b..

B1

Wynem

animation

Tuesday, March 20, 2012

AFYA YA KAMANDA GULUMO INAENDELEA VIZURI

Msanii Mkongwe wa bendi Kwongwe ya Msondo Ngoma Music, Muhidini Gurumo akiwa katika hospital ya Taifa Muhimbili, Dar es salaam jana, akipimwa mapigo ya Moyo na Ofisa Muuguzi Msaidizi wa Hospital hiyo,Suraiya Mohamed alipolazwa kufanyiwa uchunguzi wa kina toka mwishoni mwa wiki iliyopita. (Picha na www.burudan.blogspot.com)

Na Mwandishi
MWANAMUZIKI Wetu maarufu wa bendi kongwe ya  Msondo ngoma, Muhidin Gurumoaliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ugojwa wa shinikizo ladamu anaendelea vizuri.Akizungumza na Dar es Salaam jana,Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila'Super 'D' alisema Afya ya  Gurumo inaendelea vizuri na wakati wowoteanaweza kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo.Alisema kuwa madaktari wanataka kuchukua vipimo vya mwisho kwa kinakujua kila kitu kinachop msumbua  katika mwili wake."Kwa sasa tunashukuru Mungu afya ya Gurumo inaendelea vizuri tofautina mara ya kwanza na akiendelea hivi anaweza hakurusiwa hivikaribuni"alisema Super D.Hata hivyo aliwataka wapenzi wa bendi hiyo kumuombea duwa mwanamzikihuyo ili apone upesi pia aliongeza kwa kusema maonesho yao ya wikiihii ni kama ifuatavyo Alhamisi watakuwa Mwandege Mkoa wa Pwani,Ijumaawatapiga katika viwanja vya Lidaz Clab jumamosi watakuwa katikaviwanja vya TCC Sigara na Jumapili watamaliza wiki endi katika ukumbiwa Max Bar uliopo Ilala Bungoni alisema Super D.

Sunday, March 18, 2012

KITU MIA KUTOKA KWA MTU CHEE

RAMADANI SHAULI GABRIEL OCHIANG WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO KESHO

Mabondia Ramadhani Shauli wa Tanzania (kushoto) na Gabliel Ochiang wa Kenya wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito, Dar es salaam LEO kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika KESHO katika ukumbi wa friens Coner Manzese.
Bondia Ramadhani Shauli akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Gabriel Ochiang wa Kenya kulia.
Mabondia Ramadhani Shauli wa Tanzania (kushoto) na Gabliel Ochiang wa Kenya wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito, Dar es salaam LEO kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika KESHO katika ukumbi wa friens Coner Manzese.
Baadhi ya mabondia pamoja na viongozi wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupima uzito leoBondia Gabriel Ochiang wa Kenya akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Ramadhani Shauli kushoto.
picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

Friday, March 16, 2012

KAJALA KIZIMBANI

MSANII wa filamu nchini Kajala Masanja na mumewe Faraja Chambo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kula njama, kuhamisha umiliki wa nyumba na kutakatisha fedha haramu. Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alidai kuwa mwaka 2010 , Kajala na Chambo walikula njama ya kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala wilaya ya Kinondoni kinyume na kifungu cha 34 cha sheria ya rushwa ya mwaka 2007 sura ya 11. Swai alidai kuwa Aprili 14, 2010 jijini Dar es Salaam washtakiwa hao kwa pamoja kinyume na kifungu cha 34 (2)a(3) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa walihamisha umiliki wa nyumba hiyo iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam. Alidai kuwa siku hiyo ya Aprili 14,2010 washtakiwa hao ambao ni mtu na mkewe walifanya uhamisho wa umiliki wa nyumba hiyo iliyopo Kunduchi Salasala ambayo ilipatikana kutokana na fedha haramu. Wakati kesi hiyo ikiendelea Kajala pekee ndiyo aliyokuwepo mahakamani hapo na mumewe Chambo ambaye anakabiliwa na kesi nyingine za kutakatisha fedha haramu mahakamani hapo hakuwepo. Katika kesi hiyo, Kajala anatetewa na Wakili Alex Mgongolwa ambaye alidai mahakamani hapo kuwa Wakili huyo wa Takukuru , Swai hana mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba hati ya mashtaka inamapungufu. Akijibu hoja: Wakili Swai alidai kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliteua mawakili wa Takukuru chini ya Government Notice (GN) 168 ya mwaka 2010 na kuwaruhusu kuendesha kesi zisizokuwa za rushwa na kwamba katika uteuzi huo yeye alikuwa ni mmojawapo. Hivyo anauhalali wa kuendelea kuendesha kesi hiyo. Hakimu Fimbo ameiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 20, mwaka huu atakapotoa uamuzi juu ya hoja hizo.
HABARI KWA HISANI YA MWANANCHI

