Tuesday, October 19, 2010
UDHAMINI WA GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL WAFIKIA 35ML.
Udhamini wa hoteli ya giraffe katika shindano la Girafee unique model 2010 umefikia milioni 35 za kitanzania ambapo baadhi ya mambo mengine na wadhamini kadhaa wakijitokeza kudhamini shindano hilo la mitindo ambalo linategemewa kua la aina yake kwa kufungia mwaka kimitindo
Girrafe unique model ni shindano la kumtafuta mwanamitindo wa kike mwenye sifa za tofauti ikiwa na lengo kuu la kuleta mapinduzi ya mitindo nchini tanzania
Pia mbunifu wa mavazi nchini Tanzania ali lemtulah amejitokeza kama mdhamini wa mavazi na mtu atayemchukua model mmoja kama balozi wa nembo ya nguo zake zinazotegemewa kuzinduliwa mwanzoni mwa mwaka ambae atafanya kazi na mwanamitindo huyo kwa mwaka mzima ....ni kitu kikubwa sana watanzania.
Monday, October 18, 2010
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KWENYE SHOO YA USIKU WA JAHAZI JANA ULIOANDALIWA NA QSSP GROUP LMITED.
Mtangazaji wa C2C Mwane akitangaza mawili matau.
Hapa ni Omari Mkali akifanya vitu vyake
Hii ndio shoo nzima ya Jahazi iliyoandaliwa na QSSP GROUP na hili ndio nyomi yote iliyokuwa ukumbini
Ilifikia hatua ya kujiachia na kamera ya MTOTO WA KITAA na mambo yalikuwa hiviii
Na hii ndio picha ya mwisho kupiga, ikiwa ni mimi (mtoto wa kitaa) nikiwa katikati huku kushoto akiwa ni Boy Sella na kulia ni Criss. hapo ndio tulikuwa tunatoka hivyo.
Sunday, October 17, 2010
KAMA KAWA KAMA DAWA GAZEI LAKO LA DIRA YA MTANZANIA LIPO TENA MITAANI USIKOSE NAKALA YAKO SASA.
Hivi ndivyo gazeti linavyo onekana na linatoka kila JUMA TATU na hutolewa na DIRAMEDIA GROUP. Pata nakala yako kwa shilingi mia nne tu. Linapatikana nchi nzima.
HII NDIO HISTORIA YA WATENGWA.
Hawa ndio Watengwa wa A-town wanaotingisha nchi kwa Hip hop
WATENGWA ni kundi ama genge la vijana linaloshughulika na muziki wa Hip Hop maarufu zaidi kama ’gangstar rap’ lenye makazi yake jijini Arusha maeneo ya Kijenge.
Kundi hili lilianzishwa miaka 10 iliyopita likiwa na maskani yake kijenge juu, chini ya mtu mzima JCB na Chindo man... kabla ya wao kuanzisha kikundi kwa pamoja waliweza kuanzisha studio yao wenyewe waliyoipa jina la Watengwa Records.
Muvumenti yao hiyo ilileta msisimko mkubwa kila kona ya Jiji la Arusha kwani baada ya watu kusikia kuna studio hiyo ya Hip Hop pale kijenge ya juu basi wasanii wengi wachanga waliweza kufanya ngoma kibao tu.
Kutokana na kuwa na studio yao wenyewe, ndipo mwanamuziki JCB na Chindo waliamua kukaa chini na kutengeneza albamu yao ya kwanza waliyoipa jina la Iliandikwa ambayo albamu hiyo iliweza kuwatangaza vyema Watengwa kama kundi pamoja na studio kwa ujumla. Album hiyo ilibeba nyimbo kama Nawaza, Sina hata taxi, nimefurahishwa na nyingine.
Watengwa iliendeleza harakati zake kwa kuanza kuwatoa wasanii chipukizi (underground) na kuwafanya wajulikanike mitaani kama Donii, Gheto Queen ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani katika Jimbo la Califonia... wengine ni D-Wida, Chaba, Boomblast na pia kuna makundi kutoka Moo town (Moshi) yaliweza kufyatua ngoma kibao tu katika studio za Watengwa, makundi hayo ni kama vile Last Society, West Pasu na Mistari team kutoka Pasua Moshi.
Hii ni safari ndefu sana ya Hip Hop kwani kama inavyojulikana album ya kwanza huwa haiachii mikwanja ya kutosha, lakini Watengwa hawakukata tamaa na baddala yake walijipanga na kuweza kuachia ngoma nyingi tu zilizowafanya wajulikane kona zote za Arusha mpaka kufanya hata kwa mtu yeyote anayefika Arusha na kuiulizia Hip Hop basi ni lazima ataambiwa aende kijenge ya juu kwa watengwa.
