SopRAnO alizaliwa tar 2 May 1985 Dar Group hospital Ilala Dar es salaam Tz.Ni mtoto wa pili kwenye familia ya watoto wa nne watoto wawili wa kike na wawili wa kiume.Primar school alisoma Yombo Primary school na baada ya kumaliza msingi alijiunga na sekondari Jitegemee high school na baadae kujiunga na chuo cha UCC University college of computer.Amekulia mitaa ya kiwalani kaliagogo kijiwe samli Ilala dar es salaam.Alianza kujishughulisha na muziki miaka ya tisini lakini akaanza kurekodi santuri yake ya kwanza iliyoitwa HOFU iliyofanywa na producer MANECKY studio za Midman Rec mwaka 2005.Lakini hakuitoa mwaka huo kutokana na kuwa bado hakumaliza shule,Mwaka 2006 baada ya kumaliza shule aliiachia santuri hiyo pamoja na video ya wimbo huo ulifanya vizuri ingawa haikuwa sana.Lakini ukampatia show za uhapa na pale.Mwaka 2008. akaachia wimbo wake mwingine ulioitwa MSHUMAA Nao pia haukufanya vizuri sana. Mwaka 2009 alikutana na Q Chief wakawa wanafanya album ya pamoja lakini cha kushangaza ndugu yake huyo akamgeuka kwa tamaa ya fedha akamtoroka mwezake na kwenda studio nyingine kurekodi wimbo wa TUTAONANA WABAYA na Kuitoa.Lakini SOPRANO hakukata tamaa nae akaifanya kipekee na kuitoa nyimbo yake ikiwa km jibu kwa q chief ikaitwa TUSHAONANA WABAYA ambayo ilifanya vizuri na kumfanya Soprano kujulikana kila kona ya bongo.Baadae akaachia wimbo mwingine uliokwenda kwa jina la SIMU YA TOCHI Na baade kuachia wimbo mwingine NASEMA GO Ambao unafanya vizuri kuanzia radio hadi tv kwa sasa na huyo ndio Francis Xaviery Ndumbaro a.k.a SOPRANO.
No comments:
Post a Comment