Thursday, February 27, 2014
Wednesday, February 26, 2014
Friday, February 14, 2014
JHIKOMAN AWASHA MOTO SAUTI ZA BUSARA 2014...
__festival_2014_photo_by_Peter_Bennett_IMG_7420.jpg)
 
Na Andrew Chale, Zanzibar.
MWANAMUZIKI
 nguli wa miondoko ya Afro rege, Jhikoman Manyika   jana usiku Februari 
13,  aliwasha moto  kwa kupiga shoo ya nguvu iliyodumu kwa lisaa limoja 
na kukonga nyoyo umati mkubwa uliojitokeza kwenye tamasha hilo la 11,la 
Sauti za Busara mwaka huu 2014. Jhikoman alipanda jukwaani majira ya saa
 tatu usiku  sambamba na bendi yake ya Afikabisa na kupiga vionjo 
mbalimbali vya nyimbo zake za sasa na za nyuma.
Jhikoman 
aliweza kuwasha moto huo kwa kupiga nyimbo zake zilizopo kwenye albamu 
yake ya Chikonda na nyingine hali iliyokonga wadau hao wa muziki 
wakiwemo wageni kutoka mataifa mbalimbali na watanzania waliojumukika 
kwenye tamasha hilo.
Hata 
hivyo, Jhikoman alisema baada ya shoo hiyo anatarajia kupiga shoo 
zingine kwenye nchi mbalimbali kwa kufanya ziara maalum ikiwemo mataifa 
ya Ulaya. Mbali na Jhikoman wasanii wengine ni pmoja na kundi la Seven 
Survivor wanopiga muziki wa mchiriku, huku kundi la Baladna taarabu wao 
walikonga nyoyo kwa muziki wa mwambao na taarabu asili. Wengine ni kundi
 la Pongwa kutoka visiwani Zanzibar,  Tritonik (Motius), na nyingine 
nyingi.
Awali 
tamasha hilo lilifunguliwa kwa paredi iliyokusanya wanamuziki mbalimbali
 kutoka mataifa yote na kwa kila mmoja kuonyesha muziki wake mitaani na 
kasha kumalizikia kwenye viunga vya Ngome Kongwe. Aidha
 tamasha hilo la siku nne, linatarajiwa kuwa na wanamuziki mbalimbali 
vikiwemo vikundi 32, vyenye jumla ya wasanii 200, ambao watapiga shoo 
kwenye jukwaa hilo la Kimataifa. Hadi sasa mji wa Zanzibr umebarikiwa 
kuwa na wageni mbalimbali wakiwemo waliofika maalum kwa ajili ya shoo na
 wale wanaokuja kupumzika kwenye kisiwa hiki cha marashi ya 
karafuu.Aidha, tayari idadi ya wageni imeongezeka  huku baadhi ya hoteli
 zikiwa zimefurika  na biashara za kitalii zikiwa zinanunuliwa kwa 
wingi.
Kwa 
upande wake, David Ojoy ambaye ni msaidizi wa masuala ya habari wa 
tamasha hilo, anasema kuwa  hali ya wageni imekuwa kubwa kufika kwenye 
tamasha hilo ikiwemo kupata habari mbali mbali zinazoptikana kwenye 
mtandao maalum wa tamasha hilo pamoja vyombo vya habari. "Tunavipongeza 
vyombo  vya habari kwa kutupa sapoti na tunaomba tuendelee hivyo hivyo 
ilikukuza muziki wetu wa kiafrika na kujenga tamaduni imara hapa afrika 
na tamasha hili liendelee kuwa la kimataifa zaidi" alisema Ojay.
Friday, February 7, 2014
Thursday, February 6, 2014
NGUMI ZA NELSON MANDELA OPEN CHAMPIONSHIP ZAFUNGULIWA KAWE
Bondia Rashidi Samvu kutoka Kigoma kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hafidhi Kassimu wa Ngome wakati wa mashindani ya wazi ya Nelson Mandela yaofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam
Bondia Part Kimweri kutoka Tanga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Saidi Jabir wa Ngome Dar, wakati wa mashindani ya wazi ya Nelson Mandela yaofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam Kimweri alishinda mpambano huo kwa pointi
Bondia Fabian Gaudence kushoto akipambana na Hussein Mnimbo wakati wa mashindani ya wazi ya Nelson Mandela yabayofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam Gaudence alishinda mpambano huo kwa pointi
Mgeni wa heshima katikati Diwani wa Kata ya Kawe Othumani Kipete akiwa na viongozi wa Shilikisho la mchezo wa ngumi za Ridhaa nchini kulia ni Rais wa shilikisho hilo Mutta Rwakatare makamu wa rais Lukelo Willilo na
Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis
mjumbe wa bft antony mwangonda akiwa na makamu wa rais Lukelo Willilo
picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya mchezo wa Ngumi yanayokwenda kwa jina la Nelsoni Mandela Open ChampionShip yameanza kutimua vumbi katika
Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam
akizungumzia mashindano hayo yalivyo na ubora wa ali ya juu Makamu wa Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa nchini 'BFT' Lukelo Willilo 'amesema mashindano hayo kwa sasa yameboleshwa kwa kufuata taratibu za chama cha ngumi za ridhaa Dunia kwa sasa mabondia awavai kofia ngumu wanakuwa vichwa wazi hivyo wapenzi wa ngumi weje waone mabadiliko makubwa katika ngumi za ridhaa ndio ambazo ni msingi wa maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini;'
zamani mabondia walikuwa wanavaa kofia lakini kutokana na mabadiliko sasa awavai kofia wanapigana vichwa wazi ambapo kwa kuanzia tumeamua kuweka mashindano haya kwenye viwanja vya wazi na ni bule tu akuna kingilio ili kila mtu ajionee mabadiliko ya ngumi mashindano hayo yanayo husisha mikoa mbalimbali nchini
mashindano haya yatakuwa ya siku tano kuanzia jumatano mpaka jumapili na ngumi zinanza kupigwa saa kumi na moja mpaka saa mbili usiku ngumi ndio zitakuwa zikisha
Katika ufunguzi huo bondia Patrck Kimweri wa Tanga alishindwa kufurukuta mbele ya Said Jabir wa ngome na Rashidi Samvu wa Kigoma alipigwa kwa pointi na Hafidhi Kassimu wakati Fabian Gaudence akimsambalatisha Hussein Mnimbo
Sunday, February 2, 2014
"AUDIO" Vatoloco Gangz - Deadliest Men
Vatoloco Gangz wakiwa katika mchakato wa kumalizia mixtape wanadrop ngoma ya "Deadliest Men" ikiwa ni HipHop style ya Grime iliyo maarufu zaidi Uingereza, kusikiliza/Kudownload click HAPA 
Subscribe to:
Comments (Atom)


.jpg)
