b..

B1

Wynem

animation

Wednesday, January 10, 2018

COASTAL UNION WAKATAA UFADHILI WA WAZIRI JANUARY MAKAMBA

Mh. January Makamba
Mh. January Makamba akiwa kwenye moja ya mechi za ligi kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi wetu
Uongozi  wa timu ya Coastal Union ya Tanga(al maarufu Wagosi wa Kaya) umekataa ufadhili waliotafutiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano, January Makamba kwa madai kwamba kampuni aliyoitafuta kwa ajili ya ufadhili inajishughulisha na masuala ya Kamari.

Waziri Makamba alitafuta Ufadhili kutoka kampuni ya BIKO inayojihusisha na michezo ya kubahatisha ambayo ilikubali kuifadhili timu ya Coastal kwa kuingia nayo mkataba ambao utawezesha kulipa mishahara ya wachezaji pamoja na mahitaji mengine kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Makamba alisema lengo la yeye kukubali kuwatafutia ufadhili ilikuwa ni kutaka kuinua kiwango cha soka pamoja na kuipa nguvu ili  iweze kupanda daraja timu hiyo iliyoporomoka kisoka.

Akizungumza kwa simu na mwandishi wa habari hii, Waziri Makamba alikiri  kuitafutia ufadhili timu hiyo ambao ungewawezesha kulipwa mishahara na mahitaji mengine kwa kipindi cha mwaka mzima.

imefahamika kuwa uongozi wa Coastal Union umekataa ufadhili huo licha ya kufanyika mazungumzo ya awali kwa ajili ya kuingia mkataba.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa BICO, Charles Mgeta alisema kuwa taratibu za ufadhili zilikuwa zimekamilika na walipeleka fedha za awali zipatazo sh.15m/= kwa klabu hiyo kati ya fedha sh.50m/= zilizokubaliwa kwa matumizi ya mwaka mzima.
Mgeta alisema kwamba licha ya kupeleka fedha za awali pia walipeleka jezi 30 kwa ajili ya timu hiyo na kuahidi kutengeneza jezi 30 nyingine.

Ofisa Mkuu huyo alisema baada ya kutokea sintofahamu juu ya ufadhili huo kutoka CoastalUnion, kampuni ya BIKO imewataka viongozi wa klabu hiyo kurudisha fedha walizopokea kutoka kwao.

Hata hivyo, uongozi wa Coastal Union umethibitisha kupokea fedha zipatazo shs.15m= kutoka BIKO na kwamba wanachofahamu ni kwamba wanaendelea na mazungumzo na kampuni hiyo ili waweze kupata suluhu, ingawa hakufafanua zaidi.

Mwenyekiti wa Coastal Union, Stephen Mgutto alisema kwamba klabu yake ilipendekeza ipewe ufadhili wa shs. 50m/= badala ya shs. 30m/= ambazo walitajiwa.

Alieleza kuwa kushindwa kufikiwa muafaka wa shs.50m/= ulifanya uongozi wa klabu hiyo kutotaka kuendelea na mkataba na kampuni hiyo.

Katibu wa Kamati Maalum ya mashindano na Usajili, Salim Bawazir alisema kuwa Waziri Makamba amekuwa mfadhili wa timu hiyo kwa muda mrefu na alitaja baadhi ya misaada iliyotolewa naWaziri Makamba kwa Coastal Union kuwa ni pamoja na kugharamia kambi ya timu hiyo wakati wakijinoa  kwa muda wa majuma mawili kwa kutoa shs.2m/=.

“Mheshimiwa, ametugharamia kuweka kambi ambayo ilihusisha chakula na vitu vingine,  ambapo Mohamed Enterprises naye aliisaidia timu kwa kutoa vyakula vyenye thamani ya shs.2m/=”. Alisema Bawazir.

Makamba alisema kuwa ametumia karibu shs.6m/= kuisaidia timu hiyo kwa matumizi yao kuanzia mwaka jana.

“Nimewalipia mara kadhaa mahitaji yao yanayofikia shs.6m/=”, alisema Waziri huyo.

