Monday, May 26, 2014

WANAOJIITA WATOTO WA MBWA NA PANYA ROAD 149 WANASWA NA POLISI KWA MSAKO WANYUMBA HADI NYUMBA

Hawa ndio viongozi wa panya road na mbwa mwitu ambao tayari wameshakamatwa

Na Mwandishi Wetu
 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanya msako wa nyumba kwa nyumba, mtaa na maeneo yaliyoathirika kwa hofu ya vijana ambao ni vibaka maarufu kama Mbwa mwitu au Panya Road.  Msako huu uliofanyika ndani ya masaa 24 hadi alfajiri ya tarehe 26/5/2014 kwa lengo la kuwaondolea hofu na uhalifu dhidi ya makundi ya vijana wadogo wasio na ajira ambao uliibuka hivi karibuni.
        Maeneo yaliyoathirika ni Kigogo, Magomeni, Tabata, maeneo yote yanayozunguka mto Msimbazi, maeneo ya Mbagala nk.  Msako huu unaendelea kufanywa na askari wa vikosi maalum ambao wamepewa kazi ya kuhakikisha kuwa vikundi hivyo haviibuki tena na vinatokomezwaa kabisa kwa  kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kuvamia kwa mkundi wananchi ambao hawana hatia.

Kamishna kova ambaye amezungumza na wanahabari jana.

 Kati ya watuhumiwa 149 waliokamatwa mmoja amegundulika kuwa ni kiongozi aitwaye ATHUMANI SAIDI miaka 20, Mkazi wa Kigogo na amekiri anaongoza kundi la watu zaidi ya 15 ambao baadhi yao ni kati ya waliokamatwa. 
          Imegundulika pia kwamba vijana hawa wanatumia dawa za kulevya aina ya bangi na wengine hujichoma sindano na kuwafanya iwe rahisi kujihusisha na matukio ya uhalifu.  Vijana hao hupenda kushiriki katika ngoma kama Mnanda, Mchiriku, Kigodoro, Kanga moja nk. ambazo kwa kawaida huchezwa hadi usiku wa manane. 
         Wakitoka katika ngoma hizo hujikusanya pamoja na kufanya matukio ya uporaji kwa mtu wanayekutana naye, kufanya uvunjaji katika majumba na wakati mwingine wana mtindo wa kugema mafuta ya diesel au petrol katika matanki ya malori yanayosafirisha mafuta. 
         Operesheni kali inafanyika katika maficho ya wahalifu hao ikiwa ni pamoja na daraja la River side, Kigogo darajani, Manzese, maeneo ya Tandale pamoja na maeneo mengine ya maficho mkoa wa Kipolisi Temeke.
  Tunawasiliana na Maafisa utamaduni wa Wilaya zote za Mkoa wa D’Salaam kusimamisha utoaji wa vibali wa ngoma za usiku ambazo hazina tija.  Pia Jeshi la Polisi linafuatilia na kuwavizia vijana wanaopora  watu wanaotoka katika sherehe za usiku kama vile Harusi na wanaotoka katika mikesha ya Ibada na sehemu zozote zenye mikusanyiko.
      Aidha Jeshi la Polisi wanapambana na vijana wanaowavizia watu katika vituo vya mabasi pindi wanapotoka alfajiri kwenda katika shughuli zao za kila siku.
Zipo taarifa kwamba baadhi ya wazazi wasio waaminifu wamewasafirisha watoto wao wahalifu katika makundi haya kwenda mikoani ili kukwepa wasinaswe na msako huu mkali.  Hata hivyo Jeshi la Polisi lina mtandao wa kutosha kati yake na mikoa mingine na nchi jirani hivyo litawatafuta popote walipo na kuwakamata.
         Oparesheni hii ni endelevu na ya kudumu hadi kero hii ya vibaka itakavyokwisha kabisa. Baadhi ya majina waliokamatwa ni kama ifuatavyo:-
1.    DANIEL PETER @ MALUNDE, miaka 25, mkazi wa Yombo Kigunga
2.    MWISHEHE ADAM, miaka 35, mkazi wa Mtoni mashine ya maji
3.    MOHAMED SAID, miaka 32, mkazi wa Mtoni
4.    JAKAMA ALPHONCE, miaka 23, mkazi wa Mtoni Kilakala
5.    HAMADI MDUDU, miaka 25, mkazi wa Mbagala
6.    SALUM MUSA, miaka 25, mkazi wa Kiwalani
7.    ANTHONY DANIEL, miaka 20, mkazi wa Mashine ya maji
8.    FIDELIN ANTHONY, miaka 18, mkazi wa Kigogo
9.    HAMZA MAZUMA, miaka 19, mkazi wa Kigogo
10.           MGANGA ABEID, miaka 20, mkazi wa Kigogo
11.           SAID ABEID, miaka 19, mkazi wa Kigogo
12.           SALUM NYENJE, miaka 36, mkazi wa Chamazi
13.           DOMINICK PETER miaka 22, Mkazi wa Kigogo
14.           KULWA ABEID, miaka 20, mkazi wa Mabibo
15.           MUSA IBTRAHIM, Miaka 20, mkazi wa Magomeni
16.           HUSSEIN SHABAN, miaka 22, Mkazi wa Magomeni

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAA

No comments:

Post a Comment