Saturday, June 7, 2014

PIGO JINGINE KWA TASNIA YA FILAMU TANZANIA, MZEE SMALL AFARIKI DUNIA


Ni pigo jingine tena kwenye tasnia ya maigizo (filamu) hapa nchini kwani mwigizaji na mchekeshaji mkongwe, Saidi Ngamba maarufu kama Mzee Small amefariki usiku wa kuamkia leo majira ya saa nne usiku katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kifo chake kimethibitishwa na mwane, Mohamed na msiba utakuwepo nyumbani kwa marehemu Tabata, Jijini Dar es Salaam.
Timu nzima ya SULE'S INC. na Blog ya MTOTO WA KITAA tunatoa pole kwa familia, wasanii na taifa kwa jumla kwa kufikwa na msiba huu.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema pepooni aamin.
(INNA LILLHAI WA INNA ILAIHI RAAJIUN)

No comments:

Post a Comment