b..

B1

Wynem

animation

Friday, November 22, 2013

MOJA YA KAZI ZA KUTOKA SULE'S INC. & ENTERTTINMENT (SHOOTING KATIKA SEND-OFF PARTY YA DADA JULIETH MASAWE)

Sule Junior (kulia) na Alex Nyaganilwa wakiwa kwenye kamera kuhakikisha wanadaka kila tukio.
Julieth (kushoto) akiingia ukumbini sambamba na mpambe wake.
Kitu cha ndafu kama kawa
Julieth akikata keki
Kamati ya maandalizi ya sherehe ikinyanyua keki juu ishara ya umoja
Julieth Masawe akiwa na mumewe wakati wa Send-off
Watu wakiserebuka makwaito katika kufurahia sherehe.

SULE'S INC. & ENTERTTINMENT wanafanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na video production za matukio mbalimbali kama harusi, send-off, kichen party, mahafali na sherhe za aina zote.
WAPO KAWE MZIMUNI KARIBU NA KITUO CHA KANISANI 
Wasiliana nao kwa +255 719 694086 / +255 767 007515 /+255 715 379691

Wednesday, November 13, 2013

COUNTRY BOY NDANI YA AMBASADORS LOUNGE

 
Country Boy Ndani Ya Ambassadors Lounge Ijumaa Hii Tarehe 15.11.2013 Ni Birthday Party Yake Na Pia Anatambulisha Audio Na Video Ya Wimbo Wake "Watch Me" Feat Gnako,Host Wa Show Ni Kajala,Guest Performances By Mirror,Babuu Wa Kitaa,Chibwa,Tash Na Surprises Nyingine Zitakuwepo,Dj Steve B/Dj Skills,Dvj Ally B Na Dj Masu On The Set,Entru 10,000 shs kuanzia Saa 3 Usiku

Friday, October 25, 2013

Thursday, October 24, 2013

KICHUPA CHA MWANAMBUZI KIPO TAYARI, MDAU KAA MKAO WA KUKITAZAMA SIKU YEYOTE KUANZIA LEO

Video hii ya wimbo wa Mwanambuzi ulioimbwa na msanii Wynem, imefanyika katika production ya Sule's Inc. Chini ya Director, Sule Junior (Salum Suleiman)

Thursday, October 17, 2013

BONDIA, CHUGA BOY ALIVYO MSAMBALATISHA ISMAIL KAJIMA


Bondia Amani Bariki 'Chuga Boy' kushoto akipambana ya Ismail Kajima wakati wa mpambano wao uliofanyika Mbezi kwa Msuguli katika ukumbi wa Samunge Dar es salaam siku ya kusherehekea sikukuu ya Idi Chuga boy alishinda kwa pointi.

Bondia Amani Bariki 'Chuga Boy' akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ismail Kajima wakati wa mchezo wao uliofanyika mbezi kwa msuguli ukumbi wa Samunge Dar es salaam wakati wa kusherehekea sikukuu ya Idi Chuga Boy alishinda kwa point mchezo huo.

Chuga Boy akitangazwa mshindi wakati wa mpambano huo
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Wednesday, October 2, 2013

MPAMBANO WA MASUMBWI KUFANYIKA PANANDI PANANDI ILALA OKTOBA 26


Kocha wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' (kushoto) akiwaelezea jambo masahabiki wa mchezo wa ngumi kuhusu DVD zinazoonyesha mafunzo mbalimbali ya Mchezo huo.

Na Mwandish Wetu

MPAMBANO mwingine wa masumbwi kufanyika katika ukumbi wa panandi panandi Oktoba26 mpambano huo wa mchezo wa masumbwi utakaokuwa chini ya uratibu wa Kinyogoli Fondition utawakutanisha mabondia mbalimbali wenye majina na wanaotamba kwa sasa katika anga za masumbwi nchini.
Akizungumzia mchezo huo kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini kutoka kambi ya ilala Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mpambano huo utawakutanisha bondia Yakubu Maganga atakae zichapa na Ubwa Salumu katika uzito wa kilo 75 huku Seif Ali akipambana na Hassani Labanda pamoja na mipambano mengine ya masumbwi itakayo wakutanisha mabondia mbalimbali Siku hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama.Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye ame haidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakao onesha uwezo wa ali ya juu wa kutupiana masumbwi

Monday, September 30, 2013

J DEAL FT G'NAKO - NIIMBIE (Official Audio Release)

Download "Niimbie" wimbo toka kwa mkali ya R&B, J Deal au ukipenda "Jacob Deal" akiwa na Gnako the A City Kankara aka WaraWara. Wimbo ni category ya R&B toka studio za Noizmekah Arusha chini ya Producer Defxtro, kuusikiliza bofya HAPA na kwa mawasiliano zaidi check na J Deal kupitia +255 718 515 772

JIMMY MASTER FT KISUKE & SPAC DAWG - BADO NASO

Download "Bado Nahaso" wimbo wa JimmyMaster akiwa amemshirikisha Kisuke Matoke & SpacDawg mzigo toka studio za Noizmekah Arusha bofya HAPA kuisikiliza ngoma na kwa mawasiliano zaidi check na Jimmy Master aka Mnyampaa kwa nambari +255 655 499 318 powered by www.vmgafrica.com

BREAKING NEWS!!!!! MSANII NA MEMBA WA KUNDI LA WATEULE, MACK MALIK a.k.a SIMBA AFARIKI ASUBUHI HII

Msanii Na Producer Wa Music Wa Bongo Fleva Na Reggae Mack Malik Simba Amefariki Dunia Dakika 50 Zilizo Pita. Kaka Wa Marehemu Msafiri Masharubu Amesema Kuwa Alikuwa Akisumbuliwa Na Kuvimba Kwa Miguu Sana. Amefia Nyumbani Kwao Yombo. 
Mack Alikuwa Member wa Kundi la wateule na producer kwenye studio za Enrico Pale Sound Crafters. Tunazidi Kufuatilia Habari Zaidi

LORD EYEZ - ROHO ZINAWAUMA (Official Release)

Download Lord Eyes aka Lord Izzy Official full Song "Roho Zinawauma" HERE http://goo.gl/t9kDcB ikiwa ni Mkono toka Noizmekah Production Studios chini ya Producer Dx aka Defxtro, powered by www.vmgafrica.com

Thursday, September 26, 2013

JCB ft PROF JAY -DRIVE SLOW (MJ Recs) KIONJO SNIPPET

Pata kusikiliza kionjo cha JCB ft Professor Jay, wimbo unaitwa "Drive Slow" ikiwa ni kazi toka Mj Records chini ya MarcoChali, Download HAPA

Wednesday, September 25, 2013

1ST ANNIVERSARY OF THE LEGEND IS BACK

Sasa zimebaki siku 3 tu kabla ya kufika siku tunayoisubiri kwa hamu, The Legend is Back first anniversary. Project ilianza kwa support yenu na ni mwaka sasa tunatimiza kwa sapport yenu. Tulianza pamoja karibu tujumuike tutimize mwaka tukiwa pamoja. Siku hii muhimu itaambatana na shindano kali la disco dancing toka kwa mabingwa wa zamani kuiwakilisha Morogoro Maneno Ngedere na toka DSM Athuman Diga Diga. Vile vile wakali wa chacha Africa Mashariki Moddy Jazz B na Sunday Boy watachuana vikali. Utakuwa vilevile na special moment of silence kuwakumbuka malegendari wa disco waliotutangulia mbele ya haki ni j'mosi hii 28/9/2013 ndani ya isumba lounge. Wote mnakaribishwa


Tuesday, September 24, 2013

MSICHANA WA KIZUNGU ANAYEDAIWA KUONGOZA MAUAJI WESTGATE ADAIWA KUUWAWA KWENYE MASHAMBULIZI



Wakati mapambano bado yanaendelea dhidi ya wanamgambo wachache wa al Shabaab waliobaki ndani ya Westgate Mall, maofisa wa Kenya wamesema angalau al Shabaab watatu wameuawa katika harakati za kuokoa mateka
Taarifa zinasema mmoja wa magaidi hao ni mwanamke wa kizungu. Inaaminika kuwa mwanamke huyo aliyetajwa ni Samantha Lewthwaite, al-maarufu kama “White Widow” au “Mjane Mweupe” au “Mjane wa Kizungu” kwa Kiswahili. Samantha anaripotiwa kuwa ndiye kiongozi wa kundi hilo lililofanya mashambulizi.
Inasemekana kwamba kati ya magaidi waliouawa, mmoja wao ni mwanamke wa kizungu lakini bado haijajulikana kama ni Samantha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, mume wa Samantha alikua mpiga mabomu wa kujitoa mhanga (suicide bomber) anayeitwa Germaine Lindsay ambaye baada ya kusilimu alitumia jina la Abdullah Shaheed Jamal.
Abdullah Jamal alikua ni mmoja wa magaidi wenye asili ya Uingereza waliopiga mabomu ya kujitoa mhanga katika treni tatu na kuua watu 56 nchini uingereza Julai 7, 2005 ambao unajulikana duniani kama “Ugaidi wa 7/7