Thursday, April 24, 2014

BANZA STONE, CHOKI KUUNGURUMA NDANI YA RUFIT KESHO (IJUMAA 25/04/14)

Wakali wa muziki wa dansi bongo, mtu mzima Ally Choki na Banza Stone kwa pamoja watadondosha bonge la Shoo pande za Tabata katika ukumbi wa Rufita Executive ikiwa na shoo iliyondaliwa maalumu na Kampuni ya BS ENTERTAINMENT .
Akizungumza na mwandihi wetu Banza Alisema kuwa wamejipanga vya kutosha kuwapa raha na burudani ya kutosha mashabiki wao wote na wakazi wa maeneo ya tabata Segerea siku ya Ijumaa ya tarehe 25 mwezi wa nne.
"kiukweli mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi maana tumeamua kuwapa burudani ya kutosha nikiwa na bendi nzima ya Extra Bongo na mtu mzima Ali Choki"
kwa kuongezea Banza alisema kuwa amewaandalia mashabiki wake vitu vizuri ambavyo hawajawahi kuvipata kwani watawaimbia nyimbo ambazo ni mpya zikiwamo zile walizoimba na marehemu mzee Gurumo. "Kuna nyimbo nyingi tutaanza kuziimba pale ikiwa ni pamoja na zile tulizoimba na mzee wetu marehemu Muhidini Gurumo ikiwa ni 'Surprise' kwa mashabiki wetu wa maeneo ya Tabata Segerea"
Banza alimalizi kwa kushukuru uongozi wa Kampuni ya BS ENTERTAINMENT kwa kuwaandalia shoo hiyo itakayotoa burudani ya kufa mtu huku akitaja kiingilio katika shoo hiyo ni Sh. 5000/= tu malngoni.

No comments:

Post a Comment