Na Mwandishi Wetu
WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012 jumamosi hii wanatarajiwa kutembelea makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kujifunza.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi huo wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkatabala na chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) Juni, 22 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano hilo Dina Ismail, alisema ziara hiyo itawasaidia sana warembo hao katika harakati zao za kielimu.
Alisema Makumbusho ya Taifa ni sehemu muhimu kwa kila Mtanzania kufahamu kutokana na kuwepo vitu vingi vya kihistoria vilivyopata kutokea katika karne zilizopita.
“ Kama mjuavyo kule kuna kuna fuvu la mtu wa kwanza duniani (zinjathropas), vyombo, magari na vitu vingine vya kwanza kuanza kutumika,”alisema.
Dina aliongeza kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo washiriki 13 kutoka vyuo vya IFM, Ustawi wa Jamii, Chuo Cha Biashara (CBE), uandishi wa Habari (DSJ) na Huria (OUT) wanaendelea na mazoezi kwenye hoteli ya The Grand Villailiyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Warembo hao ambao wapo chini ya ukufunzi Marlydia Boniface na Bob Rich ni pamoja naVeronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda,Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redd’s Original, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Shear Illusions, Skylight Band, Lamada Hotel,Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.
|
Thursday, June 14, 2012
MISS DAR INTER COLLEGE KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA J'MOSI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment