Friday, December 19, 2014

STEPS KUTAMBULISHA FILAMU KATIKA MUONEKANO MPYA KWA MWAKA 2015

Mratibu wa mpango mpya wa Steps Entertainment, myovela Mfwaisa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mtayarishaji na mwongozaji wa Filamu nchini, Jackob Steven 'JB' akizungumzia ujio mpya wa Steps.
Wakionesha Makasha mapya ya muvi za kibongo zitakazoanza kusambazwa na Steps mwaka 2015

Na Mwandishi wetu
Kampuni ya usambazaji wa filamu bora Tanzania ya Steps Entertainment Ltd inatarajia kutoa bidhaa mpya za filamu kwa mwaka ujao wa 2015 filamu zenye ubora muonekano mzuri huku pia kuwaletea walaji bei rafiki kutoka kampuni bor a ya usambazaji wa filamu Tanzania Steps Entertainment Ltd.
Steps Entertaiment Ltd ni ilioanzishwa mwaka 2007 nchini Tanzania na makao yake makuu yako jijini Dar salaam, Kampuni ya Steps Entertainment inajishughulisha na usambazaji wa filamu za Kitanzania maarufu kwa jina la  BONGO MOVIES
Tangu kuanzishwa kwake Kampuni ya Steps Entertainment imekuwa mdau mkubwa katika kukuza tasnia ya filamu nchini Tanzania na mpaka sasa ndiyo kampuni kubwa ya usambazaji wa filamu nchini Tanzania. 
Kampuni ya Steps Entertainment kupitia mikakati yake ya kuinua tasnia ya filamu nchini Tanzaania imefanikiwa kutoa ajira nyingi kwa wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu, wakiwemo waandaaji wa filamu, Waigizaji, Wasambazaji wakubwa kwa wadogo, Wauzaji wa rejareja na wanaoonyesha na au kukodisha katika vibanda. 
Akiongea na wanahabari Carlos Johns Silondwa mtendaji mkuu ameielezea Steps Entertainment imefanikiwa pia kuvuka mipaka na kufikisha sinema za kitanzania katika mataifa mbalimbali ya nje na katika luninga za kimataifa na televisheni za ndani kuonyesha kazi za nyumbani.
“Kwa sasa mataifa mengi Ulaya na nchi za Scandinavia wanajifunza Lugha yetu ya Kiswahili kupitia filamu zetu, moja kwa moja utaona njia nyingine katika kukuza Kiswahili nje ya nchi kwa njia ya filamu tu ambazo zinasambazwa na kampuni hii, na kutengeneza ajira kwa vijana wengi,”
Pia kampuni imekuja na bei rafiki kwa mlaji baada ya kilio chake kuumiza kwa muda mrefu, kampuni kwa kutumia wataalamu pamoja na wadau wa filamu kutoka sehemu mbalimbali wamefanya utafiti ili kupata Mwarobaini wa Maharamia wa kazi za nyumbani kampuni imeshusha bei.
Hiyo inatokana na hali halisi filamu inatakiwa imfikie mtumia kwa 6,000/ lakini utafiti umebaini kuwa mtanzania anatumia zaidi kiasi cha 34,000/ na zaidi bila kuimiliki Dvd hiyo, baada ya Vibanda au Library kuanzimisha, badala ya kumuuzia. 
Filamu ambayo itauzwa ikiwa katika ubora na muonekano mzuri, inakuja baada ya filamu kutoka nje, kuuzwa kwa bei ya chini kabisa na kuleta ushindani pamoja na kuwa sinema hizo hazilipiwi kodi tofauti sana, nakuzifanya zinunulike sana kuliko filamu za ndani kutokana na bei yake kuwa ndogo.
 Kampuni ya Steps Entertainment ilifanya utafiti ili kujua ni jinsi gani filamu zinatoka mbali na bado zinawafikia walaji kwa bei ya chini ni baada ya utafiti huo ndipo Kampuni ya Steps Entertainment iliamua kujibana na kufanikiwa kuingiza na kufunga mtambo mkubwa wakisasa kuzalisha cd/dvd, kuzirekodi na kuziprinti hapa hapa nchini.
Tofauti  na siku za nyuma ambapo ilikuwa inaagiza cd/dvd kutoka nje ya nchi na kuja kuzirekodi tu, sambamba na mtambo huo pia kampuni hii imeamua kubuni kifungashio kipya yaani kasha za cd/dvd, ambayo ni za bei nafuu, zinamuonekano mzuri zaidi, ni rahisi kuhifadhi, nirahisi kusafiriha na nirafiki wa mazingira.
Mtambo mkubwa na wakisasa pamoja na kifungashio kipya vimepunguza sana gharama za kuzalishia nakala za dvd na cd na hivyo Steps imeona ni vyema kuonyesha moyo wa uzalendo kwa wateja wake  kwa kuwapunguzia bei ya kununua filamu kwa kuwauzia kwa nusu ya bei ya awali.
Kampuni ya Steps Entertainment inaamini kuwa kitendo cha kupunguza bei za filamu zake, kitawanyima Maharamia ulafi na wizi wa wazi kabisa, kama kampuni inakaribisha wadau wote wanaosambaza filamu kwa kuja kwetu kuzalishiwa filamu zao kwa bei rahisi sana ili huyu Gaidi mkubwa anayenyonya kazi zetu aache. 
  • Kinaonyesha moyo wa uzalendo lakini pia kitapandisha mauzo ya filamu za kitanzania ambapo kwa ujumla wake itaongeza kipato kwa wasanii na kuchangia pato la Taifa.
  • Kitapunguza uharamia wa filamu kwa kuwa bei itakuwa chini hivyo kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua nakala halisi.
  • Kitaziwezesha library zinazokodisha filamu kuacha kukodisha na badala yake kuanza kuuza moja kwa moja
 Hivyo basi Kampuni ya Steps Entertainment inamaliza mwaka 2014 na kuingia mwaka 2015 kwa kubororesha bidhaa zake, zikiwa katika ubora na muonekano wa kuvutia kwenye kasha la bahasha ngumu, bidhaa hizi zitamfikia mlaji kwa bei ya  1,500/= tu bei hii kwa filmu zitakazo kuwa katika kifungashio kipya pekee filamu zitakazo kuwa katika kifungashio cha zamani yaani kasha la plastiki zitaendelea kuuzwa kwa bei ile ile na wateja watakuwa huru kuchagua aina ya kifungashio pale wanaponunua nakala za filamu za Steps
Hivyo basi Steps Entertaiment imeanzisha kampeni maalum ya “Faidika na Steps kwa bidhaa bora, Wasanii nyota, na Filamu Bora”.
Kampuni ya Steps Entertainment  inawaomba wadau wote kuendelea kuzienzi filamu za kitanzania ili kukuza kipato cha wasanii na taifa kwa ujumla , kutangaza lugha ya Kiswahili na utamaduni wa kitazania.
Bei zetu zitakuwa wazi kwa maan za steps tofauti ya bei iliyoandikwa kwenye kasha ya kuonekana zikiwazimeandikwa katika kasha na mwananchi asikulaghai mtu wa Library eti usinunue hadi hakukodishe sema No.

Mwisho, Tunaiomba Serikali Chini ya Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wawasaidie wadau wa filamu kupambana na uharamia wa filamu ambao kwa sasa umevuka mipaka wezi wanafanikiwa wasanii wanabaki Maskini.
MUNGU IBARIKI TANZANIA Mungu bariki Afrika 
Carlos Johns Silondwa 
Mtendaji Mkuu.


No comments:

Post a Comment