b..

B1

Wynem

animation

Wednesday, August 18, 2010

WASANII WAFANYIWA USANII MKURANGA.

Baadhi ya wasanii wa Luninga na waigizaji wa filamu, wakiwa kwenye mkutano wa maandalizi ya uzinduzi wa Kijiji kipya cha Wasanii utakaojulikana kama Mji Mpya wa Wasanii. Mkutano huo ulifnguliwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dustan Mrutu, uliofanyika jijini Dar es Salaam miezi kadhaa iliyopita.



Asasi moja inayojitambulisha kuwa inashughulikia wasanii, inadaiwa kutapeliwa mashamba waliyodai kuyanunua katika kijiji cha Mwanzega, wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani kwa ajili ya Waandishi wa habari na wasanii.

Uongozi wa Serikali ya wilaya ya Mkuranga, umetoa maelezo kuwa wale wote waliouziwa mashamba hayo wametapeliwa, kwani si mamlaka za wilaya wala Halmashauri zilizohusika kwa namna yoyote ile katika mchakato huo. Mkuu wa wilaya hiyo,Henry Clemence, amesema tayari jeshi la polisi wilayani humo limeingilia kati na kuwashikilia kwa muda Mwenyekiti wa Kijiji hicho pamoja na viongozi wa asasi hiyo.

Alisema kuwa hadi sasa,Mtendaji wa kijiji hicho hajulikani alipo baada ya kutoroka, kwa kujua kuwa anasakwa na vyombo vya dola.

Clemence alitoa maelezo hayo baada ya watu waliochukuliwa fedha kupitia taasisi hiyo kutua wilayani humo kwa lengo la kukabidhiwa ‘MAENEO YAO’. “Wilaya ya Mkuranga haina ardhi kama hiyo,wilaya hii ipo karibu na jiji la dare s salaam..inapaswa kupangwa vizuri ili ilete manufaa kwa watu wa Mkuranga.

 
Kwa wanaotaka kuja huku (Mkuranga), nawashauri wafuate taratibu,wasivunje amani iliyopo…wanaotaka ardhi wapitie Halmashauri, wasipitie katika asasi wala kwa mtu yeyote kwa sababu taratibu za kumiliki aradhi hazielekezi hivyo,”alisema mkuu huyo.

TAMASHA LA KISWAHILI DAR LAFANA!

hapa watoto kutoka makongo wakionesha vitu vyao

Mpango mzima wa kupata elimu ulikuwepo. Hapo watuwaliohudhuria walikuwa akitazama na kunmunua vitabu mbalimbali vya kiswahili vikiwemo vya hadithi. 

Wanafunzi wa makongo wakishangilia baada ya kupata burudani.

Mtu mzima Ras Lion akichana mistari

washakiji wakitafakari jambo, kuanzia kulia ni Dk John a.k.a Mkoloni, Benjamini wa Mambo Jambo na Roja ambae ndi alikuwa ni Dj wa shoo nzima.

Ize Mchwa kutoka makongo akitoa burudani wakati wa tamasha.
Mwanangu wa kitaa aliyekuwa kwenye kundui la watu pori akifuatilia shoo kwa mbali huku akiwa na wageni wake ambo anfundisha na kiswhili na kuwaezea utamaduni wa mwafrika.
Mkurugenzi wa Art In Tanzania Kari Korhonen aliyeeka mikono mfukoni) akiongoa na baadhi ya wageni waliohudhuria Tamasha hilo kabla ya kuanza kwa tamasha.
Benjamini akizungumza jambo na mmoja wa waandaji wa tamasha hilo.