Alisema amesikia tetesi za mtafaruku baina ya viongozi kuhusu upokeaji wa msaada huo na kueleza kuwa amesikitika sana. "Iwapo msaada huo hauhitajiki, tutawapa wengine wanaohitaji”, alisema Makamba na kuongeza amekuwa akisaidia michezo kwa muda mrefu na mwaka jana alipewa ngao ya shukurani na timu ya Majimaji ya Songea kwa sababu aliwasaidia na wakafanikiwa.

"Viongozi hao wanajua kabisa kwamba mara kadhaa nimelipia mahitaji mbalimbali ya klabu ingawa kipato changu ni kidogo. Nimeenda kambini na kufanya mkutano na wachezaji kuhusu hali zao. Nikihesabu tangu mwaka jana ni fedha nyingi," alisema. 

Alieleza kuwa kuna kipindi timu ilipitia Iringa  na akalazimika kuwaomba marafiki zake wa Iringa wawapokee, kuweka mafuta na kuwapa chakula na malazi.

Alisema anatumaini kuwa mzozo huo utamalizwa kwa ustawi wa soka la Tanga.

Monday, August 21, 2017

RAIS JOHN MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA JCA NA BALOZI WA JAPAN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida leo agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.

NSSF YATOA MKOPO WA BILIONI 8.9 KUFUFUA KIWANDA CHA USINDIKAJI WA NAFAKA MWANZA

Mwanza, Agosti 20, 2017: Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF) limetoa mkopo wa Tshs bilioni 8.99 kwenda kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ya Tanzania kwa ajili ya ufufuaji wa kiwanda cha usindikaji wa nafaka katika jiji la Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za mfuko huo kutekeleza kwa vitendo sera ya uchumi wa viwanda hapa nchini.

Mkopo huo unalenga kuiwezesha Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kuweza kuvifufua vinu vyake viwili vya usindikaji wa mazao ya mpunga na mahindi vilivyopo mkoani humo kwa  kununua vifaa na mitambo mipya na hatimaye kuanza uzalishaji baada ya kusimamisha uzalishaji huo mapema miaka ya 1990.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya hundi ya mkopo huo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama alitoa wito kwa Wizara yenye dhamana ya kulimo hapa nchini kuisimamia vyema bodi hiyo kiutendaji ili iweze kuijendesha kwa ufanisi utakaoiwezesha kurejesha mkopo huo unaotarajiwa kulipwa ndani ya kipindi cha miaka sita (6) ikijumlisha kipindi cha mpito yaani (grace period) ya mwaka mmoja. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (wa pili kushoto) Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia) ikiwa ni mkopo kutoka Shirika hilo kwenda bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kwa ajili ya ufufuaji wa kiwanda cha usindikaji wa nafaka kilichopo jijini Mwanza. 

"Mbali na Wizara yenye dhamana ya kilimo, pia niwaombe sana uongozi wa mkoa wa Mwanza chini ya Mkuu wa mkoa kutambua kuwa ufanisi wa kiwanda hiki unategemea sana uwepo wa malighafi ya kutosha hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha uwiano kati ya uzalishaji wa malighafi na uzalishaji wa kiwanda vinakwenda sambamba,'' alisisitiza. 

Alilipongeza Shirika la NSSF  kwa uwekezaji wa viwanda vyenye tija kiuchumi ndani ya muda mfupi ambapo kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja uliopita hadi sasa shirika hilo limewekeza kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kiwanda cha kutengeneza viuadudu vya kuua vimelea vya mbu kiitwacho Tanzania Biolarvicide Limited kilichopo Kibaha, mkoani Pwani.

"Uwekezaji wa NSSF pia unaonekana kwenye bodi ya nafaka na Mazao mchanganyiko ya Tanzania, Mkoani Dodoma, viwanda vipya vya kuzalisha sukari Mkulazi, mkoani Morogoro, kiwanda cha chaki Maswa (Maswa Chalk & General Enterprises) ambacho kipo Simiyu...hongereni sana!'' alipongeza. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akikabidhi mfano wa hundi hiyo kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba (kushoto) huku wadau wengine wakishuhudia.

