Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa Habari.
Na Mwandishi Wetu
Wakati
CCM inatimiza miaka 37 tangu kuanzishwa kwake Februari 5 mwaka 1977,
Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata
hasa katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa Watanzania, kutunza na
kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi
imara ya uchumi wa nchi.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa
mikutano CCM Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
alisema sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na zilizinduliwa rasmi
tarehe 26
na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein Unguja
Zanzibar.
Kilele cha sherehe hizi kitakua tarehe 2 Februari, jambo ambalo Nape amelifafanua
“Ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi hivyo tumeona tufanye tarehe
mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi waweze kushiriki”
Sherehe hizi zitahitimishwa jijini Mbeya kwenye uwanja
wa Sokoine na zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa CCM wameanza kuwasili na
kesho anategemewa kuwasili Makamu Mwenyekiti
wa CCM (Bara) Ndugu Philip Japhet Mangula ambaye pia ni mlezi wa mkoa wa Mbeya akitanguliwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu
Abdulrahman Kinana.
Nape alisema “Tarehe 2 asubuhi saa moja kutakuwa na
matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama, Rais
Jakaya Mrisho Kikwete matembezi hayo yatafanyika kwenye jiji la Mbeya yataanzia
eneo la Soweto na yataishia kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mbeya.
Baada ya matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine ambapo kutakuwa na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki wa kizazi kipya, sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya televisheni pamoja na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.
Baada ya matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine ambapo kutakuwa na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki wa kizazi kipya, sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya televisheni pamoja na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.
WanaCC waliopo mkoani Mbeya wameombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa
mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi tarehe moja na pia washiriki
kwenye matembezi na sherehe zitakazofanyika tarehe 2.
Maadhimisho ya sherehe hizi yataambatana na shughuli mbali
mbali nchini kote, ikiwa pamoja na shughuli za utunzaji wa mazingira kama kupanda miti, kushiriki shughuli za maendeleo
kujenga shule na zahanati, usafi pamoja
na kutembelea wagonjwa hospitalini.
No comments:
Post a Comment