Thursday, March 15, 2012

MPIGIE KURA YOUNG D.

GALILE VS MASHALI WATAMBIANA KILA MMOJA KUNYAKUA UBINGWA

Mabondia, Selemani Galile kushoto na Tomasi Mashali wakitazamana kwa usongo wa kila mmoja kutaka kuchukua mkanda wa ubingwa wa mchezo wa masumbwi wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini TPBO walipokuwa wakitambulisha mpambano wao. Dar es Salaam jana, utakaofanyika Apri 9.katikati ni Rais wa Oganaizesheni hiyo Yasin Abdallah Mwaipaya.

Na muwandishi wetu
MABONDIA Selemani Galile na Thomas Mashali wanatarajia kupanda ulingoni Aprili 9 kuwania mkanda wa ubingwa wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) litakalofanyika katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa kati uzito wa kg 75 raundi 10 likiratibiwa na TPBO.
Wakitambiana Dar es Salaam jana, wakati wa kuonyeshwa mkanda huo Galile alisema atahakikisha anafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika atauchukua kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao.
"Mkanda lazima niiuchukue kwani najua Mashali haniwezi na hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo najiamini na mkanda ni wangu," alisema Galile.
Naye kwa upande wake Mashali alisema raundi 10 ndio zitaamua mkanda ni wanani lakini anaimani ataunyakuwa kwani anamazoezi ya kutosha na bado ataendelea kujifua na kuhakikisha anaibuka bingwa.
"Ninauwezo, nimejipanga na ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote raundi 10 ndio zitaamua nani bingwa," alisema.
Naye kwa upande wake Rais wa TPBO, Yassin Abdalah alisema mkanda huo ulikuwa wazi hivyo wakaamua kuwaambia mapromota ambapo alijitokeza Prospa Rweyomamu ambaye ndio ameandaa pambano hilo hivyo bingwa atakayepatikana ndio utakuwa kwake akisubiri mpinzani.
Mbali ya kuwepo na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na huuzwaji wa DVD za Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi wakiwemo mabondia Lenox Lewis, Evander Holfiled,David Haye, Waldmil Klitichiko,Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roj Jones na wengine wengi
Zitakuwa zikisambazwa kwa ajili ya kuwapa mabondia,mashabiki marefarii kutambua sheria na kanuni za mchezo huo Duniani ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila Super D Alisema kuwa tangia aanze kutoa mafunzo kwa njia hiyo watu wengi wameanza kuwa na uwelewa wa mchezo wa masumbwi nchini kwa kutambua sheria na mambo mbalimbali ya mchezo alisema Super D boxing Coach ambapo mpaka sasa ameweza kutoa matoleo nane tofauti ya mabingwa wa ngumi Duniani Akichanganya na mabondia wa Nchini.