Mwaka 2005 Watengwa ilipata nguvu zaidi kwa kuongeza memba mpya anayejulikana kama Yuzzo Rubama {ambaye kwa sasa anafanya shughuli zake za kimziki nchini Uholanzi}. Mwaka huo huo (2005) WATENGWA walitoa albam yao ya pili iliyoitwa Full ile Laana ambayo iliwakilisha vizuri sana na kuweza kuiweka juu Arusha kwenye hiphop.
Albam hiyo ya Full ile Laana iliongelea zaidi shida za watu wa mtaa, hasira za vijana na maisha kwa ujumla. Pia walitoa video moja kwenye albam hiyo ambayo ilikua ni Sio lazima ambayo ilichezwa vya kutosha kwenye vituo vya televisheni nyingi za Afrika mashariki. Pia albam hiyo ina vibao kama Nyani, Ukisia Paah {original version}, hatujaja kujaribu na na nyingine kibao tu ambazo nazo zilifanya vizuri sana.
Mwaka uliofata (2006) watengwa ilijijumuisha na wasanii kutoka Kenya, Rwanda na Burundi na kutoa cd ya pamoja ilioitwa East African Up vol.1. Kupitia harakati hizi watengwa ilitambulisha vipaji vingine vipya kama Mapacha, Finger Lou n.k.
Mwishoni mwa mwaka 2007, Watengwa JCB na Chingo walitambulisha albam yao ya tatu waliyoipa jina la Pigo takatifu iliyofanya vizuri katika anga ya muziki wa Tanzania na ilikuwa na vibao kama Tabia mbaya, Wanashangaa, sipotezi muda na ngoma nyingine kibao tu za ukweli ambazo ziliweza kuifanya Watengwa kua nguzo ya Hip Hop Tanzania.
WATENGWA Wakaendeleza harakati hizi kwa kufanya matamasha mbali mbali huku wakipromoti studio na wasanii wao pia. Baada ya muda Chindo na Yuzzo walienda nje ya nchi kutafuta maisha na kuutangaza mziki wao kimataifa zaidi, huku nyuma JCB na Watengwa wengine waliendeleza harakati hapa nchini.
Ndipo JCB alipoamua kutoa albam yake kama solo artist iliyoitwa Nakala za Makalia chini ya produza Daz Maledge ndani ya studio za Watengwa ambapo mpaka sasa albam hiyo ndiyo inayoitambulisha vizuri watengwa na JCB kwa ujumla.
Wakiwa wanakaribia kufikia malengo yao Watengwa wameshusha vifaa vya studio vipya kabisa na vya kisasa zaidi huku wakiwa na waandaaji watatu wa muziki, Simon Fees, D-Wida na Daz Naledge.
Chindo na Yuzzo watarajiwa kurudi Tanzania (Arusha) kwa ajili ya kuzindua upya studio ya Watengwa pia watatumia muda huu kutengeneza albam yao nyingine itakayoitwa Full ile Laana vol.2 ambayo itakua ya kimapinduzi zaidi.
Kwa mtazamo wa JCB amesema albam hiyo itakua ya kiutu uzima zaidi kutokana na ukongwe wao kwenye hii harakati hivyo mashabiki wakae mkao wa kula. Watengwa wanapatikana kwenye www.myspace.com/watengwa pia wako kwenye page ya facebook kama WATENGWA.
Saturday, October 16, 2010
CHINDO MAN a.k.a UMBWA IS BACK AGAIN.
Mafansi wa hip hop sasa kaeni mkao wa kula kwani Mwana HIP HOP Chindo man a.k.a umbwa atatua tena kwenye ardhi ya tanzania tarehe 22 octoba,2010.Umba ahji mikono imtu, mwana anakuja na albam na anaiita 'Punda'kwahiyo kaeni mkao.
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ATEMBELEA HOSPITALI ZA MUHIMBILI NA OCEAN ROAD (TAASISI ZA SARATANI.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimtazama Winter Isaac (3) ambaye ni mmoja wa watoto waliolazwa kwenye Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es salaam wakati alipotembelea Taasisi hiyo Jana Oktoba 15, 2010. Friday, October 15, 2010
HALIMA MDEE BADO ANAITINGISHA KAWE.
Hapa akisikilizia kabla ya kupanda jukwaani kumwaga sera.
Hapa akiwa jukwaani akimwaga sera zake.
Na hili ndio nyomi lililokuja kumsikiliza Mgombea HALIMA MDEE
Subscribe to:
Posts (Atom)






sa








































