b..

B1

Wynem

animation

Tuesday, August 7, 2012

NAIBU WAZIRI WA AFRIKA MASHARIKI APATA AJALI MJINI KIBAHA AKITOKEA BUNGENI JIONI YA LEO.

Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Abdullah Juma Abdalla Saddallah na familia yake wamepata ajali mbaya eneo la Tumbi Kibaha wakati wakitoka Bungeni mjini dodoma leo jion.

Ajali hiyo mbaya ilitokea majira ya jioni hii wakati naibu waziri huyo akitokea Bungeni kuelekea jijini D'salaam akiwa na mkewe pamoja na watoto wake wawili na a dereva wake ambaye aliumia vibaya na kukimbizwa hospital yaTumbi-KibahaMashuhuda wa ajali hiyo akiwemno Abdulaziz Video amedai kuwa chanzo cha ajali hiyo inasemekana alikuwa analikwepa Lori alilokuwa akipishana nalo na hivyo gari lake kuhama njia na kupinduka .
Imeelezwa baada ya ajali hiyo umati wa wananchi wakiwemo vibaka walifika eneo hilo kutaka kupora mali mbali mbali ila hawakuweza kufanikiwa baada ya raia wema kusaidia kuepusha hali hiyo .
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo baada ya kuhojia na mwandishi wa habari hizi na kuwa hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva wake ambaye ameumia kichwani." 
Chanzo: Francis Godwinblog.

No comments:

Post a Comment