 Pix.Capition

Wednesday, March 14, 2012

AIRTEL YAZINDUA INTERNET YA 3.75G


Meneja Masoko wa Airtel Bw Salim Madati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya huduma mpya ya 3.75G katikati uzinduzi uliofanyika leo katika makao makuu ya Airtel Morocco ambapo sasa wateja wa Airtel wataweza kupata huduma ya internet iliyo ya kasi na kuwapatia ufanisi Zaidi katika shughuli zao za kila siku.



Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sam Elangallor akionyesha jinsi gani huduma ya 3.75 inavyoweza kutoa huduma ya internet iliyo ya kasi na kuwawezesha wateja wa Airtel kufanya video call wakati wa  uzinduzi wa huduma ya 3.75 iliyofanyika makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na waandishi wa habari , wakishuhudia (kulia) ni mkurungezi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya na (kushoto )ni Meneja masoko Salim Madati.


Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sam Elangallor akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa halfa fupi ya  uzinduzi wa huduma ya 3.75G  ambayo itatoa huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi  kwa watumiaji wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet wawapo mahali popote. Uzinduzi huu ulifanyika katika makao makuu ya Airtel morocco





Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sam Elangallor na mkurungezi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya  kwa pamoja wakionyesha jinsi gani huduma ya 3.75G  ilinavyoweza kuwawezesha wateja wa Airtel kupata huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi kwa watumiaji wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet ikiwa ni pamoja na  kufanya video call wakati wa halfa fupi ya uzinduzi wa 3.75G  iliyofanyika makao makuu ya Airtel Morocco.




Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangallor akiinua modem na kumkabidhi Mwandishi wa habari kutoka TBC Jane John aliyejishindia modem wakati wa uzinduzi wa huduma ya 3.75G iliyofanyika makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wakishuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa Airtel








Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Bi Beatrice Singano Mallya akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma ya 3.75G uliofanyika leo katika makao makuu ya Airtel Morocco ambapo sasa wateja wa Airtel watapata internet yenye ubora na kasi  zaidi  , Pichani ni Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangallor 



Airtel yaja na internet ya 3.75G kutoa ubora na kasi zaidi kwa wateja.
•    Airtel yajenga mtandao bora wa data barani Afrika
•    Uzinduzi wa Airtel 3.75G Tanzania utawapatia watumiaji  wa data
huduma yenye kasi na ubora zaidi  katika simu zao
•    Kupitia internet ya 3.75 itawawezesha wateja kufanya maongezi ya
simu ukiwa unamwona mtu, kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na
kuperuzi na kupata miziki kutoka kwenye tovuti kupitia simu zao.
Jumanne 13 Machi 2011, Dar es Saalam–Airtel Tanzania leo imepiga hatua
kubwa katika kujenga na kukuza mtandao wa technoloijia ya 3.75G Africa
kwa  kuzindua rasmi  mtambo wa 3.75G nchini Tanzania,ambapo Airtel
itatoa huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi  kwa watumiaji
wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet wawapo mahali popote.
Mkurungenzi Mkuu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam
Elangalloor alieleza” kukua kwa technolojia hii kutakuza ufanisi
katika vyombo mbalimbali vya  mawasiliano (multimedia), kwa kuwa 3.75G
itatoa internet yenye ubora na kasi  zaidi kwa  kuwezesha wateja
kufungua tovuti mbalimbali, kufanya maongezi  ya simu kwa njia ya
video , kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na pia  kupata
muziki kutoka kwenye tovuti  kwa kutumia simu
Teknologia ya 3.75G itatoa nafasi kwa wateja kupata mawasiliano ya
data kwa njia tofauti na ya pekee kabisa, ndio maana leo Airtel
tunajisikia fahari kuwa internet yetu ya 3.75G ni uvumbuzi na
muendelezo wa mtandao (platform) wetu ili kuwawezesha wateja wa Airtel
wote nchini kupata huduma ya internet au data yenye ubora wa hali ya
juu pamoja na kasi zaidi”
Tunafanya ubunifu wa kuleta huduma zenye ubora zaidi katika mtandao
kwa kuzingatia kuwa sasaivi dunia inauhitaji mkubwa sana wa huduma za
kimtandao hasa kupitia simu ya mkononi
Ukirejea takwimu zilizofanywa na kampuni ya McKinsey & Co.
Telecommunications zinaonyesha  mpaka sasa kuna watumiaji wa simu za
mkononi wapatao milioni 400 Afrika, na kwamba bara la  Afrika ni moja
kati ya  soko linalokuwa kwa kasi zaidi huku soko la simu za mkononi
likiendelea kukua na kupanuka zaidi na kufikia kutoa huduma za
internet, huduma za benki kwa njia simu (mobile banking)  na biashara
kwa njia ya mtandao yaani (mobile commerce) .