 CHUOkikuu huria cha Tanzania kikishirikiana na shirika lisilo la kiserekali la Art In Tanzania lenye makao makuu Bahari Beach, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam wameweza kufanya tamasha la kuendeleza Kiswahili lililopewa jina Tamasha la Sauti za kiswahili wiki iliyopita katika kijiji cha makumbusho jijini Dar es Salaam.  Tamasha hilo lilokusanya kila aina ya sanaa na wasanii kibao tu wakiwepo wale wanaofanya sanaa ya asili.  Akizungumza na mtoto wa kitaa mkurugenzi wa Art In Tanzania Kari Korhonen alisema kuwa alivutiwa n asana na propozo iliyomfikia ofini kwake iliyokuwa ikimuombva awe mdhamini wa tamsha hilo “nilifurahi sana na nilishindwa kukataa kudhamini hili tamasha kwa sababu mimi binafsi napenda sana lugha ya Kiswahili”  Tamasha hilo lilijumuisha watunzi wa vitabu maarufu hapa nchini na nchi jirani ya Kenya ambapo walipata nafasi ya kukizungumzia Kiswahili kinavyopendwa hata katika nchi za ulaya.  Kuacha watunzi tamasha hilo lilibeba vikundi mbalimbali vya sanaa za kiutmaduni kutoka chuo cha sanaa bagamoyo, mikoa ya kusini kama vile kikundi cha Jembe Chibweda n wakus, pia kulikuwa na vikundi tofauti kutoka shule ya sekondari Makongo waliokuja na ngoma, sarakasi, nyimbo na kucheza shoo.  Tamashani hapo pia kulikuwa na monesho ya vitu vya kiutamaduni na uuzwaji wa vitabu vya Kiswahili vilivyotungwa na kuandikwa na waandishi mbali mbali katikabara la Afrika kama vile vitabu vya Ngugi wa Thiong’o, mithere Ngugi, Elvis musiba, Marehemu Beni Mtogwa ,Amir Rajabu, Ndyanao Balisija na wingine wengi tu.  Kama akwaida tamasha huwa halinogio kama hakuna burdani bana ….basi pale walikuwepo wasanii kibao tu katika mpango mzima wa kuwaweka sawa wageni waalikwa. Wasanii waliokuwepo katika tamasha hilo ni pamoja na Benjamini wa mambo jambo, Mkoloni, watukutu (john woka na Ras Lion) na D knob.

watoto wa makongo wakionesha ngoma za asili

Tuesday, August 17, 2010

VODACOM FOUNDATION KUTUMIA MILIONI 40/-“SHARE & CARE”

Mgeni rasmi Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaabani Simba akisoma hotuba yake katika viwanja vya Karimjee leo jioni wakati wa Futari iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania kupitia kitengo chake cha Vodacom Foundation maalum kwa watoto yatima wa vituo mbalimbali vya jijini Dar es salaam katika mfungo huu wa mwezi mtukufu wa (Ramadhan) ambapo waislamu kote duniani hufunga kama utekelezaji wa nguzo muhimu katika kumcha mwenyezi mungu.


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation umetenga zaidi ya milioni 40/- katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kusaidia watoto wanaolelewa kwenye vituo vya yatima na wale wanaoishi katika shule za bweni.

Msaada huo unaotolewa kupitia kampeni ya ‘Share and Care’ utawalenga watoto kutoka mikoa minne ambayo ni Dar es Salaam, Tanga, Pemba na Unguja na vifaa kama mchele, unga, mafuta ya kula, madaftari na maharage vitatolewa kama futari kwa watoto hao wanaohitaji upendo hususani katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya kufutari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare alisema kwa kutambua umuhimu wa jamii inayofanya nayo biashara kampuni yake imeona irudishe kiasi cha faida wanayoipata kwa wananchi ili kiwasaidie.
Akifafanua alisema kwamba tangu mfuko huo uanzishwe miaka minne iliyopita umeweza kusaidia jamii mbalimbali ya Watanzania ndani ya mfungo wa Ramadhani kwa mara ya tatu sasa hususani katika nyanja za elimu, watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wale wanaosoma katika shule za bweni na kukosa huduma za chakula.
“Kwa mwaka huu kupitia kampeni yetu ya ‘Share and Care’ tutarudisha tulichokipata na tutaweza kuwafikia watoto zaidi ya 3,000 wa mikoa ya Tanga, Pemba, Unguja na kwa kuanzia tayari tumetoa msaada wa takribani milioni 18/- kwa baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye vituo vya watoto yatima na kutoka shule za bweni mkoani Dar es Salaam,” alisema Mare.

