b..

B1

Wynem

animation

Thursday, June 7, 2012

MISS KIGAMBONI KUPELEKA MAPATO SHULE YA MSINGI KIGAMBONI

Mwandishi Wetu
SEHEMU ya mapato yatakayopatikana katika shindano la urembo la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu yataenda kusaidia ukarabati wa madarasa yaliyopo kwenye Shule ya Msingi Kigamboni iliyopo jijini Dar es Salaam imeelezwa.
Shindano la urembo la kitongoji cha Kigamboni linatarajiwa kufanyika Juni 15 kwenye Ukumbi wa Navy Beach kuanzia saa 1:00 usiku.
Akizungumza jana, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa wameamua kutoa sehemu ya fedha zitakazopatikana kwa lengo la kuipa heshima ya shule hiyo ambayo ni moja ya sehemu zilizotoa washiriki wa kinyang'anyiro hicho na wajumbe wa kamati ya maandalizi.
Alisema kuwa wanawaomba wakazi wa Kigamboni na wengine kutoka sehemu mbalimbali jijini kujitokeza kushuhudia warembo wao ambao hapo baadaye wataenda kukiwakilisha kitongoji hicho kwenye mashindano ya Kanda ya Temeke.
Aliongeza kuwa katika kusindikiza shindano hilo, bendi muziki wa dansi ya FM maarufu kama 'Wazee wa Ngwasuma' pamoja na msanii wa vichekesho Mpoko watatoa burudani ya aina yake katika shindano hilo.
Mratibu huyo kutoka kampuni ya K& L, aliwataja warembo wanaojiandaa kuwania taji hilo kuwa ni pamoja na Carolyne Dandu, Fatina Francis, Edda Slyvester, Aisha Mussa, Rosemary Peter, Doreen Kweka, Carolyne Peter, Agnes Goodluck, Sophia Martine, Rosemary Deogratius, Beatrice Boniface, Julieth Philip na Khadija Kombo.
Aliwataja wadhamini ambao tayari wamethibitisha kudhamini shindano hilo ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's, Dodoma Wine na NSSF,Hope country Motel, Norbro’s Collections, Screen Masters, Clouds FM, Times FM na Global Publishers.
Warembo watano watakaofanya vizuri watachuana na wenzao wa Chang'ombe kuwania taji la Kanda ya Temeke hapo baadaye.

No comments:

Post a Comment