Wednesday, April 23, 2014

JACKLIN WOLPER, LULU WAKIRI KULA URODA NA ALIKIBA

Ali kiba ni mmoja wa wanamuziki walio kimya sana kwenye upande wa kuongelea mambo yake binafsi, haswa kimahusiano, au hata kujitangaza kumiliki kitu kingine chochote cha thamani kama ilivyo desturi ya wasanii wengi hapa town baada tu ya kupata umaarufu, ila siri hufichuka haswa pale kwa warembo hawa wanapoamua kumwaga mpunga ndipo hapo unapoanza kujua yaliyo chini ya kapeti.Hawa ni warembo waliowahi kukiri kuwa walishawahi kuwa na mahusiano na Celeb huyu mkongwe sana kwenye anga za muziki huu wa Bongo Fleva.
 
Lulu na Kiba.
Haikujulikana mapema kama inavyotokea kwa watu maarufu wengi hapa town, ila mahusiano yao yalianza huko kitabo sana, baina ya Lulu na Ali Kiba, ila mwisho wa siku Lulu aliamua kumwaga mpunga hadharani kufunguka juu ya mahusiano yao.
“Duh! Umenikumbusha mbali sana. Nilishasahau kabisa kama niliwahi kutoka naye. Pamoja na kwamba ni kweli alikuwa mtu wangu, lakini kwa sasa moyo wangu hautaki kusikia kingine zaidi ya Bieber na namuonea wivu sana Selena Gomez (mpenzi wa Bieber).”
ila hakutaka kuzungumzia sababu za kuachana naye, nakusea ilikuwa tu sababu zake binafsi kwa sababu mapenzi yana taba moja kuwa ukiyag’ngania hasa pale ambapo hauenjoy mwisho wake ni kuumizana tu, alimalizia lulu kuelezea safari yake ya mapenzi, na hadi hivi sasa anakiri kuwa bado yupo yupo sana.
  
Wolper na Kiba.
Mapenzi ya hawa wawili inasemekana yalianza enzi hizo ambapo wawili hao walikuwa bado hawana majina kabisa hapa town, kila mmoja wao akiwa yupo kwenye hustle zakutoka kila mmoja akiwa natetea fani yake, ila kwa bahati nzuri AliKiba akaanza kupata umaarufu kuitia muziki hata kabla ya Wolper kuanza ku-make headlines kupitia filamu, akiwa kama muigizaji.
“Ni kitambo kidogo sana wote hatukuwa star lakini mwenzangu alifanikiwa kuchomoka,lakini Ali ndiye aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa Mapenzi” alifunguka Wolper,
“Ali akawa star,alipokwenda nje nikasikia wanawake wanamshobokea,sasa mimi sikutaka karaha nikakaa pembeni,lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana tuanasalimiana freshi kabisa” alimalizia akizungumzia sababu zilizomfanya aachane na Kiba wakati huo.

No comments:

Post a Comment