Tuesday, June 11, 2013

MABONDIA WA DAR NA MORO KUPAMBANA JUNE 16

http://1.bp.blogspot.com/-tDDjbjkF5XQ/UaOhMmh9ogI/AAAAAAAADDw/h6es6QeF9jc/s1600/patrick+kavako+baunsa.JPG
  Patrick  Kavako 'Baunsa'
http://3.bp.blogspot.com/-QJmfTYhcn1A/UaOhMJay30I/AAAAAAAADDo/1e6IW1v2Hwg/s1600/king+class+mawe.JPG 
Bondia, KING CLASS MAWE

  Na Mwandishi Wetu
Bondia  Patrick Anthony Kavako 'Baunsa' wa Morogoro  ametamba kumsambalatisha Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao wa raundi nane utakaofanyika siku ya jumapili june 16 katika ukumbi wa panandi panandi uliopo Ilala Bungoni Dar es salaam
Akizungumzia mchezo huo Kocha wa Kimataifa ambaye ni mratibu  wa mpambano huo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa mpambano huo ni wa kukata na shoka ambao si wa kukosa kwani kila mmoja amejitahalisha kivyake hivyo wasubili tu siku ya mpambano huo
Unajua morogoro na Dar es salaam ni mahasimu katika michezo yote ukiangalia na sasa wamekutanishwa vijana katika masumbwi hivyo kila mmoja anaitaji ushindi ili ajiongezee rekodi yake kwani 'King Class Mawe' ato kubali kupigwa na Kavako ato kubali kabisa kupoteza mpambano wake kiraisi kwani na yeye anaitaji ajulikane katika ulimwengu wa masumbwi na kuiperekea sifa morogoro kama ilivyo kwa mabondia wengine wanao tamba mkoani hapo 
Mpambano huo ulioratibiwa na Kinyogoli Fondition kwa kushlikiana na PST itakuwa chachu kwa vijana kuendelea kuupenda na kuucheza mchezo huo unaopendwa na wengi nchini
mbali ya mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka bondia Abuu Mtambwe ataoneshana umwamba na Kassim Gamboo na Bondia mkongwe kabisa Yohana Robart atamenyana na Mussa Sunga

No comments:

Post a Comment