Waziri Mhagama alitumia wasaa huo pia kuwataka  waajiri wasiolipa michango ya wanachama kuwasilisha michango hiyo kwa wakati na kwa usahihi kwani  kutofanya hivyo ni kosa kisheria na  kuanwanyima haki wanachama hao huku akisisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa wale wasiotekeleza sharia hiyo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba alimuhakikishia Waziri Mhagama kuwa mbali na kuisimamia kwa ukaribu bodi hiyo ili iweze kurejesha mkopo huo, wizara yake imejipanga kuhakikisha kwamba miradi yote ya kilimo inayohusisha uwekezaji kutoka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii hapa nchini inasimamiwa kwa umakini, ufanisi na weledi mkubwa ili kulinda pesa ya wanachama wa mifuko hiyo.

"Kwa kutambua kwamba ufanisi wa viwanda hivi unategemea zaidi kilimo kuna mipango na mikakati mizuri kuhakikisha mnyororo wa thamani unaohusika kuzalisha malighafi za viwanda hivi haukatiki,'' alisema Waziri Tizeba.
Kabla ya makabidhiano hayo Waziri Mhagama alipata wasaa kukugua mitambo ya kinu cha kukoboa mchele kinachotarajiwa kufufuliwa kupitia mkopo huo ambapo Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko Bw. John Maige (mbele) alimuhakikishia Waziri Mhagama na wadau wengine kuwa kufufuliwa kwa kiwanda hicho kutawezesha jumla ya tani 96 za mchele kukobolewa kwa siku kupitia kinu hicho.

Alitaja baadhi ya mipango na mikakati hiyo kuwa ni pamoja na ujio wa Mpango maalumu wa kuandaa mbegu bora unaotekelezwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Bill Gates. Alikili kuwa kwasasa taifa linakabiliwa na uhaba wa mbegu bora unaotakona na utegemezi wa mbegu hizo kutoka nje ya nchi huku taifa likizalisha asilimia 35 tu ya mbegu hizo.

Waziri Tizeba alitumia fursa hiyo kutangaza uamuzi wa serikali kutoa bei elekezi kwenye pembejeo za mbolea ili kudhibiti uuzwaji kwa bei holela wa bidhaa hiyo muhimu ambapo kila mfanyabiashara alikuwa akiuza bidhaa hiyo kwa bei inayotokana na utashi wake.

"Mbolea zinahusika ni zile za kukuzia na kupandia yaani UREA na DAP ambapo kuanzia leo bei elekezi itakuwa inatangazwa kulingana na maeneo husika. Tunataraji kuwa uwepo wa bei elekezi utasaidia kupunguza bei ya mbolea hususani ya UREA kwa asilimia  zaidi ya 15 kwa mfuko,'' alisema.
Hatimaye hundi hiyo ikafika kwa Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko Bw. John Maige (wa tatu kushoto). Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba (wa pili kushoto), Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Bw. Stanislaus Mabula (katikati) na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia).

 Alitolea mfano kuwa katika baadhi ya mikoa bei ya mbolea ilifika hadi Sh. 100,000 lakini chini ya mfumo wa bei elekezi haitazidi sh. 56,000 kwa mfuko huku maeneo mengine ikiwa chini zaidi ya bei hiyo.

Mapema, akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara alisema kuwa mbali na lengo la kutunza thamani ya michango ya wanachama, uwekezaji unaofanywa na shirika hilo pia unalenga kuchochea ukuaji wa shughuli mbali mbali za uchumi na kijamii ambazo pia huongeza ajira, kipato na kuinua kiwango cha maisha ya watanzania walio wengi na mwishowe kuongeza wanachama wa mfuko.

"Mkopo huu utapelekea kufufua kiwanda ambacho kitaleta ajira Zaidi ya 340 za moja kwa moja na ajira zaidi ya 23,000 ambazo hazitakuwa za moja kwa moja.Hii itachochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania na pia kuongezeka kwa wanachama wa Mfuko,'' alibainisha. 
Muonekano wa sehemu ya mitambo ya kiwanda hicho cha kukobolea mchele kilichopo wilayani Nyamagana jijini Mwanza. 

