Tuombe msaada kuwasaidia wenzetu ambao ni
mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu...
Ninakuomba kama mtanzania mwenzangu tupeane hamasa ya kupendana na kusaidiana sio katika sherehe za starehe tuu, zaidi siku hizi tuzidishe kusaidiana katika shida maana sasa shida zinazidi siku hadi siku.
Katika pitapita zangu, nimekutana na mtoto huyu Abdully mwenye ulemavu wa viungo huko Kaole, Bagamoyo. Kula kwake kwa taabu, haongei, ingawa anacheka akifurahishwa, na kulia kwa kupiga kelele akiudhiwa au akiwa na maumivu ingawa hawezi kuelekeza maumivi yako wapi.
Cha kusikitisha, mama yake mzazi amemkimbia mtoto na mume, baba nae ameanza kukata tamaa ya mwanae kwa kukosa muelekeo na msaada (support). Baba (Bw. Hamoud) anaishi na mama yake mzazi ambaye ni mtu mzima mwenye matatizo ya kiafya, macho na thyrod eshafanyiwa upasuaji nk... sasa Bw Hamoud ameacha shughuli za kutafuta fedha za kukimu maisha ili aweze kumlea kijana Abdul (4) ananza asubuhi kwa kumuosha, kumlisha kifungua kinywa..... mchana kumlisha anakula kwa taabu maana ulimi hauzunguki sawa sawa kama vile umepooza, na koo halimezi vizuri.... jioni anamsafisha na kumlisha.... maisha yamekuwa duni, kwa hivyo hata malezi ya Abdul yamekuwa magumu mno...
Alishauriwa ampeleke hospitali ya CCBRT, nae baada ya kwenda hapo alishauriwa ampeleke kwa physiotherapy kila wiki, tatizo la Bw Hamoud ni usafiri kutoka Kaole hadi msasani CCBRT ni wa daladala na mtoto mwenye ulemavu wa viuongo si mchezo... mlemavu wa aina hii anaweza kuwa na haja kubwa au ndogo mahali popote wakati wowote hata mkiwa ndani ya daladala huduma yake ngumu hapo ni mtihani...
Hapo CCBRT wanaweza kushinda kutwa kabla ya kupata huduma kipindi hicho cha kusubiri mtoto amebebwa au kupakatwa, chakula hakuna, na pahala pa kumlaza aweze anaglau kunyoosha viuongo hakuna. wahudumu wanapita na kumuangalia hapo katika foleni bila kumpa tamaa au hata nasaha. Jioni usafiri wa wa kubanana ndani ya daladala kurudi Bagamoyo, pikipiki hadi Kaole.... Baba Abdul kaishiwa nguvu ameshindwa. Wapo Kaole wanasubiri hatma ya Mwenyezi Mungu.
Abdul amepewa ki "baiskeli" cha mtoto (push chair) na akiwekwa hapo lazima afungwe na khanga ndio akae kwa usalama na kwa sasa anabanwa hapo....
Hivyo basi Kama kuna wasamaria
wenye huruma na hali hii, wanaomba:
1. Wheelchair ya kawaida Abdul akae
kwa usalama na awe na nafasi viungo viwe huru
2. Ushauri kwa kiafya
3. Ushauri wowote, na msaada wowote
utakaoweza kutoa afueni kwa Abdul na baba yake Hamoud
mpigie simu Hamoud
+255 757 652449 na +255 787 771566
kwa msaada au ushauri. Juhudi za kufungua
akaunti maalumu zinafanywa kwa wenye
kutaka kumsaidia mtoto Abdully
Mdau Dar
No comments:
Post a Comment