Thursday, January 15, 2015

HASHIM KAMBI KUONGOZA NYOTA BONGO KATIKA FILAMU YA CPU
Na Mwandishi Wetu
MSANII mkongwe katika tasnia ya filamu Swahilihood Hashim Kambi 'Ramsey’ ni moja kati ya wasanii wakubwa Bongo ambaye atawaongoza wasanii nyota na wakongwe katika filamu kubwa ya CPU inayotarajiwa kuingizwa katika Dvd baada ya kuonyeshwa katika majumba ya sinema ndani na nje ya Bongo.
Filamu ya CPU ni kazi kubwa sana kutengenezwa na watayarishaji wa ndani na kushirikisha wasanii zaidi ya mia mbili ndio filamu kubwa yenye ubora wa kipekee awali ilionyeshwa katika ukumbi wa sinema Century Cinemax Mlimani City kwa siku kumi mfululizo na kuacha gumzo kwa wapenzi wa sinema.
Kwa mara ya kwanza itauzwa katika Dvd ili kwa wale wapenzi wa filamu walioshindwa kuingia katika majumba ya sinema ilipoonyeshwa waweze kushuhudia teknolojia ya juu kutumika Bongo na kuwavutia wengi mtaani kwetu ambako ndio soko la filamu za kibongo lipo.
CPU inawakutanisha wasanii nyota na wakongwe ka aKulwa Kikumba ‘Kulwa Kikumba ‘ Dude’, Richard Mshanga ‘Masinde’, Dotnata, na nyota wengine kibao ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya filamu wakiongozwa na Hashim Kambi ‘Ramsey’ msanii aliyejijengea mashabiki wengi.

No comments:

Post a Comment