Prof.Kahayrara alisisitiza kuwa Uwekezaji huo unafanywa kwa  kuzingatia Sera ya Uwekezaji ya Shirika na Mwongozo wa Uwekezaji kwa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii unaotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kushirikiana na Mdhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).

Akitoa taarifa za kiwanda hicho,Mtendaji mkuu wa  bodi ya nafaka  na mazao mchanganyiko ndugu  John Maige alisema  mkopo huu utaongeza kiwango cha usagaji wa mahindi hadi kufikia tani 250 kwa  siku na ukoboaji wa tani 96 za mchele kwa siku pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa vyakula vya mifugo kwa Masoko ya ndani na nje ya nchi.

 "Mkopo huu pia utawezesha kuwepo kwa soko la uhakika kwa wakulima wa mahindi na mpunga hapa nchi na nitumie fursa hii kuipongeza serikali kwa hatua ya kuzuia usafirishaji wa mazao ghafi nje ya nchi.'' alipongeza Maige huku akiongeza shukrani zake kwa Mfuko wa NSSF kwa uamuzi wa kuwekeza kwenye kufufua kiwanda hicho.
Na huu ndio muonekano wa kiwanda hicho kwa nje.
Na hapa ndipo kitakapojengwa kinu cha kusagia mahindi! Baada ya kukagua kinu cha kukobolea mpunga Waziri Mhagama na wadau wengine walipata wasaa wa kutembelea eneo lingine la kiwanda hicho ambapo kwa mujibu wa Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko Bw. John Maige ndipo kitakapojengwa kinu cha kusagia mahindi chenye uwezo kusaga mahindi hadi kufikia tani 250 kwa siku. 
Ukafika wasaa wa kufafanua mradi huo. Kwa mujibu wa Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko Bw. John Maige (aliesimama)mkopo huu utaongeza kiwango cha usagaji wa mahindi hadi kufikia tani 250 kwa siku na ukoboaji wa tani 96 za mchele kwa siku pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa vyakula vya mifugo kwa Masoko ya ndani na nje ya nchi. Vinu hivyo vinavyofufuliwa kwa mkopo wa NSSF vilisimamisha uzalishaji wake tangu mapema miaka ya 1990 baada ya kushindwa kujiendesha.
Ikawa ni pongezi tu kwa NSSF na Serikali kwa kufanya kile kilichoshindikana kwa miongo ya miaka!Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Bw Stanislaus Mabula akitoa shukrani zake kwa naiba ya wananchi wa jimbo hilo pamoja na wakazi wa Mwanza kwa ujumla. Pamoja na faida nyingine nyingi, kufufuliwa kwa kiwanda hicho kunatajwa kuwa kutazalisha ajira zaidi ya 340 za moja kwa moja na ajira zaidi ya 23,000 ambazo hazitakuwa za moja kwa moja.

Sunday, August 20, 2017

BONDIA SELEMANI SIMBA HAPANIA KUTOA KICHAPO KWA MABONDIA KUANZIA AGOST 26 VIJANA


Na Mwandishi Wetu
BONDIA wa ngumi za kulipwa kutoka Singida Selemani Simba 'Singida Unaited' amendelea na mazoezi ya kujifua kwa ajili ya mpambano wake wa Agost 26 utakaofanyika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni ambapo atapambana na Kallage Ramadhani bondia anaenolewa na kocha mkongwe katika ngumi Rajabu Mkamba

