Saturday, October 10, 2015

Aunt Ezekiel: Stukeni, hakuna mabadiliko bila kufanya kazi


 Na mwandishi Wetu
Watanzania hasa vijana wameshauriwa kuyafikiria kwa umakini mabadiliko wanayoyataka kabla ya kuchukua maamuzi wanaytaka kuchukua, hali itakayopelekea kuwa na umakini watakapofikia siku ya kupiga kura, siku ambayo wanapaswa kufanya maamuzi yaliyp sahihi.

Hayo yamesemwa na msanii wa filamu Aunt Ezekiel ambaye yupo katika kundi la kampeni la Nimestuka linalomuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dk John Pombe Magufuli, ambalo linafanya ziara za kijiji kwa kijiji kuwahamasisha vijana kukipigia kura Chama cha Mapinduzi ili kirudi madarakani kuendelea na utekelezwaji wa ilani yake ya uchaguzi.

Aunt amewaambia wakazi wa Malunga, Shinyanga, wasidanganywe na bei za bidhaa kwamba zimepanda sana ukilinganisha na miaka kumi iliyopita. Hizi bei pia zisingeweza kuwa zile zile kwa miaka kumi, hata wao wangekuwa wafanyabiashara wangepandisha tu.

"Mabadiliko bila na wewe kama kijana kujishughulisha hayawezi kuja, itakuwa ni miujiza, na hii ndio sababu yangu ya msingi nikaamua kurudi kwenye chama cha Mapinduzi ambako mgombea wake anasisitiza vijana kufanya kazi", alifafanua Aunt Ezekiel.

Aunt ambaye alikuwa ni mmojawapo kati ya wasanii wanaoliunga mkono kundi la vyama vya siasa la UKAWA, ame3waambia vijana wa Malunda kwamba vyama vya upinzani, bado havijawa tayari kutawala kwa kuwa linatumia vibaya nguvukazi ya vijana.

"Kule tunafundishwa kulalamika tu, kupinga serikali, hatuambiwi tufanye nini maisha yetu yawe bora, hatuambiwi kuhusiana na kuanzishiwa miradi, hii sio busara hata kidogo
 StanBakora, mmoja kati ya wasanii walio katika ziara ya Kijiji kwa Kijiji ya Nimes'tuka, akiongea mbele ya hadhara Shiyanga mjini
 Mboto naye akimwaga Pipi kwa wakazi wa Malunga
 Miss Tanzania Lilian Kamanzima, naye pia alitoa ujumbe wake 
 Umati wa wananchi wa Shinyanga mjini waliojitokeza katika mkutano wa kundi la Nimestuka uliofanyika katika kata ya Malunga

 Kitale akiingia uwanjani kwa ajili ya kuongea na wananchi wa Malunga...
Inspekta Haroun, ..Babu

No comments:

Post a Comment