Hata hivyo, sura ya saratani ya matiti inabadilika kwa kiwango cha waathirika kuongezeka kwa takriban mara saba katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

“Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kiwango cha saratani ya matiti ni asilimia 16 ya waathirika wote wa saratani duniani ambao ni wanawake, jambo ambalo linaifanya kuwa saratani iliyoenea zaidi ambayo si saratani ya ngozi, miongoni mwa wanawake wote duniani,” anaelezea Dk. Amit Thakker, Afisa Mtendaji Mkuu wa muda wa African Medical Investments plc (AMI).

“Hii ni saratani inayoongoza katika kuwaathiri wanawake kwenye nchi zinazoendelea na zilizoendelea, huku saratani ya shingo ya kiazi ikifuatilia kwa karibu, na kuchukua nafasi ya pili. Takriban matukio milioni 1.3 hutokea na kutambulika kila mwaka, duniani.

Barani Afrika, takriban waathirika wapya 20 kwa kila watu 100,000 yanasajiliwa na kiwango hiki kinaongezeka,” aliongeza Dk. Thakker.

Kwa mujibu wa WHO, takriban wanawake 87.9 kwa kila wanawake 100,000 nchini Uingereza walibainika kuwa na saratani ya matiti mwaka 2008, ikilinganishwa na kiwango kidogo cha wanawake 19.3 kwa kila wanawake 100,000 kwenye nchi za Afrika Mashariki. Hata hivyo, WHO inafanua kwamba idadi hii inatokana na kiwango kikubwa cha uelewa wa utambuzi wa awali nchini Uingereza, jambo ambalo si la kawaida kwenye nchi za Afrika Mashariki, ikiwemo Tanzania.

Dk. Nimfa Ranido, daktari mkazi wa magonjwa ya wanawake kwenye Hospitali ya AMI, jijini Dar es Salaam anaunga mkono hoja hiyo na kusema “Saratani ya matiti inatibika lakini mara nyingi zaidi tunapata wanawake wanaofika kutibiwa huku athari za ugonjwa zikiwa zimefikia hatua za mbele zaidi.

Barani Afrika, uelewa wa saratani ya matiti na utambuzi wa awali ni muhimu sana katika kupambana nayo; iwapo saratani ya matiti itabainika mapema, itakuwa rahisi zaidi kuitibu katika hatua hiyo. Wanawake wengi wa Kiafrika hawana ufahamu wa kujifanyia utambuzi wao wenyewe au jinsi ya kuwezesha matiti yao kukaguliwa, hivyo, elimu na kuongeza uelewa ni muhimu sana.”

Kwa kuwa mwezi Oktoba ni mwezi wa kuhamasisha uelewa juu ya saratani ya matiti, AMI wameamua kuendesha kampeni ya uelewa huo kupitia Hospitali na Zahanati ya Mwanamke Mwenye Afya Njema (Well Woman Clinic) jijini Dar es Salaam, Tanzania.

“Sio tu kwamba mtazamo wetu ni kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa wetu, lakini tunataka kuwawezesha na kuwaelimisha juu ya afya zao ili waweze kubakia na afya njema kila wakati,” aliongeza Dk. Ranido.

Dk. Ranido anaeleza kwamba wanawake walio katika umri wa kati ya miaka 20 na 30 wanapaswa kuwa na ukaguzi wa matiti wa kitaalam (clinical breast exam – CBE) kama sehemu ya kawaida ya ukaguzi wao wa afya wa mara kwa mara, ambao unafanywa na mtaalam wa afya, angalau kila baada ya miaka tatu.

Wanawake ambao wana zaidi ya umri wa miaka 40 wanapaswa kushauriana na daktari wao juu ratiba ya kufanya kipimo cha afya cha matiti (mammogram).

“Licha ya hayo yote, ukaguzi wa matiti unaofanywa na mwanamke mwenyewe ni (breast self-exam-BSE) ni muhimu sana kwa wanawake walio katika miaka 20.
Kama utakuwa na utaratibu wa kujikagua mara kwa mara, utatambua jinsi matiti yako yanavyokuwa na jinsi unavyoyahisi yakiwa katika hali ya kawaida, na utaweza kutambua dalili zozote zilizo tofauti mapema ili uweze kuzungumza na daktari wako mapema iwezekanavyo,” alisema Dk. Ranido.

Kuna dalili mbali mbali ambazo wanawake wanapaswa kuzitambua, kama vile uvimbe ndani ya matiti, mabadiliko ya umbo na ukubwa wa titi, na ni muhimu sana kuongea na daktari wako iwapo utakuwa na shaka au maswali yoyote kuhusu afya ya matiti yako.

“Katika jitihada zetu za kuongeza uelewa wa saratani ya matiti miongoni mwa wanawake barani Afrika, Zahanati yetu ya Mwanamke Mwenye Afya Njema itatoa huduma zilizopunguzwa gharama kwa kipimo cha mammogram kwenye miezi ya Oktoba na Novemba mwaka huu.

African Medical Investments ni wabia na washirika wako katika vita dhidi ya saratani ya matiti,” anahitimisha Dk Thakker.