Akizungumzia mpambano wake Simba amesema kuwa amekuja Dar kwa ajiri ya kupambana na kuwapiga mabondia wote watakaopambana nae wakati wowote ule bondia huyo mpaka sasa kashapigana mapambano mawili kati ya hayo mawili kashinda moja na kudundwa moja

akizungumzia matarajio yake katika masumbwi amesema anatamani kufika mbali zaidi kama Ibrahimu Class 'King Class Mawe' walivyofanikiwa kufika mbali na mpaka sasa kuwa bingwa wa Dunia

katika mpamano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya ubingwa kati ya bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe'  na Baina Mazola 'Simba Mazola'
mapambano mengine ya siku hiyo ni sajo bosco Jr atakumbana na juma rashidi mdobi na Issa Nampepecha ataoneshana umwamba na Abbas Mwamba wakati Karim Ramadhani ataoneshana kazi na Yohana Dhobian na Keisii Amali atakuchiana ngumi na Hashimu Chisola na Said Wigo atazipiga na Chicho Ramadhani

Mapambano haya yote yatasimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC ambayo yenye dhamana ya kuendesha mchezo wa ndondi za kulipwa nchini

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile:-

Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez, Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi

Monday, August 14, 2017

Roma - Zimbabwe [Official Music VIdeo]

RAIS WA MISRI AWASILI NCHINI LEO KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI

Rais wa Jamhuri ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi akishuka kwenye ndege yake baada ya kuwasili nchini mchana huu, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Misri Mhe. Abdel Fattah el-Sisi akisalimiana na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili nchini hivi punde kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake,  Rais wa Jamhuri ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa J.K Nyerere, Jijini Dar es salaam mchana huu, ambapo atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili Agosti 14-15, 2017. 

Sunday, July 30, 2017

MABONDIA IDD MKWELA VICENT MBILINYI SELEMANI SIMBA NA ROLEN JAPHERT WAENDELEA KUNOLEWA NA SUPER D.

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwiu nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimnowa bondia Idd Mkwela anaeijandaa na mpambano wake wa Agost 12 katika ukumbi wa Manyara Park uliopo Manzese Dar Es salaam.

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwiu nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimnowa bondia Idd Mkwela anaeijandaa na mpambano wake wa Agost 12 katika ukumbi wa Manyara Park uliopo Manzese Dar Es salaam
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wa pili kutoka kulia akiwa na mabondia Selemani Simba Vicent Mbilinyi na Idd Mkwela
Mabondia Idd Mkela na Rolen Japhert wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi yanayoiendelea katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM Shule ya Uhuru Kariakoo Dar es salaam

KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM KARIAKOO 

KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KUSHOTO AKIWA NA MABONDIA SELEMANI SIMBA, VICENT MBILINYI NA IDD MKWELA BAADA YA MAZOEZI

Tuesday, July 25, 2017

WAZIRI LUKUVI AWEZESHA UJENZI WA MABWENI IRINGA


Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bibi Amina Masenza.
Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akiwa amevalishwa vazi la heshima la wazee wa kabila la Kihehe baada ya kuwezesha ujenzi wa Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akiwa amevalishwa vazi la heshima la wazee wa kabila la Kihehe baada ya kuwezesha ujenzi wa Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa mbele.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa nyuma.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa ndani.
Vitanda kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.
Vitanda kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.
Eneo la kunawia lililo ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.

………………………….

Na Hassan Mabuye

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ismani Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Japan amesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa kwa kiasi cha shilingi milioni 270.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Idodi Iringa Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida alisema kuwa misaada hiyo inatolewa kupitia kodi za watu wa Japan kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kimaendeleo nchini Tanzania.

Ubalozi huo wa Japan ambao umesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi umetokana na maombi ya mbunge wa Jimbo hilo la Isimani Mhe. Wiliam Lukuvi aliyoyaomba katika ofisi ya ubalozi kufuatia bweni la awali la shule hiyo kuteketea kwa Moto.

Balozi huyo alisema kuwa mkataba wa ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi Idodi sekondari ulisainiwa February mwaka 2016 kwa dolla za kimarekani 130,166 sawa na milioni 270 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo.

Ubalozi wa Japan nchini Tanzania umeahidi kuendelea kusaidia miradi mbali mbali ya kimaendeleo ndani ya mkoa wa Iringa na maeneno mengine hapa nchini ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli.