Hivyo basi kwa kuzingatia hili,  ndio maana Airtel tunaendelea na
mikakati kama hii ya kuwaletea wateja internet yenye kasi zaidi ya
3.75G ambayo ni sambamba  na lengo letu la kuendea kupanua mtandao
ili kutoa mwanya wa mawasiliano kuwafikia wakazi wengi wa vijijini
ambao walikuwa wamesahaulika na mapinduzi ya mawasiliano katika bara
la Afrika.
“wote tunafahamu kuwa mawasiliano ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya
jamii ya sasa lakini bado kunachangamoto kubwa sana katika kupata
huduma hii kwa baadhi ya sehemu barani Africa. Lakini tukumbuke
Mawasiliano ni haki ya msingi kwa kila mtu na si vinginevyo hivyo kwa
kupitia mtandao wa Airtel internet yenye kasi zaidi ya 3.75G ninaamini
tutaweza  kuunganisha idadi kubwa ya watu kwa kukuza mahusiano ndani
na nje ya ya jamii zetu, kuendeleza na kuutangaza utamaduni wetu,
pamoja na kupanua wigo wa wale wanaofanya biashara kupitia mtandao wa
internet “ Aliongeza Elangalloor.
Ikiwa tayari mteja ameunganishwa na teknologia ya 3.75G simu yake
itaonyesha 3.75G, HSDPA, WCDMA or HSPA. Hii inategemeana  na Aina ya
simu aliyonayo mtumiaji lakini kasi ya kuunganishwa ni yenye ubora
zaidi.
Airtel itaendelea kuwekeza kwenye huduma ya data katika soko lake lote
huku lengo likiwa ni kuwa mtandao mpana zaidi wa teknologia ya 3.75G
katika bara zima, na itaendelea kutoa huduma bora na inayokidhi
mahitaji ya watumiaji



Tuesday, March 13, 2012

MSONDO NGOMA YENDELEA KUTOA BURUDANI KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR

Msanii Mpya wa bendi ya Msondo ngoma, Shabani Lendi (kushoto) akipuliza Saxphone wakati wa onesho la bendi hiyo iliyofanyika jumapili katika Ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni wengine ni Hamisi Mnyupe, Romani Mngande na Msemaji wa Bendi hiyo Rajabu Mhamila Super D 
Waimbaji wa bendi ya Msondo ngoma wakiimba wakati wa onesho lao lililofanyika jumapili katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni kutoka kushoto ni Hasani Moshi,Shabani Dede,Msemaji wa Bendi hiyo Rajabu Mhamila Super D na mwimbaji Juma Katundu.
Msanii mpya wa bendi ya Msondo ngoma Shabani Lendi Akifanya vitu vyake wakati wa Onesho Hili.

