b..

B1

Wynem

animation

Sunday, March 10, 2013

HABARI GROUP YAFANYA HARAMBEE NA KUFANIKIWA KUKUSANYA ZAIDI YA MILIONI SITA


Mratibu wa Kikundi ya HABARI Group Bi.Rabia Bakari akikabidhi risara ya kikundi hicho wakati wa uzinduzi 

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki katikati akichangia katika harambee ya kikundi cha Habari Group ambao ni waanishi wa Habari waliojikusanya kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na pia kuhudumia jamii isiyojiweza kikundi hicho kinaendeshwa chini  ya jumuiya ya kukuza uchumi Ilala 'Jukuila' kikundi hicho kimezinduliwa March 8 Mlezi akiwa ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angela Kairuki wa pili kulia Udhinduzi huo umedhaminiwa na Mfuko wa Pesheni wa PPF pamoja na Hotel ya Lamaa kushoto ni mratibu wa hafla hiyo Bi, Rabia Bakar

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki kushoto akiangalia baadhi ya dokomenti

Wana kikundi cha Habari Goup wakijitambulisha mbele ya mgeni rasmi.
Picha zote na www.burudan.blogspot.com

Saturday, March 9, 2013

NEW SONG FROM SOPRANO MUSIC - AMENISAHAU



AWADH SALEHE: KIFAA CHA WORLD OF BENEFIT CHENYE MAKEKE MENGI!

Na Magreth Mgina
Awadh Saleh, si jina zito sana katika tasnia ya filamu lakini kwa wale ambao wameshashuhudia uwezo wake katika kazi ya uigizaji wa filamu wanakiri kwamba ni kifaa kinachoweza kuwatingisha nguli wengi wa tasnia hiyo.
Mbali ya umbo lake lenye muonekano wa kina Roberto de Niro, Antonio Banderas na wengineo, Awadh ana vitu vingi vilivojificha ambavyo hujitokeza wakati wa kazi tu. Staili ya uigizaji wake, umakini wa kuisoma na kuielewa script na jinsi anavyoweza kubadilika kwa kila muigizaji anayekutana naye ndivyo vitu vinavyodhihirisha uwezo wake katika tasnia hii ya filamu.
Awadh Saleh ni miongoni mwa washiriki wa filamu ya World of Benefit iliyowakutanisha nguli kama Mzee Chilo, Mama Mjata, Rose Ndauka na Hemed Suleiman Phd. Ameweza kuonesha uwezo mkubwa ndani ya filamu hiyo kiasi cha kuwashangaza nguli hao.
Pia ndani ya filamu ya World of Benefit, Awadh amekutana na wasanii damu mpya kama vile mwanamuziki Ali Timbulo, visura Tutti Rahman, Miriam, Latipher Mkuu na Natalia.   
Wengi watapata fursa ya kushuhudia makeke yake ndani ya filamu ya World of Benefit ambayo imemalizika kuchukuliwa picha hivi majuzi na sasa iko katika editing.


Wednesday, March 6, 2013

MWENYEKIT WA JUKWAA LA WAHARIRI, ABSOLOM KIBANDA AVAMIWA NA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI



 Pichani ni Ndugu Absalom Kibanda akiwa amelazwa kwenye moja ya chumba cha matibabu,hospitali ya Taifa Muhimbili.Get Well soon Absalom Kibanda.Picha kwa hisani ya Mtandao wa Mabadiliko.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri, na Mhariri Mkuu Mtendaji wa New Habari Coperations Ltd, Ndugu Absalom Kibanda, amevamiwa usiku  wa kuamikia leo akiwa anashuka nyumbani kwake Mbezi Beach na watu wasiofahamika na kumpiga kichwani. Amepata majeraha Makubwa kichwani na hasa jichoni,aidha taarifa inaeleza kuwa baada tukio hilo Kibanda alikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu.
Wadau hii ni taarifa ya kushtua sana,lakini tutazidi kutaarifiana kadiri ya habari zitakavyokuwa zinapatikana,kikubwa tumwombee Mungu amponye haraka mpiganaji mwenzetu.
Kwa hisani ya Michuzi Blog

Monday, March 4, 2013

JAPHET KASEBA ALIPO MSAMBALTISHA MANENO OSWAD


Bondia Japhert Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Maneno Osward wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa taifa Kaseba alishinda kwa point

Bondia Japhert Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Maneno Osward wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa taifa Kaseba alishinda kwa point

Bondia Aliphonce Mchumiatumbo kushoto akioneshgana uwezo wa kutupiana masumbwi na Josephe Marwa mpambano wa uzito wa juu uliofanika jumamosi Mchumiatumbo alishinda kwa K,O raundi ya sita

Bondia Japhert Kaseba akinyooshwa mkono juu na refarii Antoni Ruta baada ya kuibuka mshindi kwa kumgalagaza Maneno Osward. 
Pichazote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Sunday, March 3, 2013

ILIVYOKUWA KWENYE UTENGENEZAJI WA FILAMU YA WORLLD OF BENEFIT PANDE ZA UWANJA WA NDEGE WA MWL. J.K. NYERERE

Filamu hii ya  WORLD OF BENEFIT imewashirikisha wasanii kama Rose Ndauka, Timbulo, Hemed phd, Awadh, Mzee chilo Mama Mjatha na wengine
Kaa tayari kwa ujio wa FILAMU HII

OCHU SHEGGY FEAT. ANETH OFFICIAL HD ( EMPTYSOULZ PRODUCTION)

Saturday, March 2, 2013

TIMU NZIMA IKIWA KAZINI

Kama inavyoonekana hapo ni timu nzima ya graphic designers wa gazeti la mwananchi na mwananspoti na MCL kwa jumla wakiwa bize na kazi.