“waziri Lukuvi lileta maombi ya miradi mbalimbali ambayo miongoni mwake ni kujengewa Hostel ya wasichana ya shule ya Ismani ambayo ilijengwa toka mwaka 2005 na mwaka 2008, kujenga jengo la OPD na wodi ya wagonjwa katika zahanati ya Mlowa na mwaka 2010 kununua gari la wagonjwa katika zahanati ya Mlowa, kwa hiyo namshukuru Waziri Lukuvi kwa kusimamia vema miradi hiyo”

“Leo nimefurahi kuona ujenzi umekamilika kwa kiwango kizuri vitanda vya kutosha, mfumo wa kuhifadhi maji wa Hosteli hii umekamilika ikiwa na uwezo wa kulaza wanafunzi 208 kama kusudio la ujenzi, na ni matumaini yangu mradi huu utatunzwa vema”

Balozi huyo alisema kutokana na usimamizi mzuri walioufanya kampuni ya Koyo Corporation kampuni ya kijapani imetoa msaada wa taa zinazotumia nguvu ya mionzi ya jua kwa ajili ya kutumia wanafunzi wote watakaoishi katika bweni hilo.

Hata hivyo alisema ubalozi wa Japan nchini utaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania chini ya kauli mbiu ya hapa kazi tu.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza awali akimkaribisha balozi huyo alisema kuwa serikali ya mkoa inafurahishwa na msaada huo ambao umesaidia kupunguza msongamano ya wanafunzi bwenini na hivyo bweni hilo ambalo litatunzwa vizuri.

Waziri Lukuvi pamoja na kupongeza msaada huo wa kujengewa bweni na miradi mingine amewataka wanafunzi hao kutunza mabweni hayo na kujiepusha na hatari zozote za kuchoma moto, kitendo ambacho kinasababisha upotevu mkubwa wa mali na uhai wa wanafunzi hao.

Monday, July 24, 2017

Tundu Lisu afikishwa mahakamani leo Dar es SalaamIMG-20170724-WA0007.jpg


IMG-20170724-WA0008.jpg
Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lisu, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka yake ambayo bado haijawekwa wazi.
FB_IMG_1500896499844.jpg
Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lisu (mwenye fulana nyekundu) akiwa mahakamani.
FB_IMG_1500896506343.jpg
IMG_20170724_144943.jpg 
PICHA: Mawakili Peter Kibatala na Fatma Karume wakinena jambo mahakama ya Kisutu kabla ya kusikilizwa kesi ya mteja wao, Mbunge Tundu Lissu.


Thursday, July 20, 2017

RAIS NKURUNZINZA AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MOJA NCHINI TANZANIA

 
Rais wa Burundi aagwa rasmi baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini Tanzania. Ziara hii imefanyika katika Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera. Aidha Mhe. Rais Nkurunziza na mwenyeji wake Mhe. Rais John Pombe Magufuli wamehutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Posta mjini Ngara

Monday, April 24, 2017

SHEREHE YA UBATIZO WA MTOTO ROSELYN HENRY KAPINGA KATIKA UKUMBI WA VIP WANYAMA HOTEL SINZA.

Cake maalum kwa ajili ya Ubatizo wa mtoto Roselyn Kapinga iliyoandaliwa na Aunt Agnes Makwati ikiwa tayari kwa kukatwa.
Aunt Eva (Doto) akiwa amembeba Roselyn kabla ya kuanza tukio la kukata Cake.
Mama wa Kiroho Aunt Esther Mbapila akitoa zawadi ya Roselyn kwa mama Roselyn
Cindy Makwati akimlisha cake Mama Roselyn kwa niaba ya Roselyn huku baba Roselyn akishuhudia tukio hilo.
Cindy akijiandaa kumlisha cake Aunt Agnes ambaye ni mama yake.
Babu Roselyn naye hakuwa nyuma katika kusherehekea Ubatizo wa mjukuu wake. Mtoto Roselyn Henry Kapinga alipata Ubatizo siku ya Jumatatu ya Pasaka ya tarehe 17/04/2017 katika kanisa la Mt. Petro Oysterbay jijini Dar es salaam na baadae kufuatiwa na sherehe fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa ndani katika Hoteli ya Wanyama Sinza jijini Dar es salaam.