Tuesday, January 28, 2014

MCD WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNI USIKU HUU


MCD.JPG.jpg
MCD enzi ya uhai wake

Mpiga Tumba mahiri katika muziki wa dansi hapa nchini, Soud Mohamed, ambaye pia alifahamika sana kwa jina la MCD, amefariki Dunia usiku huu  katika hospitali ya KCMC mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro alikokuwa amepelekwa kwa matibabu. MCD ambaye alikuwa na bendi ya African Stars a.k.a Twanga Pepeta na baadae akahamia bendi ya Mashujaa Band na Kurudi tena Twanga Pepeta amepatwa na mauti hayo usiku huu, Taarifa za kifo cha MCD zimethibitishwa rasmi na Msemaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Hassani Rehani.
Tutazidi kupeana taarifa za msiba huu kwa kadri  zitakavyokuwa zikitufikia.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
AMIN.

Chanzo - MTAA KWA MTAA

No comments:

Post a Comment