Naye Sheikh mkuu wa Tanzania Mufti Shaban Bin Simba ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema mbali ya hafla hiyo kutoa futari isiyozoeleka majumbani pia imetoa fursa kwa waislamu kutoka maeneo mbalimbali kukutana katika kumi la kwanza na kukumbushana juu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Aidha Mufti Simba licha ya kuishukuru kampuni ya Vodacom Tanzania kwa misaada iliyotoa kwa jamii ya waislamu alisema jambo hilo linahitaji pongezi na kutaka liungwe mkono na kuigwa na kampuni zingine nchini.


“Kupitia kampeni hii ya ‘Share and Care’ mliyoianzisha ili kuisaidia jamii ya waislamu katika kipindi hiki cha mfungo natumaini kampuni zingine zitapata fursa ya kujifunza kutoka kwenu,” alisema.

Tofauti na hayo Sheikh mkuu alitoa rai kwa Vodacom Tanzania kuwa kitendo hicho kizidi kuitia moyo kampuni hiyo na kutumia changamoto waliyoipata kurekebisha kwenye mapungufu na kuboresha zaidi katika mafanikio waliyofikia.

Monday, August 16, 2010

HATIMAE MISS TANZANIA WAINGIA KAMBINI LEO

Mratibu wa Miss Tanzania Ndg. Hashmu Lundenga

MRATIBU wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga amebainisha kwamba warembo wanaowania taji la taifa 'Vodacom Miss Tanzania 2010' wameingia kambini leo Jumatatu Agosti 16.

Aidha amesema kwamba mrembo atakayeshindwa kuripoti leo bila ya kutoa taarifa kwa kamati yake atakuwa amejiondoa mwenyewe katika kinyang’anyiro hicho.

shindano la kumsaka mrembo wa taifa mwaka huu, 'Vodacom Miss Tanzania 2010', litafanyika Septemba 11 jijini Dar es Salaam.

Lundenga, amesema kuwa warembo 31 watashiriki kinyang'anyiro hicho, wakitoka katika kanda mbalimbali nchini.

Alisema warembo hao wataweka kambi katika hoteli ya Giraffe na wakiwa kambini, mbali ya kujifua kwa fainali ya michuano hiyo, watapata nafasi ya kujifunza stadi za maisha ya kila siku.

Lundenga aliwataja warembo waliofanikiwa kupata tiketi ya kushiriki shindano hilo kuwa ni Alice Lushiku, Irene Hezron na Amisuu Malik kutoka kanda ya Kinondoni, Esther Dennis, Gloria Kaale (Chuo Kikuu Dar es Salaam), Shadia Mohammed, Furaha David, Mary Kagali (Nyanda za Juu Kusini), Bahati Chando, Salma Mwakalukwa na Consolatha Lukosi watakaoiwakilisha Kanda ya Ilala.

Wengine ni Flora Florence, Mary Adam, Angelina Ndege wa Kanda ya Mashariki, Genevieve Emmanuel Mpangala, Anna Daudi, Britney Urassa (Temeke), Glory Mwanga, Prisca Mkonyi, Jally Murei (Kaskazini), Gloria Mosha, Chrostine Justine (Chuo Kikuu Huria), Flora Martin, Rachel Sindbad Pendo Sam (Elimu ya Juu), Beatrice Premsingh, Willemi Etami, Pilli Issa (Kati), Fatma Ibrahim, Buduri Ibrahim na Margareth Godson wa kanda ya Ziwa.

Lundenga aliongeza kuwa maandalizi ya shindano hilo yako katika hatua za mwisho na kwamba wasanii mbalimbali watatoa burudani katika siku ya onyesho hilo.

 Watu wangu wa kitaa msijali baadae kidogo mtapata picha za warembo walivyokuwa wakiwasili kambini pale Giraf ocean vew hotel kupitia humuhumu kwenye blog yenu ya kijanja kabisa.

JCB asema muziki wa Bongo haulipi

Mtu mzima JCB


Mwana hip hop mkongwe kabisa,JCB kutoka utengwani pale kijenge ya juu, Ara chug ameibuka na kusema kwamba bado muziki wa Bongo haujaanza kulipa kama inavyotakiwa japo kuwa wasanii wanaendesha magari.