Monday, March 12, 2012

MAN U YAREJEA KILELENI


MANCHESTER, England
MANCHESTER United imefanikiwa kurejea kileleni katika Ligi Kuu ya England baada ya kuifunga West Brom mabao 2-0, wakati Manchester City ikipata kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Swansea City. Man United ambayo ilikuwa ikishika nafasi ya pili kabla ya mechi ya jana kwa muda mrefu, imefanikiwa kupanda kileleni kwa tofauti ya pointi moja, ambapo kwa sasa inaongoza ikiwa na pointi 67 wakati Man City ina 66 na timu zote zikiwa na mechi 28.Katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, Wayne Rooney ndiye aliyeipatia Man United mabao yote mawili katika dakika ya 31 kisha kumalizia la pili kwa penalti dakika ya 71. 
Kwenye Dimba la Liberty, Luke Moore ndiye aliyefunga bao pakee la Swansea katika dakika ya 83. Man City ilipigana kusawazisha bao hilo lakini hali ya mambo ilikuwa ngumu.

Sunday, March 11, 2012

SIKU YANGU YA JANA PANDE ZA KAWE BEACH.

Hapa ndio tulikuwa tumefika Kawe Beach Kuanzia kulia ni mtu mzima Salu Boy, Villy na Abell.
Mwanagu Saidawg akistua wana wengine kuwa leo tupo kitaa cha Kawe Beach, huku Villy akimuita Mhudumu.
Mhudumu alifika na Kutusikiliza

Sule Junior a.k.a Mtoto wa kitaa Na Saidawg.
Baada ya mambo yote mzigo ukaendelea. Hapa nikiwa na wanangu Villy (kushoto), Saidawg (wapili kutoka kushoto), mimi mwenyewe Mtoto wa Kitaa na wa mwisho kulia ni Abel. Huku nikisukuma mzigo taratibu maana mimi huwa kazi popote a.k.a ofisi ni niliposimama.

Friday, March 9, 2012

MKALI WA FACEBOOK KUPIGA SHOO KESHO VIWANJA VYA POSTA KIJITONYAMA

Msanii wa Mziki kutoka South Africa, Cleopas Monyepao (DJ Cloe) kulia akizungumza na waandishi wa habari, Dar es salaam jana kuhusu onesho lake la leo litakalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama kushoto ni Msanii aliyeongozana nae Dumiseni Mkihanya
Msanii wa Mziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo  A.K.A Ommy Dimpoz kushoto akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo kuhusu Onesho lake litakalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama kulia ni msanii kutoka, South Africa, Cleopas Monyepao (DJ Cloe) na Dumiseni Mkihanya na Meneja wa Kinywaji cha Savana, Diana Musheruzi.

Na Mwandishi Wetu

CLEOPAS Monyepao maarufu kama DJ Cleo mkali wa nyimbo ya Facebook kutoka Afrika Kusini kesho anatarajia kutoa burudani katika viwanja vya Posta, Kijitintama Dar es Salaam.
Dj Cleo ameambatana na wachezaji wake Dumisani Makihanya 'Bleksem' na Dj Soul T ambaye amekuwa akionekana katika video mbalimbali za nyimbo zake.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Dj Cleo alisema amefurahishwa sana na ujio wake hapa nchini ikiwa ni kwa mara ya kwanza na hiyo ni kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili.
Alisema, anaamini katika onesho lake hilo la kesho atajifunza mengi kutoka kwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kuwajua wanamuziki na muziki wa hapa nchini sambamba na Utamaduni kwa kiasi fulani.
Aliongeza kuwa anahitaji sana kujifunza utamaduni wa Tanzania kwani nchi hizo zinashirikiano mkubwa na zinaendana kwa mambo mbalimbali kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na muonekano wa wananchi wake.
Alisema, kwa upande wa burudani atawapa mashabiki burudani nzuri na ambayo wataridhika nayo ingawa mashabiki wengi wanaujua wimbo wake wa Facebook lakini yeye ananyimbo nyingi hivyo zitakuwa ni 'Supries' kwao.
"Watu wengi wanaujua wimbo wangu wa Facebook lakini zipo nyimbo nyingi ambazo zitakuwa ni mpya kwao na ninaamini watazipenda hivyo waje kwa wingi ili waweze kujionea na kusikia," alisema.
Naye kwa upande wake mmoja wa wanamuziki ambao wataimba jukwaa moja na DJ Cleo, Omari Nyembo 'Ommy Dimpoz' alisema, anajisikia faraja kubwa kupanda jukwaa moja na msanii huyo kwani anaimani naye atajifunza mengi kutoka kwa msanii.
Alisema, kupanda jukwaa moja na wasanii wa nje kunawasaidia muziki wao kufahamika Kimataifa zaidi kwani utajulikana ukilinganisha kazi yake hasa mwanamuziki huyo ni ya Udj.
Sambamba na wanamuziki hao pia jukwaa hilo litapambwa na Suma lee, Dully Sykes, Juma Nature, Tip Top Conection, Wanaume Halisi, Chege na Temba, Wanaume TMK na Wakali Dancers


