KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila
'Super D' amepata mwaliko wa kwenda kufundisha pamoja na kuwapati ujuzi aliokuwa nao katika mchezo wa masumbwi mwaliko huo alioupata kutoka mkoa wa Ifakala mjini Kilombero kutoka kwa klabu ya Kilombero Boxing Klabu ambaye mwenyekiti wake ni Hiyari Bohari na katibu wa Klabu Hiyo ni Ramadhani Mindu wamempatia mwaliko wa siku mbili
Kocha huyo kwa ajili ya kuwanoa Makocha na kuwapatia ujuzi wa ziada mabondia chipukizi mwaliko huo unaomtaka kwenda kutoa ujuzi wa mchezo wa masumbwi kwa kushirikiana na kocha kutoka mkoa wa Morogoro Boma Kirangi mafunzo hayo yanayotakiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agost yanaonekana kuwa na umuhimu kwa kuwa vijana wengi wamejitokeza kuwa na mwamko wa mchezo wa masumbwi nchini
Hata hivyo Super D 'alisema kuwa amepokea mwaliko kwa furaha na yupo tayali kutoa ujuzi wake alioupata wakati wa mafunzo ya kimataifa kwa vijana watakaojitokeza' Super D aliongeza kwa kusema mchezo wa maumbwi nchini unapendwa na wengi ila unakosa wafadhili kwa ajili ya kutoa sapoti mbali mbali Super D ametoa wito kwa makampuni mbalimbali pamoja na wadau wa michezo kujitokeza kusaidia kwa namna moja au nyingine hususani mafunzo anayotaka kuyatoa akiwa mkoa wa Kilombero
Ambapo vijana wengi wanapenda kufahamu zaidi mchezo huo kwani kuna vijana zaidi walioamasika kucheza mchezo huo kwa kuwa na nia moja ya kuhakikisha mchezo wa masumbwi unawafikisha mbali ya kuwa ni mchezo pia utawapatia ajira
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Super D, alisema tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana
mbalimbali
No comments:
Post a Comment