Akichati na Mtoto wa kitaa mawili matatu JCB alisea kwamba wanamuziki wa Tanzania bado hawanufaiki na kazi zao kama ilivyo kwa nchi nyingine.

Sms ya kwanza mtu mzima ya mtu mzima Jcb ilisema…

“Unajua ni nini arifu!? …..Kikweli, muziki wa Bongo bado haulipi. Lakini ukiutazama juu-juu utaona kama unalipa, kumbe sio,” alisema JCB.
JCB aliendelea kuchati na kusema “Muziki wa bongo bado haulipi kiivyo japo mnaona wasanii wanaendesha magari lakini sio wanachostahili kwa kazi wanayoifanya.”

Mtengwa huyu aliyebaki peke yake baada ya wenzake kuhamishia majeshi Marekani JCB amemua kuuza yeye mwenyewe albamu yake, huku akishirikiana na wadau wake tofauti-tofauti.

Katika mpango mzima wa kuisambaza albamu yake JCB alisema kwa sasa yupo nyumbani (Arusha) anaendeleza harakati za hapa na pale huku akiendelea kubana mzigo wake taratibu.

Mkali huyo wa hip hop kwa sasa anatamba na kibao chake cha Ukisikia Paaaa, alichowashirikisha wakali wengine wa Hi Hop kama Fid Q, Jay Moo na Chid Benz, huku ngoma hiyo ikwa imepikwa na mtu mzia Yudi na Jay Mader katika studio ya Tongo Record.
Albamu ya JCB iliyopo mtaani inakwenda kwa jina la Nakala za Makala ikiwa na ngoma 16 alizozifanya katika studio tofauti-tofauti.

JCB alizitaja ngoma zilizopo kwenye albamu yake ya Nakala za maka kuwa ni pamoja na Kijenge ya juu, Tumetoka mbali, Kijiti, Moment of silence, Minato, Bongo fleva part 1&2, Prison break na nyingine nyingi tuu.

ITAFUTE BANA HALAFU USIKIE MAPINI YAKLIYOPO MULE NDANI KWA MAANA NI NOMA

Friday, August 13, 2010

Mikoko ya Vodacom kuwainua washindi kiuchumi

Hapa ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Francois Swart (kulia), akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua promosheni mpya ya ‘Chizika na Mkoko’ ambapowateja wa Vodacom wameshaanza kujishindia kila siku gari jipya aina ya Hundai i10 yenye thamani ya sh. Milioni 12 kwa kutuma ujumbe wa Mkoko kwenda namba 15544. Hafla hiyo ilifanyika Mlimani City, Dar es Salaam. Magari 100 yatashindaniwa. Kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nector Foya, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, Ephraim Mafuru na Vodacom Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald.