Wednesday, February 27, 2013

NEW HIT FROM KING KAPITA FT GODZILLAH - KUNA TATIZO KWANI?


SAMIR NA PHILIP KOTEY KUWANIA UBINGWA WA AFRIKA UZITO WA 'MIDDLE'

    Philip Koyey akishushuana makonde na bondia Kelly Brook owa Uingereza

Na Mwandishi Wetu
Nchi ya Ghana iko katika hekaheka na bashasha za mapambano kadhaa ya ngumi mwezi wa Machi tarehe 30 wakati ubingwa maarufu wa middle weight utakapo gombaniwa na mabondia Issah Samir na Philip Kotey. Wawili hawa ni maarufu sana katika tasnia ya ngumi nchini Ghana na barani Afrika kwa ujumla. Watakutana wakati wanapogombea mkanda wa IBF AMEPG uzito wa middle.
Muziki wa aina ya Tangle unahitaji watu wawili kuucheza na ndivyo hivyo miamba hii miwili itakapokutana kwenye "musiki wa masumbwi" ulingoni wakati kila mmoja wake atakapoonyesha ulimwengu kuwa yeye ndiye bondia maarufu zaidi katika bara la Afrika uzito wa middle.
Pambano hili linaandaliwa na GoldMike Boxing Promotions Syndicate, kampuni inayoongozwa na bw. Michael Tetteh pamoja na kigunge mmoja wa biashara za vyalula vilivyokaushwa wa Ghana bw. Henry Many-Spain ambaye pia ni Mamamu wa rRis wa IBF Africa idara ya fedha.
Hivyo siku ya Machi 30, miamba hii miwili itakutana katika mpambano uliopewa jina la “Watoto wa Nkrumah” jina lilaloheshimika sana katika nchi ya Ghana kutokana na Rais wake wa kwanza Mh. hayati Kwame Nkrumah!   
Nchi ya Ghana imejitokeza kuwa maarufu katika michezo na inajizatiti kuendeleza michezo yote hususan mpira wa miguu na ngumi. Ni nchi ambayo imeshawahi kutoa mabingwa wengi wa dunia kama kina Azumah Nelson na Ike Quartey ambao walikaa na mataji ya ubingwa ngumi kwa iaka kadhaa na kulitangaza vyema bala la Afrika.
Sasa ni juu ya miamba hii miwili kuafuata nyayo za akina Azumah Nelson, Ike Quartey, Joseph Agbeko na wengine wengi!

IBRAHIMU MAOKOLA AJIFUA KWA AJILI YA MPAMBANO WAKE MARCH 2


Bondia Ibrahimu Maokola akifanya mazoezi ya kupiga panch bag wakati wa kujiandaa na mpambano wake na Rajabu Majeshi utakaofanyika katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa March 2  Mpambano huo utakua wa utangulizi kabla ya mpambano wa Maneno Osward na Japhert Kaseba.
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Wednesday, February 20, 2013

KAMA ZAMANI YA MWANA FA KUTOKA FEBRUARI 25, 2013



Ile track iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki, KAMA ZAMANI kutoka kwa MwanaFA akiwashirikisha wakongwe wa burudani nchini, Kilimanjaro Band (NJENJE) pamoja na Mandojo & Domokaya sasa kutoka Tarehe 25 mwezi huu.
Kwa mujibu wa MwanaFA, alisema track hiyo itapatikana moja kwa moja katika mitandao mikubwa inayouza na kusambaza muziki duniani yaani iTunes, Amazon na Spotify na kuomba fans wake waupate huko.

NGOMA MPYA YA JCB & MOPLUS FT DOMO KAYA - NIENDE WAPI


Monday, February 18, 2013

NGOMA MPYA YA GRACE MATATA Ft OTUCK WILIAM - IMBA NAMI

Grace Matata ft. Otuck Wiliam
Song : Imba Nami
Produced by : Willie HD & Duke Gervalius
Studio: M Lab records.

Friday, February 15, 2013

MSANII GOLDIE AFARIKI


Goldie akiwa na Prezzo - enzi za uhai wake
***************

Mwakilishi wa nigeria katika shindano bba-2012,goldie amefariki masaa machache baada ya kuwasili nchini humo,taharifa zinasema muda mfupi baada ya kutua na ndege nchini nigeria.
Hhali ya msanii goldie ilibadilika ghafla, kufikia kukimbizwa hospitali ambako hakuchukuwa muda, alifariki dunia, usiku wa jana.
Rafiki wa karibu wa goldie, ambaye pia ni msanii kutoka nchini Kenya, CMB-Prezzo alitua mjini lagos-nigeria akitokea kenya, tayari kwa maandalizi ya tv-show ambayo ilikuwa ni project yake Prezzo na marehemu Goldie, inasemekana pia moja kati ya mipango ya marafiki hawa wawili, lilikuwepo swala la ziara ya kutembelea baadhi ya nchi za africa mashariki,i kiwemo tanzania, uganda na kenya, wakati dhumuni lilikuwa ni kuitangaza single mpya ya Goldie iitwayo -Skibobo
Goldie pia amefanya wimbo na msanii kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya 'AY' 

...MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI-AMEN.

NGOMA MPYA YA SUMA MNAZALET FT DANNY JOE - AHSANTE


Sunday, February 10, 2013

VUMILIA - DUSHE DUSHE

MABONDIA FRANISIC MIYEYUSHO VS SADIK MOMBA KUPAMBANA PASAKA


Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishina msuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka.

Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishina msuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka, wanashudia katikati ni Promota wa mpambano huo, Kaike Silaju na Makamu wa Rais wa PST, Aga Peter.
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com