Thursday, March 8, 2012

BAADHI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI NCHINI TANZANIA (2010 / 2011)


 Upokeaji wa kitabu kwa ajili ya wanafunzi, The Dutches of Cornwall Camilla
Parker Bowles (kushoto)akikabidhi kitabu kwa Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete kwenye viwanja vya WAMA jijini Dar es Salaam (kulia) kitabu hicho ambacho kimetimiza idadi ya vitabu milioni moja vilivyotolewa na kutoka kwa taasisi ya British Charity READ International. (2012).

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kulia) akijadiliana na wanafunzi wenye  vipaji maaluum  katika maabara ya chuo hicho jinsi ya upasuaji wa mnyama .Mama Kikwete alitembelea Malaysia 2011.
Mkee wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaonyesha watoto jinsi ya kunawa mikono salama na sabuni wakati wa maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam 2011.

Picha ya chini,  wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki matembezi ya kuchangia watoto jijini Dar es Salaam 2011, (kulia) ni Picha ya kushoto, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki matembezi ya kuchangia watoto jijini Dar es Salaam 2011,(kulia) ni Mkurugenzi wa Benki ya Barcklays Kihara Maina.
Yameandaliwa na Mdau Mwanakombo Jumaa

Monday, March 5, 2012

ILIVYOKUWA KWENYE MECHI KATI YA BONGO KEDI NA MWANZA KOMEDI.

Kikosi cha Komedi toka Mwanza katika pcha ya pamoja kabla ya mchezo.
Kikosi cha Bongo Komedi toka Dar es salaam katika picha ya pamoja kabla ya mchezo
"Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mh.Said Amanzi iliupate mikono ya wachezaji hawa wa nyumbani kwako lazima utupie ngawira kwenye chungu....!!!"
Mheshimiwa aliambiwa na msanii huyu ambaye ndiye alikuwa mganga wa timu ya Bongo Komedi na shahidi alikuwa kingwendu na wenziwe "Mheshimiwa umenishika mimi baaaaassss!!! tushashinda...."
Mganga wa Komedi Mwanza kushoto na shabiki...

Mshambuliaji Tale toka Bongo Komedi alikuwa mwiba kwa ngome ya Komedi Mwanza hapa ni kana anapiga vile .... anafinyaaa.....
Mara goliiiii....
Sharo Millionaire ni moja kati ya wachezaji walokuwa wasumbufu kwenye mchezo huo na of coz alitupi lake moja...
Nkabaaaa!! Hili ndilo bao la Sharo Millionaire ambapo mengine yalifungwa na Tale ambaye alifunga mawili na jamaa mwingine hivi.....
Mashabiki na macho yao kwenye stage mara baada ya dakika 90 kumalizika.

Mtanga alipata shavu sana toka kwa watoto naye bila hiyana....flash!
Man of the match Tale akiwapa wakazi wa Mwanza rubudani...
Mfuniko wa maraha.

Ni burudani toka kwa Sharo Millionaire na wenzake Bongo Komedi toka jijini Dar wakitoa rubudani kwa stage CCM Kirumba Mwanza leo.
Timu ya Bonggo komedi ilibuka kifua mbele kwa ushindi wa goli 4-3.