 
BAADHI ya washindi wa magari ya Hyundai i10 yanayotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia promosheni yake ya ‘Shinda Mkoko’ wamesema zawadi hiyo itawasaidia kukuza uchumi wao kwani itarahisisha usafiri katika shughuli zao.
Akizungumza kwa njia ya mahojiano kutokea Dodoma baada ya kuibuka mmoja ya washindi wa promosheni hiyo, Tolino Pechaga ambaye ni fundi umeme wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alisema anatumaini gari hilo litakamilisha ndoto yake ya kimaisha katika kujiletea maendeleo.
Akifafanua alisema, ingawa alikuwa akitumia magari ya wafanyakazi kutoka Maili mbili anakoishi hadi Udom, ujio wa Hyundai i10 utamaliza muda wa kukimbizana na basi hilo na kumpa nafasi ya kufanya kazi zake binafsi baada ya muda wa kazi kwa mwajiri wake.
“Unajua mimi ni mwajiriwa wa chuo, lakini nafanya pia kazi zangu binafsi. Usafiri ulikuwa kikwazo namba moja kufikia malengo yangu, lakini sasa kila kitu kitaenda sawa kwani tayari nitakuwa na usafiri wangu binafsi utakaorahisisha maendeleo yangu,” alisema Pechaga.
Kwa upande wake Benard Asenga wa Keko Magurumbasi jijini ambaye ni mfanyabiashara wa duka la bidhaa ndogondogo na vyakula alisema alikuwa akitumia muda mwingi na baiskeli kufuata bidhaa sokoni Kariakoo, lakini gari hilo litamuwezesha kuboresha utoaji huduma kwa wateja wake.
Aidha Asenga alifafanua kwamba mara baada ya kukabidhiwa Hundai i10 aliyojishindia atabadilisha mtindo wa biashara anaoufanya na anafikiria kuwa mjasiriamali wa kati (SME’s ) na kumiliki duka la bidhaa za jumla na rejareja.
“Sasa sitatumia tena baiskeli kufuata bidhaa mjini, nafikiria kukuza biashara yangu kutoka hatua moja kwenda nyingine jambo litakaloniwezesha kukuza hali yangu kiuchumi,” alisema mfanyabiashara huyo.
Naye Simon Kihuru ambaye ni dereva wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songea alisema zawadi hiyo iliyotolewa na Vodacom Tanzania itampunguzia gharama za usafiri kwa ajili kuwapeleka na kuwarudisha watoto wake shule kwani wataweza kutumia gari hiyo kwa matumizi ya binafsi.
“Kama nilivyosoma kwenye magazeti mbalimbali kwamba gari hiyo haitumii gharama kubwa kuihudumia, kwa kuwa mimi ni dereva itaniwezesha kutunza fedha zangu baada ya kukwepa huduma za daladala ambazo sio salama sana hususani kwa watoto,” alisema Kihuru.
Akizungumza hivi karibuni kwenye hafla ya uzinduzi wa promosheni ya ‘Shinda Mkoko’ iliyopanga kuwazawadia wateja wake gari moja aina ya Hyundai i10 kila siku Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema shindano hilo litawahusisha wateja wote wa kampuni hiyo nchini na kwamba ndani ya siku 100 kila siku mtu atakuwa anajipatia gari moja.
Alisema promosheni hiyo ni moja kati ya shughuli zitakazoambatana na maadhimisho ya miaka kumi ya utoaji huduma wa Vodacom Tanzania nchini. Mpaka promosheni hiyo itakapokamilika tayari magari 100 ambayo kila moja litakuwa na thamani ya milioni 12/- yatakuwa yameshatolewa.

HAPPY B'DAY FID Q!

Mtoto wa kitaa kama kawa anakutakia siku kuu njema ya kuzaliwa mtu mzima Farid kubanda. Cha msingi ni kukaza tu katika mambo yako ili u8sirudi nyuma blaza na kumuomba mungu akupe afya kwani afya ndio kila kitu. wana wa kitaa wanasema wana kupenda sana na wanatarajia mambo mazuri kutoka kwako.
HAPPY B'DAY FID Q!

Tuesday, August 10, 2010

Harakati zangu ndani ya Fiesta.

Katika harakati zangu ndani ya viwaanja vya leaders nilkutana na watu kibao tu ambao nilikuwa natarajia kukutana nao lakini hawa ni baadhi tu ya wanangu wa kitaa ambao tulikutana pande zile.

Hapa ni mtu mzima Raymond Mshana (kushoto) akiwa na Boy Sella . Hawa  wana wanatokea pale C2C.

 
apa ni Mtoto wa kitaa (mwenye kapero) akiwa na mtu mzim Izzo Bussiness


Izzo B. akiwa na Boy Sella


Mwanangu Swalehe (wa mble)kutoka kitaa cha cnza nae alikuwepo
Hili ndio nyomi lilokuwepo pale bana. Wote hawa walikuja kushuhudia Fiesta.
Hapa kijana 76 (saba sita) kiwa na Mtoto wa kitaa ndani ya fiesta.

Wednesday, August 4, 2010

Vodacom yaja na ‘SHINDA MKOKO’

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Francois Swart (kulia), akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa promosheni mpya ya ‘Chizika na Mkoko’ ambapo mteja atajishindia kila siku gari jipya aina ya Hundai i10 yenye thamani ya sh. Milioni 12 kwa kutuma ujumbe wa Mkoko kwenda namba 15544. Hafla hiyo ilifanyika Mlimani City, Dar es Salaam. Magari 100 yatashindaniwa. Kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nector Foya, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, Ephraim Mafuru na Vodacom Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Francois Swart (kulia) , na Miss Vodacom Tanzania 2009, Miriam Gerald wakiwa wameshika moja ya mabango kuashiria uzinduzi wa promosheni mpya ya ‘Chizika na Mkoko’ ambapo mteja atajishindia kila siku gari jipya aina ya Hundai i10 yenye thamani ya sh. Milioni 12 kwa kutuma ujumbe wa Mkoko kwenda namba 15544. Hafla hiyo ilifanyika Mlimani City, Dar es Salaam. Magari 100 yatashindaniwa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa KAMPUNI HIYO, Ephraim Mafuru.
01. Magari mawili kati ya 100 yatakayoshindaniwa katika promosheni ya Chizika na Mkoko, yakioneshwa wakati wa hafla ya uzinduzi uliofanwa na Vodacom Tanzania, Mlimani City, Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa promosheni mpya ya Chizika na Mkoko, wakiangalia injini ya moja ya magari aina ya Hundai i10, yatakayoshindaniwa .

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kuanzia Agosti 2 mwaka huu imepanga kuwazawadia wateja wake gari moja aina ya Hyundai i10 kila siku katika promosheni itakayochukua siku 100 (takribani miezi mitatu) baada ya uzinduzi wa kihistoria unaofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Promosheni hiyo itakayofahamika kama ‘Chizika na Mkoko’ ni moja kati ya shughuli zitakazoambatana na maadhimisho ya miaka kumi ya utoaji huduma wa Vodacom Tanzania nchini. Mpaka promosheni hiyo itakapokamilika tayari magari 100 ambayo kila moja litakuwa na thamani ya milioni 12/- yatakuwa yameshatolewa.

Akizungumzia kuhusiana na promosheni hiyo Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema shindano hilo litawahusisha wateja wote wa kampuni hiyo nchini na kwamba kila siku mtu atakuwa anajipatia gari moja.

“Katika kusherehekea maadhimisho haya ya utoaji huduma zenye mafanikio kwa wateja wetu na jamii kwa ujumla, tumeona tutumie fursa hii kumbukumbu ya miaka kumi ya utendaji wa Vodacom Tanzania kwa kurudisha faida iliyopatikana kwa wateja wetu,” alisema Mafuru.

Aidha aliongeza kwamba washindi katika promosheni hiyo watapatikana baada ya kuwa na pointi nyingi watakazojikusanyia ambazo zitachezeshwa kwenye droo ili kumpata mshindi wa promosheni hiyo kila itakapochezeshwa.

Ili kushiriki kwenye promosheni hiyo Mafuru alisema, washiriki wote watatakiwa kujiunga kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15544 kwa gharama ya shilingi 550 itakayotoa nafasi kwa wateja wa kampuni hiyo kujishindia kila siku Hyundai i10 zitakazotolewa kwa siku 100 mfululizo.

Mbali na hilo promosheni hiyo pia itaenda sanjari na washiriki kuulizwa maswali ya ziada watakayohitajika kuyajibu ili na kupata ambapo kila swali sahihi litakuwa na pointi 20 kama zinazotolewa kwa washiriki watakaokuwa wakijiunga kila siku. Pointi hizo zitahesabiwa kadri zinavyoongezeka.

Idadi ya pointi atakazokuwa nazo mshiriki zitawakilisha idadi ya siku ambazo mteja ameshiriki kwenye droo hiyo. Aidha kila SMS mtu atakayoituma itamuongezea idadi ya pointi kwa siku husika na si vinginevyo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru, ni kwamba kadri mshiriki atakavyojikusanyia pointi nyingi ndivyo atakuwa na nafasi kubwa ya kujishindia gari kwenye promosheni hiyo kadri itakavyokuwa ikiendeshwa.

“Kama itatokea mshiriki ama mshindi anajitoa ama kujitoa au asiyetaka kujipatia zawadi, itatulazimu kutomtangaza ama kumtaja,” alisema Mafuru.

Hyundai i10 ni gari inayohimili mazingira ya mijini (hatchback) ambayo imetengenezwa na Kampuni ya magari ya Hyundai Motor Company, na lilizinduliwa rasmi nchini Oktoba 31, mwaka 2007.

Gari hiyo ya gharama nafuu ni rahisi kuihudumia kwani inatumia kiwango kidogo cha mafuta ikiwa pia tofauti na magari mengine ambayo unapoyatumia unajisikia raha na kukuweka huru.

Monday, August 2, 2010

JAM SESSION NI KAMA KAWA KILA J'PILI

Kama kawa jumapili ya wiki hii nilikuwa mitaa ya sinza na nikimpa shavu mwanangu mmoko wa kiitaa kama dawa niliweza kuget mapcha mawili matatu ya ukumbusho pande zile.
kama kawa mtu mzima Charles Benedictor Halawa a.k.a CBH alikuwa kiwakilisha vilivyo na kuandaa na kuendeleza Jam seshen nakama ilivyo kawaida ya jam sesheni inakusanya vijana kutoka sehemu mbalimbali za jiji li dar kwa kukaa na kucheza pamoja.
Hili ni suala la kila jumapili mazeee kwa hiyo kama ulikosa lewiki hii basi tukutane pale jumapili ijayo. ............ Au sio?!.....
Kama vipi cheki na mapicha hapo chini halafu tuooneeeeee!
Mpango mzima wa kucheza shoo kwa pamoja ilikuwa ni kama kawa!
CBH akiwa na Jux
ALLY Sella akiwa na CBH
Hapa ni mtoto wa kitaa akiwa hana habari (yuko bize na simu tu)huku kushoto kwa akiwa ni mtu mzima Ally Sela akiwa anchonga na mrembo.
Mshikaji mmoja akionesha kiatu alichovaa kwa pozi!
Jux akiwa amepozi na Ally Sella
Watu wakijiachia kwenye Dansing floo kama inavyo onekana kwa juu.
Hapa ni CBH akipewa shavu katika kuprezent kipindi cha Jam seshen

Majunki wa kitaa wakifanya vitu vyao.
kama kawaida watu walijiachia
Warembo wakiwa wamejiachia kinoma
CBH akiawa na mtoto wa kitaa
Ally Sela wa televisheni ya C2C akiwa amepozi na mtoto wa kitaa wakisow lav.
Ally Sela akiwa na warembo wa Sinza katika picha ya pamoja
CBH akiwa na mrembo aliekuwa akimsaidia kuendesha kipindi.

Wednesday, July 28, 2010

KALALE PEMA MPENDWA WETU PRIMITIVA

PRIMITIVA PANKRASI

Aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Primtiva Pankrasi, amefariki dunia juzi mchana katika hospitali ya Lugalo ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipofika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu ya kawaida ‘Check up’ kama kliniki ya ujauizito.
Imeelezwa kuwa Primtiva kabla ya kufikwa na mauti alipatwa na presha ya ghafla na kupoteza uhai wakati madaktari wakihangaika kunusuru maisha yake lakini haikuwa bahati kwani sisi tulimpenda sana lakini mungu alimpenda zaidi.
Primitiva anataraiwa kuzikwa kesho jioni majira ya saa kumi katika makaburi ya kinondono.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPOONI - AAAMEN.

Monday, June 21, 2010

Kama kawaida mtoto wakitaa niliibuka wan dei hivi kwenye masuala ya kijamii na kuchangia damu kwenye benki ya damu salama bana ili kuweza kusaidia binadamu wenzetu.
Kudadadadadaki mtoto wa kitaa nikajikita na kuanza kuchonga mawili matau na wasahauri kisha kuto hiyo damu banaa!
Hapa ndio nilifika na nilikutana na mwana mmoko ambaye ni dansa wa kundi la obadaa la hapa bongo.

Hapa nilikuwa kwa mama mshauri bana nikipewa maushauri ya kutosha.
hapa nilikuwa kwenye mpango wa kuchukua kichupa cha kujazia damu




Ndio kama hivyo baana mambo yalivyokuwa karibuni na nyie wengine mje kutoa na kchangia hiyo damu bana tuwasaidie wenzetu wakitaa.